Nauli za daladala kupanda Dar

Mafuta yamepanda sana!
Alafu Hute una uhakika wananchi waliichagua CCM?
Kitendo cha kuchaguliwa rais na bado wakakaa kimya kama watapigiga hawatapiga kura na kwenda kuburudiaka watalinda kura zao mapaka siku ya matokeo
 
Mna mwone habari inaweza kuanza na tetesi halafu kukatokea na mtu anae lifahamu jambao hilo vema aka-confirm sasa mkianza kumsakama hivyo ina maana neno tetesi hapa JF halina maana.....au siku hizi tetesi hazitakiwi hapa JF....

mara nyingi tetesi za jf hugeuka kuwa kweli
 
wewe ndio umeleta habari halafu unadai sisi ndio tukujuze? we vipi, mwongo mkubwa!

mkutano uko scheduled for the 7th, Jan
Pasco............Nadhani maana ya TETESI hujui ndiyo maana umemwita muongo.
 
Wananchi watakumbwa na maumivu mengine baada ya bei ya umeme kuongezwa kwa asilimia 18.5 kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu kufuatia serikali kupandisha nauli za mabasi.
Safari hii Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesema kuwa inatarajia kutangaza viwango vipya vya nauli nchi nzima kuanzia Januari 31, mwaka huu.
Hayo yalibainishwa jana na Meneja Ufundi na Usalama Barabarani wa Sumatra, Aaron Kisaka, katika kikao cha pamoja cha wadau wa usafirishaji Mkoa wa Tanga kuhusiana na mapendekezo ya viwango vipya vya nauli.
Kisaka alisema hatua hiyo inafuatia maelekezo ya Sheria ya Sumatra namba 13 inayoruhusu mamlaka hiyo kutafuta maoni, habari na kufanya uchunguzi wa viwango vipya vya nauli vinavyoweza kutumika kwa maslahi ya wasafiri na wasafirishaji.
Alisema utaratibu wa Sumatra katika kubadili viwango vipya vya nauli unafanyika mara moja kwa mwaka au pale ambapo faida juu ya mtaji inakuwa chini ya asilimia tano au chini ya asilimia 25.
“Mpaka kufikia mwisho wa mwezi Januari, Sumatra itakuwa imetangaza viwango vipya vya nauli, lakini ikumbukwe kuwa viwango hivi vinazingatia pia ubora wa miundo mbinu ya barabara husika,” alisema Kisaka.
Kwa upande wao, wadau wa usafirishaji wa Tanga waliohudhuria kikao hicho ambao ni Muungano wa Wasafirishaji Abiria Tanga (Muwata) na Umoja wa Wenye Mabasi Mkoa wa Tanga (Taboa), walisema kuwa ombi la kutaka kubadili viwango vya nauli ni kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji katika utoaji huduma.
Wasafirishaji hao walisema kuwa wamekuwa katika wakati mgumu kumudu mfumo wa utoaji huduma kutokana na kupanda maradufu kwa bei ya mafuta siku hadi siku, kuongezeka kwa bei ya vipuri, soko huria la vyombo vya usafirishaji sambamba na upandaji holela wa kodi mbalimbali nchini.
Akisoma taarifa ya Muwata kwa niaba ya wenzake, Kaimu Mwenyekiti wa Muungano huo, Hatwabi Shabani, alisema kuwa kiwango cha nauli mpya kilichopendekezwa kitakuwa ni kiwnago cha juu katika utozaji wa nauli ambapo viwango vya chini vipo na vitaendelea kuwepo kutokana na fursa na ushindani wa kibiashara.
“Fursa ya utozaji nauli chini ya kiwango pia itatokana na umbali, maafikiano na makubaliano ya kondakta na abiria wake ili mradi nauli isivuke kiwango kilichoridhiwa na mamlaka …matumaini yetu ni kuboresha huduma ya usafiri iwe endelevu ili kuwezesha wananchi kufanikisha shughuli za kiuchumi na kijamii,” alisema Shabani.
Hata hivyo, wasafirishaji hao walisema tathmini hiyo ya bei mpya za nauli imefanywa kwa mtazamo wa kupanda kwa gharama za mafuta kwa kukadiriwa kufikia Sh. 2,000 kwa lita.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dk. Ibrahim Msengi, akifunga kikao hicho, aliwataka wasafirishaji wa Jiji hili kutambua kwamba sehemu kubwa ya uchumi wa nchi hutegemea usafiri hasa kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Dk. Msengi alisema katika kulitambua hilo, ndio maana serikali ikaona umuhimu wa kuwakutanisha wadau wa usafiri na mamlaka husika kabla ya kufanya maamuzi yoyote ili kutoa ushiriki wa mawazo kwa kila upande ikiwemo mtoaji na mpokeaji huduma.
“Serikali inathamini sana mchango wenu wasafirishaji na ndio maana ikaona si busara kufanya maamuzi peke yake bila kuwashirikisha kwani nia ni kuona mtoaji huduma anafaidika na kile anachokitoa, lakini pia anayetumia huduma hii ambaye ni Mtanzania anaipata bila vikwazo lengo ni kuleta ufanisi katika utendaji na utekelezaji,” alisisitiza Msengi.
Tangu Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) ilipoliruhusu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mwezi uliopita kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.5, wananchi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa hatua hiyo itawaathiri kimaisha.
Hata hivyo, pamoja na malalamiko hayo, serikali ikisema uamuzi huo haukwepeki kwa lengo la kuiwezesha Tanesco kujiendesha kibiashara.
CHANZO: NIPASHE
 
kweli kuchagua CCM ni kuchagua maafa kasi zaidi nguvu zaidi ari zaidi bora maisha kwa kila mtz
 
kweli kuchagua CCM ni kuchagua maafa kasi zaidi nguvu zaidi ari zaidi bora maisha kwa kila mtz
Sio kuchagua ccm, kwani walichaguliwa hao au walinyakua? Wananchi wengi walijitokeza kuchagua maisha nafuu yaliyotangazwa na wapinzani lakini kwa kuwa ccm iliapa kwamba piga ua lazima ccm ishinde kwa hali yoyote ndio ikawa. Kura hazikuonyesha ccm wameshinda.
 
kuna taharifa ya kuwa nauli za mabasi na dala dala zimepanda na kuwa kati ya shs 500 na 800 wajumbe mnalionaje hilo?
 
kuna taharifa ya kuwa nauli za mabasi na dala dala zimepanda na kuwa kati ya shs 500 na 800 wajumbe mnalionaje hilo?

Godwine hiki ni kilio kwa watz. embu tujuze imepanda katika mkoa gani kwani hizi nauli zinatofautiana mkoa hadi mkoa pia ungetuwekea source ingependeza zaidi.
 
Ingepanda kama mara 20 hivi ili wakereketwa wa CCM wakione cha moto maana wengi wao hoi hae kama mimi
 
Itapendeza zaidi kama ingekuwa sh 1000 kwa kilometer ili wananchi tuingie mtaani coz this is too much! Mara umeme, mafuta, nauli vimepanda bei all at once hivi huu mwaka utaisha kweli maana ndo tumeuanza na kasumba zote hizi.
 
HUENDA safari za kwenda mikoani kwa mabasi zikapungua endapo Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) itaridhia maombi ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (Taboa).

Taboa inapendekeza nauli ya mabasi hayo ipande kwa asilimia 100 kwa kile inachodai ni ongezeko la gharama za uendeshaji, lakini inapingwa na Baraza la Watumiaji wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra CCC).

Katika maombi yake, Taboa imeambatanisha mchanganuo wa ongezeko la gharama za usafirishaji na mapendekezo ya nauli yaliyoainishwa katika madaraja matatu yakionesha
ongezeko hilo kwa kila daraja.

Sumatra CCC kwa upande wake inashikilia nauli hizo zibaki kama zilivyo kwa maelezo kuwa hakuna gharama zilizoongezeka.

Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Sumatra, Ahamad Kilima, alisema jana kwenye mkutano wa wadau, mapendekezo yao yanataka nauli ipande kwa Sh 69.86 kwa kilometa kwa kila abiria kutoka Sh 26.60 kwa kilometa ya sasa kwa mabasi ya kawaida, ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 163.

Alisema kwa mabasi ya Semi Luxury, walipendekeza Sh 97.59 kwa kilometa kutoka Sh 40.70
ambalo ni ongezeko la asilimia 140.

Kwa mabasi ya anasa walipendekeza Sh 113.71 kwa kilometa kwa kila abiria kutoka Sh 46.40 ya sasa ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 142.

Alitoa mfano wa mabasi ya Dar es Salaam-Arusha ambayo nauli ya sasa ni Sh 16,400 mabasi ya kawaida na kutaka iwe Sh 43,000.

Pia kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya Sh 22,000 iwe Sh 58,000.

Akisoma mchanganuo huo mbele ya wadau wa usafirishaji, Katibu wa Taboa, Wilbard Mtenga, alielezea baadhi ya gharama hizo kuwa ni mishahara ya wafanyakazi wanne ambayo ni Sh milioni moja, riba kwa mikopo kwa ununuzi wa mabasi ambayo ni asilimia 19, ununuzi wa matairi na mengineyo ambayo gharama zake zilioneshwa kwa mwezi na mwaka.

Mwenyekiti wa Sumatra CCC, Gilliard Ngewe, alisema wamefanya utafiti makini kwa kupitia mikoa kadhaa kwa mabasi aina ya Scania na ya kichina ya Yutong na kugundua kuwa nauli inapaswa kuongezeka na kuwa Sh 29.75 kwa kilometa kwa mabasi ya kawaida.

Alitoa mfano wa nauli ya Dar es Salaam-Mbeya kwa basi aina ya Scania ambayo nauli ni Sh
22,200, akapendekeza iwe Sh 24,778 ambapo ongezeko ni Sh 2,500.

Alisema kwa Yutong, nauli ya Dar es Salaam - Mbeya inapaswa kupungua kwani ilitakiwa kuwa Sh 28.51 kwa kilometa ambayo ni Sh 23,749 badala ya nauli ya sasa ya Sh 33,900.

“Kutokana na takwimu hizi thabiti kutoka kwa watoa huduma wenyewe, sisi tunaona nauli zibaki kama zilivyo, ili kupata muda wa kuangalia mwenendo wa upatikanaji wa mabasi nafuu yenye ubora katika barabara zetu,” alisema Ngewe.

Mwenyekiti wa Taboa, Mohammed Abdulla, alisema mapendekezo hayo waliyatoa mara ya mwisho mwaka 2008 wakati gharama zilipopanda kwa asilimia 20 tofauti na walivyokuwa wakiomba.

Mshauri wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Wilson Mashaka, alipinga ongezeko la nauli kwa kiasi hicho kwa kuwa miaka ya nyuma walikuwa wakidai ongezeko la nauli kutokana na mfumuko wa bei ambao sasa hadi asilimia 5.5.

Katibu wa Umoja wa Madereva Waendao Mikoani (UWAMADA), Salum Abdalla, alisema wamiliki hawana umoja wa kudai kupanda nauli, kwani kila mmoja anajiamulia yake kutokana
na gharama.

Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Israel Sekirasa, alisema wamepokea mapendekezo hayo na watayafanyia kazi na kutoa uamuzi mwezi huu baada ya kupokea maoni ya wadau Januari 15.
 
Nimesikiliza mapendekezo ya nauli mpya za mabasi zikanistua sana, nikaogopa sana na kujiuliza nchi hii tunaelekea wapi..?

Kumbuka kupanda kwa nauli hizi kutasababisha kupanda kwa bei za bidhaa karibu zote hapa nchini na sana sana mikoani kwa ndugu zetu ambao maskini wa Mungu kipato chao....


Ndugu Wana JF, kama watanzania tufanyeje kuepusha balaa hili?
 
Huu ndo upuuzi mwingine wa nchi yetu, tutapata maisha bora kwa kila mtanzania kweli?
 
Back
Top Bottom