Godlisten Masawe
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 738
- 283
Tunazungumzia nauli kupanda kutoka shillingi mia hadi mia mbili, na katika my original post, nimeelezea kwa uwezo wangu wote binafsi naona tatizo lipo wapi. Vinginevyo hakuna anaekataa kwamba wananchi wana hali mbaya, lakini wapo wanaopinga (mimi nikiwa mmoja wapo) vitendo vya baadhi ya viongozi kutumia hali hizo mbaya za wananchi, kisiasa.
Heshima kwako Mchambuzi;
Una mawazo mazuri sana kamanda.
Pamoja na wabunge kutumia matatizo (hali mbaya) ya wananchi kujinufaisha kisiasa; Binafsi nawaunga mkono tamko la wabunge wa dsm kwa sababu moja tu ifuatayo;
- Taifa letu limeazimisha miaka hamsini ya uhuru, ilitakiwa pale tuwe na daraja na wananchi tuvuke bure (bila kutoa hata tshs. 5), Sitaki kuangalia wala kufahamu mapato na gharama za uendeshaji wa kivuko.