Nauliza: TBC1 Wana bifu gani na CHADEMA?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini ni mfuatiliaji wa masuala ya siasa na ni mwanademokrasia na ni muumini katika haki na usawa na napenda kuona wanasiasa na vyama vyotevya siasa vinatendewa haki katika masuala ya siasa.

Kifo cha Mpambanaji Wangwe aliyekuwa Mbunge wa Tarime kiligubikwa na utata mkubwa sana huku Wanasiasa wa vyama vyote wakishutumiana kuhusiana na kifo hicho kwa minajili ya kujijenga kisiasa na kukitumia kifo hicho kujijenga kisasa huko Tarime kama tunavyosikia yanayoendelea huko Tarime kwenye kampeni kwenye Jimbo hilo.

Vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa mchango mkubwa katika kutujuza yaliyotokea wakati wa kipindi cha msiba wa Wangwe na chombo cha TBC1 hakikuwa nyuma maana walipeleka timu yao huko Kimokorere kwenye msiba na ingawa TBC Radio (pamoja na baadhi ya magazeti) ili-ripoti mambo yaliyokuwa yakitokea huko kwa namna ambayo haikukifurahisha CHADEMA maana taarifa za chombo hicho cha umma zilioneka kutokuwa fair na CHADEMA na baadhi ya wadau mimi miongoni mwao nilishangazwa na jinsi TBC Radi walivyokuwa wakiripoti mambo yaliyokuwa yakijiri huko na kupelekea CHADEMA kuwasilisha malalamiko katika Jukwaa la Wahariri wakida baadhi ya magazeti yaliripoti habari za matukio ya Tarime kwa kupotosha na kwa kuichimba CHADEMA na hatimaye JUkwaa la Wahariri kuunda tume kuchunguza tuhuma hizo za CHADEMA.

Baada ya Kampeni za Uchaguzi wa Ubunge na udiwani kuanza huko Tarime vyombo karibu vyote vya habari viliendelea kutupasha juu ya mambo yanayojiri katika kampeni hizo ambazo kwa mujibu wa habari hizo Kampeni hizo zimetawaliwa na vurugu kubwa na faulo kubwa kutoka pande zote zinazoshiriki uchaguzi huo.

Mwezi Septemba (baada ya kampeni za uchaguzi kuanza) TBC1 walimkariri Mjane mmojawapo wa Marehemu Wangwe: Mariam Wangwe akiituhumu CHADEMA kuwa imeitelekeza familia ya Marehemu Wangwe na hakikushiriki kwenye Arobaini ya Marehemu na akimtaka Spika Sitta kuunda tume ya BUNGE kuchunguza mazingira ya kifo cha Wangwe.

Siku chache baada ya taarifa hiyo, TBC1 tena wakawakariri baadhi ya viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Dar es salaam wakikituhumu chama chao na kuhusiana na kifo cha Wangwe! TBC1 kwa makusudi au kwa kutokujua kuwa CHADEMA hawana kitu kinachoiutwa Mkoa wa Dar es Salaam katika safu yao ya Uongozi wakaipa umuhimu mkubwa taarifa hiyo, wakiiweka kando kauli mbiu yao nzuri ya TBC1 "Ukweli na Uwazi".

Nachokiona mimi ni kuwa TBC1 ama ina bifu na CHADEMA au inawapotosha kwa makusudi kabisa Watanzania kwa kujaribu kuwaambia Watanzania kuwa CHADEMA si chama makini hapa nchini; TBC 1 imekubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kwa manufaa ya wanasiasa hao ili kukipaka matope CHADEMA kwa manufaa ya watu au kikundi hicho. TBC1 ni vema wakumbuke kuwa wao ni chombo cha Umma kinachoendeshwa kwa kodi za Watanzania wote wa vyama vyote vya siasa na ya kuwa wanapaswa kuvitendea haki vyama vyote vya siasa maana hakuna chama kilicho bora cha siasa vyote viko sawa. TBC1 ni kama vile hatuambii chochote kuhusu Kampeni za Uchaguzi Tarime badala yake wanatafuta na kuzipa uzito habari zinazoiumiza CHADEMA tu!

Badala yake nashauri TBC1 waige kutoka ITV ambacho kimuundo kingeweza kabisa kuwa biased kwa kufuata mapenzi ya mmliki wake ambaye ni mtu binafsi lakini kwa kutambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuuelimisha umma kinatujuza habari za Kampeni za Tarime kwa umakini mkubwa kwa kutoa habari ambazo ziko fair kwa vyama vyote.

TBC1 kama wanashindwa kutoa habari zilizo fair kwa vyama vyote ni heri wakae kimya kabisa kuliko kucheza mchezo ambao sisi Watanzania tutakuja kuwahukumu iwapo habari wanazotoa ambazo kwa kiasi kikubwa ziko biased zitapokuja kuwa sehemu ya vurugu zinazotokea au zitazotokea kati ya Wanachama wa CHADEMA na Watawala.

Kwa kuwa habari walizotoa TBC1 kweye taarifa zao mwezi Septemba zililenga kuikandamiza CHADEMA kwa faida ya Vyama vingine vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Tarime kwa makusudi au kwa bahati mbaya (isingekuwa bahati mbaya kama TBC1 wangefanya utafiti wa tuhuma hizo kabla ya kuzirusha na kujua malengo ya wanaoituhumu CHADEMA kwa kuzingatia kuwa hiki ni kipindi cha kampeni za Uchaguzi TaRIME).

TBC1 wangeweza kukaa kimya kabisa kama walivyfanya Jukwaa la Wahariri walioamua kuikalia ripoti yao kuhusu madai ya CHADEMA kwa kuhofia kuwa ripoti hiyo inaweza kutumika na baadhi ya vyama kujipatia umaarufu dhidi ya vyama vingine.

TBC1 Jirekebisheni.
 
kwani TBC1 ni ya nani?
Hao wamiliki wa TBC1 si kila kukicha wanashambuliwa na CHADEMA na hao wao shambuliwa wanajibu kwa kupitia TBC1 kama Mtikila vile.....
 
kwani TBC1 ni ya nani?
Hao wamiliki wa TBC1 si kila kukicha wanashambuliwa na CHADEMA na hao wao shambuliwa wanajibu kwa kupitia TBC1 kama Mtikila vile.....

Kama wangetaka kujibu mashambulizi wanastahili kutumia vyombo vyao vya habari kama gazeti la Uhuru na radio uhuru. Lakini pale unapotumia vyombo vya habari vya serikali kwa manufaa ya chama kimoja cha siasa, ni makosa makubwa!
 
Jeshi la polisi Tanzania , TV ya Tanzania na Zanzibar, Makampuni ya Umma , JWTZ, Usalama wa Taifa woooooooooooooooooooote ni sehemu ya CCM na lazima wafanye wawezalo kuisaidia CCM hawajui na wala hawaamini katika mabadiliko .
 
Nadhani shida ya TBC 1 ni kwamba bado kuna ile mentality ya u-CCM. Nilipokuwa bongo mapema mwaka huu nilikaribishwa kwenye sherehe zao za kuzinduliwa kwa TBC (from Radio Tanzania na TVT) Katika hafla hiyo nilishangaa kuona professionals wakijiona wao ni CCM kwanza na watangazaji, waandishi habari baadaye. Kwa hiyo sishangai kabisa kwani wanajiona ni chombo cha CCM.
 
Nadhani shida ya TBC 1 ni kwamba bado kuna ile mentality ya u-CCM. Nilipokuwa bongo mapema mwaka huu nilikaribishwa kwenye sherehe zao za kuzinduliwa kwa TBC (from Radio Tanzania na TVT) Katika hafla hiyo nilishangaa kuona professionals wakijiona wao ni CCM kwanza na watangazaji, waandishi habari baadaye. Kwa hiyo sishangai kabisa kwani wanajiona ni chombo cha CCM.

Hii kali kweli kweli.
Mimi ni mpenzi wa kuangalia TBC1, hasa taarifa zao za habari. Lakini mmmhh wamesimamia zaidi upande serikali...and therefore CCM.

Sasa hivi kinadharia TBC ni shirika la umma. Kivitendo bado. Virusi vya CCM vimeshajipenyeza. Anti-virus iko bungeni.
 
Kama unafuatilia ya siasa bongo utagundua vyama vingi vya siasa vinaendeshwa na vyombo vya habari magazeti au majukwaa ya mtandao wanasiasa wanasoma magazeti na maoni ya wengine ndio wapate cha kusema wanapoongea na wananchi wao haswa chadema wao hawana cha kuongea hawana mpya
 
Kama unafuatilia ya siasa bongo utagundua vyama vingi vya siasa vinaendeshwa na vyombo vya habari magazeti au majukwaa ya mtandao wanasiasa wanasoma magazeti na maoni ya wengine ndio wapate cha kusema wanapoongea na wananchi wao haswa chadema wao hawana cha kuongea hawana mpya

Wawe na jipya ili iweje?
Unafikiri watu hawana akili timamu walete mapya tu wakakti bado yale yaliyotufikisha hapa bado hatujayashughulikia?
Hata dawa zenye kutibu kuna timig ya dosage na si kubugia tu ukidhani utapona...Acha wananchi wa absorb.....Wanaelekea kuujua ukweli na wakiupata mtakwisha...
Naamini kama chadema na wao wangekuwa wanamiliki dola kama ccm basi tungekuwa na mengi mapya.
Wananchi sasa ni wakati wao wa kureact na si kusubiri jipya na huku they are actually doing nothing.
Sasa tunasubiria kuona reaction ya wananchi hao mara baada ya kuwekewa ukweli wazi....La sivyo umasikini utaendelea sana tu na hatma ya Taifa letu itazidi kuwa uncertain.
 
TBC si ya Serikali ya CCM ama?So what is there to be expected?
 
Kama unafuatilia ya siasa bongo utagundua vyama vingi vya siasa vinaendeshwa na vyombo vya habari magazeti au majukwaa ya mtandao wanasiasa wanasoma magazeti na maoni ya wengine ndio wapate cha kusema wanapoongea na wananchi wao haswa chadema wao hawana cha kuongea hawana mpya


Mkuu,

Mbona wewe hujawahi kuwa na jipya hapa JF?
 
TBC si ya Serikali ya CCM ama?So what is there to be expected?
Kevo,
Ninavyoelewa mimi TBC is supposed to be an independent agency although supported by taxpayers money. Otherwise wangeziacha ziendelee tu kama RTD na TVT ambazo zilikuwa vyombo vya serikali. Hata kwenye sherehe za uzinduzi rais Kikwete alisema hivyo. BBC and VOA are government supported but they are independent by nature. Nadhani ndilo lengo la kuunda TBC. Sasa kazi iliyopo ni kubadilisha mindset ya viongozi wa TBC, board of governors, kuwa TBC si chombo cha CCM.
 
Hivi CHADEMA na FREEMAN MBOWE bado ni relevant ?

Sina hakika, maana kwa ushahidi Ze Comedy walilipwa na Manji watoke EATV waende TBC1 sasa sina hakika kama Manji ndiye mmiliki wa TBC1 ama anaifadhili kama anavyoifadhili CCM, NCCR-MAgeuzi na DP kule Tarime!!!!
 
sasa hawa CHADEMA si wanayo FREEMEDIA sasa wanaona tabu gani ku utilize kwa ajili ya faida yao?
 
sasa hawa CHADEMA si wanayo FREEMEDIA sasa wanaona tabu gani ku utilize kwa ajili ya faida yao?

Mkuu hapa umenena, watumie Freemedia kama ambavyo CCM, DP, NCCR-Mageuzi wanavyotumia TBC1, Uhuru, Majira, Habari Leo, Asumini, Dira Tanzania, Hoja, Mtanzania (japo sasa wameanza kuzinduka)
 
Nadhani wengi wetu tumesahau yaliyotokea Kenya wakati wa uchaguzi hata pale Mzee Kivuitu alipotaka kutangaza matokeo ya uraisi alipozongwa akakimbilia chumba kingine akawaita KBC(ya serikali) wengine wakaachwa nje akatangaza matokeo na yaliyotokea wote tunafahamu.


Labda wapinzani waanzishe TV yao kwani zilizopo zinaogopa rungu la CCM kuwashukia(rejea kauli ya Fisadi Sumaye "Mfanyabiashara Mwenye kutaka mambo yake yamnyookee awe CCM")


Kaaazi kwelikweli TBC Tido na Mungi wanakazi kubwa na CCM
 
Mkuu hapa umenena, watumie Freemedia kama ambavyo CCM, DP, NCCR-Mageuzi wanavyotumia TBC1, Uhuru, Majira, Habari Leo, Asumini, Dira Tanzania, Hoja, Mtanzania (japo sasa wameanza kuzinduka)
You are missing the point. TBC is funded by our money. We should all be able to utilize it in a free and open society. And as far as I know Chadema has no tv.
 
Back
Top Bottom