Nauliza hiviiiiiiii Kiti Moto ni....

attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
 
Daa nimeshakamua kilo baada ya kutoka masijidi, hii si haramu wakuu, kama ni haramu kwa nini Mungu aliumba hii kitu? Hizi ni imani tu, utaacha kula kitimoto kama unallergy nayo au kama ina sumu ambayo inaua.
 
Huku kutamanishana sio kabisa sie wengine wa huku tunamiss mapishi yake hasa ile ya Mbeya kule, unaweka ndizi, viazi na mboga za majani as extra duh udenda tayari mwenzenu
 
Waungwana salamu
Jamani nakwazika miye, Eti Kiti Moto ni ruksaaaaaaaaaaa na kama ni ruksaaa ni kwa dini zote? Nasika waislamu hawali lakini nawaonaga kitaa wakijipiga na ze kitis. Wakristu wao wanakulaga tena bila kificho. Je huyu jamaa ni kweli ruksa?


1. Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2. mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
3. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
4. Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
5. Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro.
6. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.
7. Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtauwa katika wale waliomhudumia daima;
8. na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yafa.
9. Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;
10. akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,
11. akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;
12. ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.
13. Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.
14. Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.
15. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.
16. Jambo hili likatendeka mara tatu; kisha kile chombo kikapokewa tena mbinguni.
17. Hata Petro alipokuwa akiona shaka ndani ya nafsi yake, maana yake ni nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiisha kuiulizia nyumba ya Simoni, wakasimama mbele ya mlango,
18. wakaita; wakauliza kwamba Simoni aitwaye Petro anakaa humo.
19. Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.
20. Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma.
21. Petro akawashukia wale watu, akanena, Mimi ndiye mnayemtafuta. Mmekuja kwa sababu gani?
22. Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mchaji wa Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno kwako.
23. Akawakaribisha wawe wageni wake. Hata siku ya pili, Petro akaondoka akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yafa wakafuatana naye.
24. Siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, hali amekusanya jamaa zake na rafiki zake.
25. Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia.
26. Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu.
27. Na katika kusema naye akaingia ndani, akaona watu wengi wamekusanyika.
28. Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.
29. Kwa sababu hiyo nalikuja nilipoitwa, nisikatae; basi nawauliza, ni neno gani mliloniitia?
30. Kornelio akasema, Siku tatu zilizopita, katika saa ii hii, yaani saa tisa, nilikuwa nikisali nyumbani mwangu; nikamwona mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zing'arazo,
31. akasema, Kornelio, kuomba kwako kumesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.
32. Basi, tuma watu kwenda Yafa, ukamwite Simoni aitwaye Petro, anakaa katika nyumba ya Simoni, mtengenezaji wa ngozi, karibu na pwani; naye akija atasema nawe.
33. Mara nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Basi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Bwana.
34. Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
35. bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
36. Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),
37. jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana;
38. habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
39. Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini.
40. Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika,
41. si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.
42. Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu.
43. Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.
44. Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
45. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.
46. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu,
47. Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
48. Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.
 
Tatizo la pale B bar hawapo shap alafu mapishi yao sio mazuri na ule mzani wao haupimi vizuri.

hahaaaa mdau mwenzangu, kumbe jirani, hiyo ni kweli aisee, wanachelesha sana, ila siku hizi nimegundua kitimoto nyingine pale Shekilango jirani na Sansiro CLub, open space, ila shida mvua.
daaah naandika mate yamejaa mdomoni.
 
Swala sio aleji tu, kale kamnyama kametulia bwana...hahaaaa, kipindi fulani nilikuwa nafanya kazi pale makambako Iringa, basi wale watu ni wazuri kweli yaani buku tatu unaambiwa chagua mwenyewe; maini, mbavu, moyo, steki au nini....kule unavyoona mjini hapa wanachoma mahindi na kuuza kule ni Kitimoto mtu wangu...hah hahhaaaa utapenda. Mbona nilinenepa.

MUHIMU: Ni dawa kwa wagonjwa wa HIV hasa yale mafuta yake
 
hiyo ruksa mmiku yani hapa ushanitamanisha naona jpili mbali ss kwann umeleta hoja hii

mimi mwenyewe nilikuwa sina mpango sasa amenisababisha niunde safari ya kwenda kukitafuta.....sio vizuri ujue wewe eeka mangi
 
Ni katamu bwana....ila usiwaambie hawa ndugu zetu; waislamu na wasabato...watatumalizia...tuendelee kuwadanganya kuwa ni Sumu sio haramu tu bali pia ni sumu......imekula kwaoooooo
 
Swala sio aleji tu, kale kamnyama kametulia bwana...hahaaaa, kipindi fulani nilikuwa nafanya kazi pale makambako Iringa, basi wale watu ni wazuri kweli yaani buku tatu unaambiwa chagua mwenyewe; maini, mbavu, moyo, steki au nini....kule unavyoona mjini hapa wanachoma mahindi na kuuza kule ni Kitimoto mtu wangu...hah hahhaaaa utapenda. Mbona nilinenepa.

MUHIMU: Ni dawa kwa wagonjwa wa HIV hasa yale mafuta yake

Hapo kwenye Red Mkuu yawezekana kweli Maana kule Makete yule Mdudu huwa anatolewa ile Ngozi ya Nje halafu inauzwa Separately halafu nasikia ile Ngozi yenyewe ni deal kuliko hata ile Steki ha ha haaaaaaaaaaa
 
Ni katamu bwana....ila usiwaambie hawa ndugu zetu; waislamu na wasabato...watatumalizia...tuendelee kuwadanganya kuwa ni Sumu sio haramu tu bali pia ni sumu......imekula kwaoooooo

hahaaaa, nimecheka sana hayo maneno yako, Kiti moto inasifa moja, ukionja kutoka ni kazi, aisee .
 
Hapo kwenye Red Mkuu yawezekana kweli Maana kule Makete yule Mdudu huwa anatolewa ile Ngozi ya Nje halafu inauzwa Separately halafu nasikia ile Ngozi yenyewe ni deal kuliko hata ile Steki ha ha haaaaaaaaaaa

jamajamani, jamani, jamani, mnajiandalia kupanda kwa demand kisha itasukuma bei kwenda juu wakati supply iko constant.
 
Mnajua kweli nimeona tunafanya makosa; unajua tunachofanya hapa tunai-promote tena bureeeee, halafu hawa jamaa wataacha kapande bei bwana, wale jamaa kule makete ni kweli yaani eti ngozi ni bei kuliko steki, bei ya steki kwa kilo ni buku 2500 hadi 3000 kwa baadhi ya sehemu tena kitu orijino hakuna sindano wala mchina

Shemeji yenu alikuja kunitembelea siku hizo nipo Makambako mbona aligoma kurudi hapa bongo.

Jamani, ndugu zetu wamekosa jambo
 
ok, nice weekend

Mkumbuke kwenda Kuabudu after all these jokes...
 
Jamani karibuni kwa chotta banana kipo cha kuchoma kwa gesi ni balaa.
ANGLES PUB aka Chotta, bar hiyo nayo inatatizo la wateja wengi, nilikua na piga misele maeneo hayo wakati nikiwa mwalimu wa Kemia pale Airwing sekondari, Chatta yuko pale tangu miaka ya 90 mwishoni, nakumbuka kilikua kijiwe changu, naamini banana ndio eneo linaloongoza kwa kuuzwa kitimoto nyingi kuliko eneo lingine lolote, maana kuna bar zaidi ya 20 pale nyuma, mpe salaam Chota na wahudumu woote pale , kina Reheme , kashinde , swahiba, kama bado wapo. daaah umenikumbusha mbaali sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom