Wadau nimeishi mjini zaidi ya miaka 20 lakini barabara naiogopa, ajali naziogopa usipime sasa najiuliza hawa vijana wetu waliojiajili kwa kuendesha bajaji na bodaboda sheria za usalama barabarani wanazijua kweli kama waendesha vyombo vya moto.? Nahofia sana manake siku za karibun kumezuka wimbi kubwa la vijana wa kijiweni kuendesha hivi vyombo wapo ninaowafahamu nina uhakika hawana leseni. Sielewi upande wa trafik hususan hili swala kwao wanalichukuliaje.