Nauliza: TBC1 Wana bifu gani na CHADEMA?

Kwa uelewa wangu wa kawaida, TBC1 ni kituo cha matangazo kinachomilikiwa na umma. Nadhani haihitaji darasa kubwa sana kutambua umma ni upi na wapigakura ni kina nani. Kwa kuwa TBC1 ni ya umma basi inapaswa iwatumikie wote na si kubagua na kutengeneza makundi.

Nimeangalia kwa muda sasa kituo hiki, kwa kweli wamejitahidi kwa kiasi fulani kutoa habari nzuri, yaani ni kwamba taarifa yao ya habari kwa sasa inaangalika vizuri sana. Kwa upande wa 'bifu' na chadema hapa sasa ndo unapoweza kuanza kuona udhaifu mkubwa wa TBC1 na si kwa chama hiki tu ukikilinganisha na CCM bali ni kwa vyama vyote vya kisiasa na hata asasi za kiraia zenye msimammo mkali dhidi ufisadi, mara nyingi hapa kuna kufumba macho kwa TBC1.

Ukiangalia vituo vya tv na hata redio vinavyomilikiwa na umma katika mataifa hasa yaliyoendelea, utagundua kuwa umma kwanza na kisha chama, umma unapaswa uhabarishwe habari zote na si za watu fulani kana kwamba wao ndo wenye mamlaka na kiuo hiki.

Tido ni mtu makini na amesaidia sana kubadili aina ya utangazaji hapo TBC1 lakini bado kuna kitu kinamkaba na hasa ukikumbuka suala la kutorusha hotuba ya Slaa wakati wa kipindi cha bunge lililomalizika hivi karibuni, sitaki kusema kuhusu hili kwani wamekwisha liombea msamaha lakini kwangu mimi ni ushauri wa bure tu kuwa umma ndo unapaswa kutumikiwa na si kujipendekeza kwa vyama, au kitundi cha watu.

Watu tunataka kuona habari za pande zote na si kutulisha majni kwa habari za upande mmoja



UMMA NDO UNAAMUA
 
Kwa demokrasia za Afrika... nasubiri kuona siku ambako vyama vya upinzani vitasema vyombo vya habari vya serikali havipendelei chama tawala... Nasubiri sana kuona hilo.
 
sasa hawa CHADEMA si wanayo FREEMEDIA sasa wanaona tabu gani ku utilize kwa ajili ya faida yao?



Mkuu,

Acha upotoshaji,kwa hiyo wataka kusema au kulinganisha TBCI na Freemedia? Kwanini badala ya TBCI usiweke radio uhuru?
 
Its known clearly kwamba TBC is for the nation.Hata hawa ze comedy walioanza sijui kama wataendeleza makeke yao.Lets see.
 
Back
Top Bottom