Nauli Feri: Mnyika, Hata Wewe?

Hayo ni maswali ya msingi. Kabla ya kuangalia uboreshwaji wa huduma, mapato ya wananchi, n.k, ni muhimu kwanza tuwe na takwimu juu ya gharama za uendeshaji wa kivuko kile, ambazo wabunge walizembea kuzihoji huko bungeni, na badala yake kuja kutupiga blah blah kwenye vyombo vya habari. Na ndio maana hoja yangu ya msingi ni kwamba kina Mnyika et al. hawana legitimacy kuhoji hayo barabarani. Hawana takwimu zozote zinazowasaidia kujenga hoja kwamba ongezeko la sh. 100 ni kubwa sana; Mbaya zaidi, walizembea kuhoji kamati ile ya bunge kuhusu gharama za uendeshaji wa kivuko kile. Kutokana na mapungufu hayo, hawana legitimacy, na wamekurupuka kwa msukumo wa kisiasa huku mantiki ikiwasuta. Warudie ile kamati ya bunge kwanza. Na mtu sharp kama Mnyika lazima kwa sasa analijua hilo, sina uhakika kuhusu wengine.

Magufuli ana mapungufu mengi kama kiongozi, lakini ni dhahiri kwamba Magufuli sio kiongozi wa 'kupurupuka' katika maamuzi.
Maadam swala hili lilipitia Bungeni na wakalipitisha bila kupinga... Inasikitisha sana kuona wabunge hao hao leo wanapinga ongezeko bila kuwa na takwimu kuthibitisha inawezakana kwa njia ipi na sii kusikilizia Upepo wa wananchi wanapozomea..Mnyika anatakiwa kuwa makini sana ktk maswala haya ya utendaji kazi maana sii mara ya kwanza kuvurugana na Magufuli akiwa upande wa JK ktk kutoa ahadi zinazoharibu utendaji kazi...kama lile sakata la Machinga na vibanda vyao Ubungo..
 
Magufuli jimboni kwake aliomba kivukoni wananchi wasilipe ila halimashauri ikasema tunakitegemea sana kwa mapato ya halimashauri je yy naye alikuwa mjinga?

Na hapo ndio ujue suala hili la kigamboni pia lina uwindaji wa maslahi binafsi chini kwa chini ili Manispaa ndio ipewe mamlaka ya kuendesha kivuko cha kigamboni, ili waheshimiwa wajipatie tender mbalimbali, huku pia wakitafuna mapato kwa njia ya posho za vikao, wakiwa kama madiwani (katika mazingira ya manispaa....mbunge ni diwani pia by default);
 
Nafasi ya uongozi (UBUNGE) kama ya kina Waheshimiwa Mnyika, Mtemvu, Ndungulile, Zungu, ni moja na nafasi za juu sana za uongozi katika Jamhuri yoyote ile. Wabunge wanawakilisha MATUMAINI, HOFU, SHABAHA na KIU ya wananchi. Ndio maana nafasi hii inahitaji utashi wa hali ya juu. Mbunge anatakiwa awe na sifa za ‘kiongozi bora’ (sio ‘bora kiongozi’), vinginevyo ataishia kuwa kiongozi mpotoshaji, na anayeongoza au kutoa maamuzi kwa kufuata upepo, huruma kwa wapiga kura wake, pamoja na ‘maslahi binafsi’. Mbunge anatakiwa awe na sifa pamoja na:

· Consistency au uthabiti katika maamuzi na utendaji, na sio leo hili, kesho lile.
· Upeo na uelewa wa mambo anayoyasimamia au zungumzia kwenye umma.
· Ujasiri wa kuwaambia hali halisi wapiga kura wake, bila ya uwoga.
· Uwezo wa kutofautisha baina hoja/maamuzi ya kisiasa na yale ya kimantiki.
· Msimamo usiobadilika/kuyumba kutokana na upepo wa kisiasa.
· Ujasiri wa kusimamia kitu anachokiamini/maamuzi magumu.
· Uwezo wa kufikiri kabla ya kufanya maamuzi muhimu/kutoa kauli au msimamo mbele ya umma.

Katika sakata la Magufuli na nauli feri, ni dhahiri kwamba wabunge wetu hawa - Waheshimiwa Mnyika, Mtemvu, Zungu, Ndugullile, Mnyika na wengineo, wamepwaya katika sifa nyingi hizi. Kwa nafasi zao, wameonyesha ukosefu wa uthabiti (consistency) katika kauli/maamuzi yao, wamekosa upeo, wamekosa ujasiri wa kuwaambia ukweli wapiga kura wao bila ya uwoga, washindwa tofautisha hoja/maamuzi ya kisiasa na ya kimantiki, wameji expose kwenye mazingira ya kuweza badili misimamo yao siku za mbeleni, wameshindwa kuwa na ujasiri wa kuunga mkono maamuzi ya kimantiki ya magufuli, na wameshindwa kufikiri kwanza kabla ya kutoa kauli nzito kwa umma/wapiga kura wao. Ndio maana, kwa haya yote, Magufuli amewapiku, ingawa wanajidanganya mbele ya umma, kwamba wao ndio wapo sahihi, na magufuli ndio hayupo sahihi. Nitafafanua.

Feri ya Kigamboni ni kivuko ambacho kinaendeshwa kwa ruzuku kubwa sana ya serikali (yani government subsidy). Sina uhakika kama waheshimiwa wetu hawa wanalielewa hilo. Vinginevyo watumiaji wa kivuko kile wangekuwa wanalipa nauli kubwa sana kama kivuko kingekuwa kinaendeshwa na sekta binafsi, au hata kwa ubia kati ya sekta binafsi na serikali (yani Public –Private Partnership).

Waheshimiwa wabunge Mnyika na wengineo, kwenye sekta ya usafiri wa umma (madaladala) ambayo ipo chini ya soko huru, na kusimamiwa na Sumatra, mtumiaji wa chombo cha usafiri (daladala) kutokea Feri hadi Posta, anatozwa shillingi 300 (mia moja zaidi ya nauli ya Feri ya sh.200). Ikumbukwe kwamba umbali kutoka Feri Hadi Posta ni kama Kilometa 3, hivyo mtu ukiamua kutembea, unaweza kufanya hivyo. Kwa maana nyingine, ni hiyari kwa mtu kulipa nauli ya sh. 300 au kutembea. Lakini wengi huwa wanaamua kulipa sh.300, na shughuli za uchumi zinaendelea.

Lakini suala la kivuko cha ferry ni tofauti. Kivuko cha Feri hakiendeshwi na kanuni za soko huria. Umbali wa kivuko kile ni takribani kilometa moja kutoka upande mmoja hadi mwingine. Na tofauti na umbali kutoka Feri hadi posta ambao mwananchi ana hiyari ya kuchagua kati ya kutembea au kulipa nauli ya dala dala ya sh. 300, mwananchi hana hiyari kuchagua kupanda pantoni au kuongelea. Hivyo, lazima mwananchi alipe shillingi 200 kuvuka upande wa pili. Lakini ni muhimu nikasisitiza hili: miaka ya nyuma, serikali ilikuwa inatoa huduma ya kivuko kuanzia asubuhi hadi saa sita usiku. Lakini kwa sababu ya kujali wananchi wake, ikaamua huduma ile itolewe masaa 24. Tusisahau kwamba huduma hii ilitolewa kwa masaa 24 kwa kipindi kirefu sana kwa nauli ya shillingi 100. Na pia tusisahau kwamba pantoni lile likiwashwa asubuhi, halizimwi tena, hivyo kupelekea gharama za uendeshaji kuwa kubwa mno, in terms of fuel consumption (mafuta ya diesel). Sasa katika mazingira haya, Mheshimiwa Mnyika na wengine, tatizo lipo wapi serikali ikiamua kuongeza nauli kwa shillingi mia moja?

Waheshimiwa wabunge Mnyika na wengineo, tuseme basi serikali inajitahidi kukamilisha daraja la kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa eneo lile. Je, mtakuwa na consistency katika hoja zenu? Kwani ni dhahiri kwamba, Daraja likikamilika leo, litakuwa na urefu wa kilomita sio chini ya saba (kati ya 7-10), na ramani zinaonyesha kwamba litaanzia maeneo ya Kurasini na Kushukia maeneo ya Kibada. Umbali huu wa kilometa saba, ni karibia mara saba ya umbali kutokea Feri hadi Posta ambako watu wanalipa nauli ya daladala sh.300. Daraja likikamilika, ni wazi usafiri kwa umma kutoka kurasini (DSM) hadi kibada (kigamboni), utaendeshwa chini ya kanuni za soko huria (madaladala), na wasafiri watalipa sio chini ya sh.300. Muhimu zaidi ni kwamba wananchi watakuwa na uhuru wa kuchagua kutumia daladala (chini ya soko huria) au pantoni (iwapo economics za pantoni zitakuwa bado zinaruhusu). Je, waheshimiwa wabunge, tuseme kwamba wananchi wafanye mgomo juu ya nauli ya kuvuka daraja kwa daladala (chini ya kanuni za soko huria) kwa sh. 300 au zaidi, mtakuwa upande gani, wa Sumatra au Wananchi? Ikumbukwe pia kwamba hili daraja kushukia Kibada haina maana msafiri amekamilisha safari yake kwenda upande wa pili wa feri, kwani umbali kutokea Kibada hadi upande wa pili wa feri (kigamboni) ni karibia kilometa 18. Sasa ukimjulisha umbali wa kivuko cha daraja (kilometa 7) na umbali wa Kibada hadi upande wa pili wa feri (kilometa 18), tunapata jumla ya umbali wa kilometa sio chini ya 25. Je, nauli mpya ya daladala chini ya soko huria kwa umbali wa kilometa 25 itakuwa sh 200 kama ya kivuko? Jibu ni hapana.

Waheshimiwa wabunge, kuna wakati bunge letu tukufu liliunda kamati maalumu kuchunguza gharama za uendeshaji wa kivuko cha kigamboni ili kubaini changamoto zilizopo, lengo likiwa ni kutafuta njia za kuboreshwa huduma ile kwa wananchi. Nyinyi kama wabunge mlikuwepo bungeni kuweza kuhoji mengi sana, lakini hamkufanya hivyo, na badala yake mnakuja kuyahoji masuala ya mapato barabarani. Kwa mfano, ripoti ya bunge ilibaini kwamba mapato kwa siku ni 9,000.000 (shillingi milioni tisa - enzi za nauli ya shillingi 100); Ripoti ile ikaendelea kusema kwamba ziada (yani surplus) kwa mwezi ni shillingi milioni tano. Lakini kamati ile haikutoa takwimu juu ya gharama za uendeshaji, na badala yake, ikatoa taarifa za masalio kwa mwezi. Sasa hoja yenu kwamba kuna ufisadi katika ukusanyaji wa mapato, kwanini hamkuijadili bungeni wakati kamati ile inatoa ripoti yake? Waheshimiwa wabunge, mngekuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuhoji ongezeko la Magufuli la sh 200 leo iwapo tu mngekuwa makini bungeni, kuhoji takwimu juu ya gharama za uendeshaji kwa siku katika kivuko cha ferry ni zipi. Au pengine hamkuwepo bungeni, au hamkuwa na upeo wa mbali, vinginevyo mlipoteza fursa nzuri sana, ambayo ingeweza kutuokoa na sakati hili linalochanganya wananchi. Wapiga kura wenu ni muhimu wakagundua uzembe wenu huu.

Kwa vile kamati ya bunge haikutoa takwimu juu ya gharama, nimejaribu kutumia nyingine ili angalau tupate makisio ya gharama kwa siku na kubaini yafuatayo i.e. if we work backwards: Mapato kwa siku sh. 9,000,000 (chini ya nauli ya sh.100) ; Masalio (surplus) kwa mwezi, sh.5, 000,000 (chini ya nauli ya sh.100). Hii ina maana kwamba masalio/surplus kwa siku ni Sh. [5,000,000] GAWANYA KWA [SIKU 30[, ambayo inatupa Sh. 166,666 kama masalio/surplus kwa siku. Hivyo basi, gharama kwa siku itakuwa: [Sh. 9,000,000] TOA [Sh. 166,666], ambayo ni sawa na na Sh. 8,833,333 kwa siku.

Waheshimiwa wabunge, kwa kutumia simple economics peke yake – gharama za kuendesha kivuko hiki ni 98% ya mapato kwa siku. Sasa tukianza kuangalia suala la kupanda kwa gharama za bidhaa muhimu kama mafuta n.k, JE, ni haki kweli kumshambulia magufuli, kisa, amepandisha nauli kwa sh. 100, hivyo kufanya masalio kwa siku yawe sh.333, 332 (laki tatu), badala ya Sh. 166,666? Inawezekana kinachoogopesha wabunge hapa ni the fact kwamba nauli imepanda kwa asilimia 100, kwani ulilitazama suala hili ki-asilimia, bila ya kuwa makini, kitakwimu, ongezeko la asilimia 100 ni kubwa sana. Vinginevyo, kwa sasa, shillingi mia moja ya kitanzania ni karibia na SENTI SITA katika dollar za kimarekani. Waheshimiwa, sote tunajua jinsi gani bei ya mafuta katika soko la dunia imekuwa inaongezeka kila kukicha. Serikali ilianza kutoa huduma ya kivuko kwa masaa 24 kwa kipindi kirefu sana kwa nauli ya Sh.100. Je, mnajua ilikuwa inatoa ruzuku kiasi gani? Na imechukua muda mrefu sana kabla serikali kupandisha nauli kwa shilling mia zaidi (sawa na SENTI SITA za kimarekani), katika kipindi ambacho bei ya mafuta duniani imepanda kwa mamia zaidi, ya hiyo senti sita ya dollar.

Kuna hoja pia kwamba Magufuli hakufuata Sheria, Je ni sheria ipi iliyo muhimu zaidi ya ile iliyopitishwa na Bunge ambalo nyinyi ni wawakilishi wetu - THE FERRY ACT ambayo ukiitazama, utabaini kwamba Magufuli na washauri wake, wameifuata mstari kwa mstari kabla ya kufikia uamauzi wa kuongeza nauli kwa shillingi 100? Waheshimiwa, na hasa John Mnyika - ambapo Ubungo ni Jimbo lako, kwanini haufuatilii suala la Kituo cha mabasi cha ubungo ambako kuna usumbufu na gharama zisizo na sababu kwa wananchi, pengine kuliko suala la kigamboni? Mfano, ili mtu uingie kituo cha ubungo kwa mguu, kwa dakika moja tu kumsindikiza ndugu yako anaesafiri ambae anahitaji msaada kwa sababu ya uzee, au ulemavu au umri mdogo (mtoto wa shule), unatozwa sh 200, je hamuoni kwamba hili nalo ni tatizo? Au ni kwa sababu, tofauti na mapato ya ferry ambayo hayapo chini ya manispaa, mapato ya Ubungo yapo chini ya manispaa ambako kwa nafasi zenu kama wabunge, mnakaa kwenye VIKAO kama madiwani kupitia/kupanga bajeti, na kula posho za vikao?

Kwanini huwa amhoji sheria zinazotumika na Sumatra kupandisha nauli za daladala ovyo? Au ni kwasababu mna imani kubwa sana kwamba soko huria huwa halifanyi makosa, na badala yake makosa hufanywa na serikali tu? Ni dhahiri kwamba kwenye usafiri wa umma ulio chini ya soko huria (daladala), wapo waheshimiwa wengi wenye maslahi binafsi. Vinginevyo, hata kwenye suala la nauli za mateksi, bajaji, ilitakiwa wabunge pia waibane serikali isimamie hilo, sio kuwaachia wamiliki wa vyombo hivi kuwaburuza wananchi watakavyo. Hata nchi za wenzetu, nauli za mateksi sio za makisio, ni kwa mujibu wa sheria.

Ushauri:
· Ongezeni juhudi katika kujenga hoja zenye mantiki, na mjifunze umuhimu wa kukwepa maamuzi ya kisiasa pale pasipotakiwa, vinginevyo mtachanganya wananchi.
· Elimisheni wapiga kura wenu kwamba uamuzi wa Magufuli ni sahihi, na toeni ahadi kwao kwamba mkienda bungeni mwisho wa mwezi huu, mtaenda kuhoji kamati husika kuhusu suala ambalo mlilizembea kweney vikao vilivyopita - takwimu juu gharama za uendeshaji wa pantoni kwa siku, ili muwe na legitimacy ya kuhoji mnayohoji leo juu ya shilling 200, vinginevyo, hamna that legitimacy as we speak.
· Ibabeni serikali juu ya misamaha ya kodi kwa mwaka ambayo inakaribia asilimia 20 ya bajeti nzima ya mwaka, na muelekeze suala la subsidy ya kigamboni huko, sio kwa magufuli.
· Litazameni suala la market failure kwa makini ili muelewe mapungufu, sio juu ya Ferry pekee, bali hata madala dala, bajaji, na mateksi.
· Vinginevyo, kama hamridhiki, nyinyi ndio watungaji wa sheria zetu, fuateni ushauri wa Magufuli kwamba, pengine Manispaa zichukue jukumu la kuendesha Ferry ili muelewe economics zake, kwani huko mkiwa kama sehemu ya madiwani, pengine mtatusaidia kutuondolea siasa kwa jambo ambalo limejaa mantiki tupu.
· Na Mwisho, Magufuli anastahili kuomba msamaha kwa kauli zake zilizokosa ustaarabu, lakini hastahili kubadilisha msimamo juu ya ongezeko la nauli, kwani uamuzi wake ni sahihi.

Ndugu pamoja na uzuri wa uchambuzi wako lakini kuna kasoro moja ambayo ninahisi ndiyo lengo la uchambuzi wako. Hilo si kingine bali ulitaka kumlenga Mnyika katika suala hilo la kupinga kupanda kwa gharama ya feri. Ukiangalia katika uchambuzi wako jina la Mnyika lilitawala kichwa chako kiasi unarudia jina la Mnyika hata mara mbili (tazama kwenye red).

Jambo moja ni wazi kuwa uamuzi wa umoja wa wabunge wa Dar ulikuwa uamuzi wa pamoja hata kama katika mjadala siyo wote waliounga mkono wazo. Katika utaratibu wa vikao maamuzi ya wengi ndiyo yanayopitishwa hata kama hoja hiyo ni potofu kiasi gani. Fikiria jinsi ambavyo mara kadhaa wabunge wamelalamikiwa na wananchi wakati wanapitisha maamuzi kule Dodoma hata kama wapinzani wachache huyapinga. upinzani wa wachache hauwezi kuzuia maamuzi kupita kwa sababu uwingi ndio unaotumika kuamua siyo uzito wa hoja.

Tukirejea suala la maamuzi na tamko la wabunge wa Dar, sina uhakika kama Mnyika kama Mnyika alikuwa akiunga mkono maamuzi ya kikao kile na kwa namna ile. Tuseme kuwa Mnyika alikuwa akipinga azimio hilo lakini katika kupigia kura (wengi wape) sidhani kama kuna haja kweli ya kumlaumu Mnyika kiasi cha mchambuzi. Ninasema hivyo kwa sababu sijasikia tamko la Mnyika kama Mnyika zaidi ya tamko la wabunge katika ujumla wao.

Kwa upande mwingine mmoja kati ya wabunge nilimsikia akisema kuwa kuhusu suala la kivuko amewasiliana na Dr. Magufuli kabla ya tukio hilo la kupandisha nauli bila kupata ushirikiano. Hivyo, bado Dr. Magufuli alikuwa na haja ya kushirikiana na wabunge hao na wala asitudanganye kwamba suala halistahili kuchukuliwa kisiasa. Hivi, yeye anapowalaumu wabunge kwenye vyombo vya habari anahofu nini kukutana nao?
 
Maadam swala hili lilipitia Bungeni na wakalipitisha bila kupinga... Inasikitisha sana kuona wabunge hao hao leo wanapinga ongezeko bila kuwa na takwimu kuthibitisha inawezakana kwa njia ipi na sii kusikilizia Upepo wa wananchi wanapozomea..Mnyika anatakiwa kuwa makini sana ktk maswala haya ya utendaji kazi maana sii mara ya kwanza kuvurugana na Magufuli akiwa upande wa JK ktk kutoa ahadi zinazoharibu utendaji kazi...kama lile sakata la Machinga na vibanda vyao Ubungo..

Tatizo letu ni kwamba viongozi wenyewe ndio wanawapotosha wananchi kwa kutowaambia ukweli katika masuala kama haya, kwani wao kama viongozi wanaangalia zaidi hali zao za kisiasa, kwa kuangalia wananchi wanaegemea wapi, bila ya kujali kuwasahihisha au kuwaelimisha wananchi kwa manufaa yao wenyewe wananchi.
 
Na hapo ndio ujue suala hili la kigamboni pia lina uwindaji wa maslahi binafsi chini kwa chini ili Manispaa ndio ipewe mamlaka ya kuendesha kivuko cha kigamboni, ili waheshimiwa wajipatie tender mbalimbali, huku pia wakitafuna mapato kwa njia ya posho za vikao, wakiwa kama madiwani (katika mazingira ya manispaa....mbunge ni diwani pia by default);
Lakini hivi ndivyo ilitakiwa kuwa maadam tumeingia mfumo wa manispaa kusimamia maendeleo ya miji.. Tatizo lake ni Ufisadi na hata kama tutapinga hilo bado ufisadi upo palepale unaposimamiwa na wizara..

Kwa hiyo kama ingekuwa hakuna Ufisadi leo na tunaogopa kuhamisha mamlaka hayo City ningeelewa..Kinachofanyika hapa ni kutoa Ulaji mfuko mmoja kwenda mfuko mwingine lakijni hasara kwa wananchi inabakia palepale. Tunachotakiwa kufanya ni ku scrap mfumo mzima na kuandika upya mamlaka ya Halmashauri, vyombo vya ukaguzi wa mahesabu na ufanisi ktk makusanyo ya kodi, vibali, liseni na kadhalika toka kiila manispaa hadi serikali kuu.

Maadam hatuna miiko na maadili swala hilihalina suluhu yoyote zaidi ya kwamba hata hizo Tsh 200 haziendi ktk kuhakikisha kivuko kinajienbdesha bali zinakwenda mfukoni mwa watu..Bado serikali itatakiwa kuchangia na pengine kwa kiasi kikubwa zaidi ya mwaka jana au juzi.
 
Ndg. Mchambuzi, hongera sana kwa uchambuzi wako ambao nauunga mkono. Pengine kama wewe, nimefadhaishwa sana na namna wabunge wetu walivyolichukulia suala hili, huku wakisaidiwa na vyombo vya habari ambavyo vimechangia kutoa mwanga kule kusiko na umuhimu, na kuacha kwenye umuhimu mkubwa wa kuwaelewesha wananchi.

Hii inamaana kuwa, hata kama kuna tatizo katika kauli za Magufuli, kauli hizo hazikupaswa kupewa uzito kuliko uzito wa kugomea nauli yenyewe. Waandishi wetu walipaswa kumhoji waziri afafanue kila jambo lililosukuma uamuzi wa kupandisha nauli; na nina imani wangepata majibu. Kuacha hilo kwa kutega tu microphone na kuandika alichosema bila ufafanuzi, na siku inayofuata kuandika tu wanachosema waheshimiwa wabunge bila ya kuwauliza maswali magumu kama uliyoangazia wewe, ni kushindwa kufanya kazi yao sawa sawa. Na kwa nafasi hiyo, wamekuwa vipaza sauti tu wasio na uwezo wa kuelimisha umma. Hapa wao wamekuwa sehemu ya tatizo la Magufuli, na wala si sehemu ya ufumbuzi wa matatizo ya Wananchi.

Katika sehemu fulani ya Tanzania yetu ya leo, vyombo vya habari vinaunda vibaya uwezo wa kujadili hoja wa jamii yetu. Watu wamejenga tabia ya kupenda kulalamika sana, kama vile kujenga nchi si kazi yao, na wanajaribu kwa kila njia kukwepa jukumu hilo. Pengine unaweza kuangazia kwa upana zaidi wajibu wa vyombo vya habari katika migogoro kama hii, hata ukichukulia suala la Kigamboni kama case study?

Kwa muda mrefu, JF imekosa michango mizito yenye uchambuzi wa kina kama wako. Nakutia moyo uendelee kuchangamsha jamvi kwa kutoa chambuzi za namna hii ili kutusaidia wale ambao tunakosa uelewa wa mambo mbali mbali. Magazeti yetu nayo ndo hivyo tena...
 
Ndugu pamoja na uzuri wa uchambuzi wako lakini kuna kasoro moja ambayo ninahisi ndiyo lengo la uchambuzi wako. Hilo si kingine bali ulitaka kumlenga Mnyika katika suala hilo la kupinga kupanda kwa gharama ya feri. Ukiangalia katika uchambuzi wako jina la Mnyika lilitawala kichwa chako kiasi unarudia jina la Mnyika hata mara mbili (tazama kwenye red).

Jambo moja ni wazi kuwa uamuzi wa umoja wa wabunge wa Dar ulikuwa uamuzi wa pamoja hata kama katika mjadala siyo wote waliounga mkono wazo. Katika utaratibu wa vikao maamuzi ya wengi ndiyo yanayopitishwa hata kama hoja hiyo ni potofu kiasi gani. Fikiria jinsi ambavyo mara kadhaa wabunge wamelalamikiwa na wananchi wakati wanapitisha maamuzi kule Dodoma hata kama wapinzani wachache huyapinga. upinzani wa wachache hauwezi kuzuia maamuzi kupita kwa sababu uwingi ndio unaotumika kuamua siyo uzito wa hoja.

Tukirejea suala la maamuzi na tamko la wabunge wa Dar, sina uhakika kama Mnyika kama Mnyika alikuwa akiunga mkono maamuzi ya kikao kile na kwa namna ile. Tuseme kuwa Mnyika alikuwa akipinga azimio hilo lakini katika kupigia kura (wengi wape) sidhani kama kuna haja kweli ya kumlaumu Mnyika kiasi cha mchambuzi. Ninasema hivyo kwa sababu sijasikia tamko la Mnyika kama Mnyika zaidi ya tamko la wabunge katika ujumla wao.

Kwa upande mwingine mmoja kati ya wabunge nilimsikia akisema kuwa kuhusu suala la kivuko amewasiliana na Dr. Magufuli kabla ya tukio hilo la kupandisha nauli bila kupata ushirikiano. Hivyo, bado Dr. Magufuli alikuwa na haja ya kushirikiana na wabunge hao na wala asitudanganye kwamba suala halistahili kuchukuliwa kisiasa. Hivi, yeye anapowalaumu wabunge kwenye vyombo vya habari anahofu nini kukutana nao?

Sababu yangu kubwa ya kumtaja Mnyika ni kwa sababu ninamheshimu na kuthamini sana kazi yake kama mwakilishi wa wananchi. Ni moja wa wabunge kumi ambao naona wanatosha katika nafasi zao, ukichanganya vyama vyote vya siasa, pengine yeye akiwa katika tatu bora. Kwa umakini wake, sikutegemea angetumbukia katika sakata ambalo ni la kimantiki kuliko siasa. Ni hayo ndio yamenisukuma zaidi kuhoji - hata wewe Mnyika ninaekuaminia? Ubungo ni mbali kidogo na kivuko tofauti na ILALA NA TEMEKE, angekaa kimya kwa siku kadhaa kujipanga kutoa maelezo juu ya msimamo wake angekosa nini? Vinginevyo, wengine wa CCM (sio wabunge wote) tumeshawazoea na blah blah na matusi yao, pale wanapoingiliana maslahi. Lakini sio mtu kama Mnyika. Nasimama kuhukumiwa kwa kumtaja Mnyika, lakini haikuwa kwa nia mbaya kabisa.
 
Hapa ndio mnapokosea....Magufuli alitoa kauli ile baada ya kuzomewa! hakuna anayesema wananchi waombe msamaha kwa kuzomea.......

Acha Uh*y* wako ww!!! Kiongozi kama waziri hatakiwi ku-overeract kiasi kile hata amekuwa provoked kiasi gani.

Kuweni wastaarabu jamani!! Nendeni na wakati! Enzi zile hazipo tena!! Kusoma kote na kuchanganyika kote na watu wa background zingine bado mnaishi enzi zile tu>> Duh! Kazi kweli kweli!!!
 
Nilipokusikia unagombea Ubunge Kinondoni, nilifikiri ni aina ya wale wanaofanya show game tu za "na mimi niligombea" , lakini baada ya kuyafuatilia mawazo yako hapa jamvini ninashawishika kuwa hiki ni aina ya kichwa kinachopaswa kiwepo Bungeni.

Kwa heshima na taadhima nakuomba ufikirie kugombea jimbo la mkoani Mbeya mwaka 2015, ukiisubiria Kinondoni na fitna zake za kisiasa hautafanikiwa, big up sana Mchambuzi..
 
Unnecessarily...kamanda mchambuzi huwa nakuheshimu sana. Nakumbuka ile article yako juu ya Baba wa Taifa Nyerere! Leo umechemka. Naona umeinga kwenye mradi wa spinning na propaganda wa Magufuli, kwa kujua ama kutojua. Pole! Juzi nilimsikia mtangazaji mmoja wa Clouds FM (nililazimika kusikiliza coz nilikuwa ndani ya gari ya mtu), akiweka sauti ya Pombe Magufuli, hasa pale aliposema ati anamheshimu sana Mdee kwa sababu ana-concetrate na jimbo lake (hajui kuwa Mdee yuko safarini), akasema ati Mnyika ameshindwa kushughulikia mambo kama ya mabweni UDSM na nauli ya Ubungo Terminal (pia hajui jitihada za Mnyika ndizo zilisababisha nauli isipande kwenda shilingi 300 kama ilivyokuwa imepangwa na sasa hivi kutokana na juhudi hizo, jiji linapitia sheria ndogo ndogo juu ya suala la Ubungo Terminal kucheki utaratibu huo).

Mtangazaji yule (alikuwa Redio One, somebody Ayo sijui), kama ulivyofanya wewe hapa, akamalizia kwa kusema "hiyo ni sauti juu ya Waziri Magufuli akijibu hoja za wabunge wa Dar es Salaam juu msimamo wao wa kupinga ongezeko la nauli ya shilingi 100, akiwemo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika." Come one what a crap!

The same to u brother. Hoja yako hii ya kipuuzi kabisa isiyolingana na uwezo wako niliozoea kuuona hapa mara kwa mara! Nimeshindwa kuendelea kusoma mpaka mwisho baada ya kuona kuwa umeingia kwa kiasi kikubwa katika spinning ya Kundi la Pombe Magufuli, ambalo limeamua kuweka msisitizo kuwa kinachopingwa na wote wenye akili timamu eti ni ONGEZEKO LA SH. 100! To hell, hii si hoja kwa watu wenye akili walioona crap ya Magufuli bro. Kuna issues kadhaa za msingi, suala si sh. 100, hata kidogo, ukijadili hivyo ure missin the point at large bro! Nitakueleza baadae kidogo!

Qualify some several conclusions zako, mara unasema serikali inaweka pesa nyingi sana katika kuendesha kivuko hicho!!!!! He kiasi gani hicho bro hebu kiseme! Je kinatosha au hakitoshi kujenga daraja hapo mahali ili tuondokane na bugudha ya watu kulipia mahali ambapo haikusathili kama serikali ingetimiza tu wajibu wake wa kutoa huduma kwa watu kwa kujenga daraja! Kuna vitu kadhaa katika hoja yako nataka nikueleze ili ufikirie upya attack zako kwa Mnyika na wabunge wenzake. Ntakueleza...punde
 
Mnyika ana haki ya kutetea kama watu wanakusanya milioni 18 kwa siku kama alivyokiri magufuli mwenyewe na hakuna maboresho yoyote ni nini kinachowafanya watoze 200 ambacho wameshindwa kukifanya kwa tozo ya sh 100??
 
Asante kwa mchango wako mzuri,

Yote haya ni kwasababu hatuna figures na wabunge hawakazanii hilo, na hawakubali uzembe waliofanya kuiacha kamati ile kuwasilisha kazi yake bila ya kuliambia bunge, na umma kuhusu Gharama za kuendesha kivuko ni zipi. Na huo ndio msingi wa hoja yangu kwamba wabunge hawana legitimacy kuhoji ongezeko la shillingi mia, na warudi wakajipange upya katika kikao kijacho ili kurekebisha tatizo. Pengine wana majibu ya maswali yako, ambayo hawatuambii, lakini wanatumia hayo kutoa kauli walizotoa, hatujui. Vinginevyo kwa, kwa kuzingatia uzembe ule, pamoja na uchambuzi wangu ambao unaweza kuwa hauna upeo, i stand to say kwamba Magufuli yupo sawa, na katika hoja yangu nimetumia mantiki, sio siasa kufikia hapo.

Pia naomba utambue kwamba Mnyika hajakaripiwa, amehojiwa akiwa mwakilishi wa wananchi, na hizo ndizo taratibu. Na nisingependa kuingia katika mjadala wa kumzungumzia Mheshimiwa Mnyika kama Mnyika, nimeshaelezea kwanini nimeona mapungufu yake katika hilo, na kwa sasa kilicho mbele yetu ni mawazo juu ya jinsi gani tunaweza kujinasua katika tatizo hili, na kuweka mambo sawa. Nitajadiliana na wewe in that context, not in the context ya Mnyika. Vinginevyo, ninamheshimu sana Mnyika, na kama wewe ndio Mnyika, naomba sana utambue hilo, na kama ni mtu unayemfahamu, tafadhali kamweleze hilo. Na kiongozi makini haoni tatizo kukosolewa. kwani nadhani hata Mnyika anafahamu kwamba POLITICS IS A LEARNING PROFESSION, na haijalishi umekaa kwenye politics miaka mingapi. Asante sana.
 
Mnyika ana haki ya kutetea kama watu wanakusanya milioni 18 kwa siku kama alivyokiri magufuli mwenyewe na hakuna maboresho yoyote ni nini kinachowafanya watoze 200 ambacho wameshindwa kukifanya kwa tozo ya sh 100??

je, gharama za uendeshaji kwa siku au mwezi, sisi kama wananchi hatuna haki ya kuambiwa ni shillingi ngapi? This is where wengi wetu tunalikwepa katika kutetea wahusika, na tukipata takwimu hiyo, nina uhakika wengi wetu, kama sio wote tutakuwa katika kurasa mmoja - Kimsimamo.
 
Ndg. yangu mcambuzi unaeza kuwa sawa pia ucwe sawa, Tshs 200 sio nyingi lakn pia ni nyingi kutokana na mtu, Hawa wananchi wanaolalamika co Mataahira,wana akili zao timamu. Uchumi wa nchi yetu kila siku unazidi kushuka na maisha yanazidi kuwa magumu, kwako 200 inaeza kuwa ndogo lakn co kwa yule. UKIONA watu 200 tu wanalia namna hii juA WATANZANIA TUMEPIGIKA MBAYA, na Magufuli analijua hili, Kama uchumi wa nchi unaporomoka nilitegemea Magufuli angefanya mchakato wa kupunguza hiyo nauli ya Shs 100 na sio kuongeza, kikubwa waweke ucmamizi yakinifu ktk mapato, mtu mwenye akili timamu huezi mtetea aliyekaa na kupandisha kutok sh 500 mpk 1800 kwa guta na sh 500 mpk 1500 kwa Suzuki, hiyo co akili ni MATOPE. NAWAUNGA MKONO WABUNGE WA DSM, na sikubaliani na majibu ya kipumbavu ya kupga Mbizi ya bwn Maguful,NAJUA Unajua MNYIKA ni kiongoz makini na ndio mana akawa heading yk na ndio mana tunamwambia Mh. Mnyika uzi huohuo. MAGUFULI ATUOMBE RADHI WATANZANIA.
 
Iwapo hoja hii ni sensitive kwa baadhi ya watu humu, wale wote wenye mtazamo huo, mngeshauriana na MODs ili waifute hii thread, kama ambavyo huwa inatokea nyakati fulani fulani. Vinginevyo, as long as it stays, nitaendelea kujadili masuala muhimu na yanayowagusa wananchi, pamoja na kuhoji matamshi ya wawakilishi wao kwenye masuala nyeti kama haya, focus ikiwa sio WABUNGE WA CHADEMA au CCM (mbali ya kuwataja tu awali kwa majina wajulikane ni kina nani), bali kuwahoji kama wawakilishi wa wananchi, huku tukijikita zaidi kwenye mada husika, lengo likiwa kuijadili, na kuitolea mapendekezo, na kisha kumaliza mjadala husika.
 
Ndg. yangu mcambuzi unaeza kuwa sawa pia ucwe sawa, Tshs 200 sio nyingi lakn pia ni nyingi kutokana na mtu, Hawa wananchi wanaolalamika co Mataahira,wana akili zao timamu. Uchumi wa nchi yetu kila siku unazidi kushuka na maisha yanazidi kuwa magumu, kwako 200 inaeza kuwa ndogo lakn co kwa yule. UKIONA watu 200 tu wanalia namna hii juA WATANZANIA TUMEPIGIKA MBAYA, na Magufuli analijua hili, Kama uchumi wa nchi unaporomoka nilitegemea Magufuli angefanya mchakato wa kupunguza hiyo nauli ya Shs 100 na sio kuongeza, kikubwa waweke ucmamizi yakinifu ktk mapato, mtu mwenye akili timamu huezi mtetea aliyekaa na kupandisha kutok sh 500 mpk 1800 kwa guta na sh 500 mpk 1500 kwa Suzuki, hiyo co akili ni MATOPE. NAWAUNGA MKONO WABUNGE WA DSM, na sikubaliani na majibu ya kipumbavu ya kupga Mbizi ya bwn Maguful,NAJUA Unajua MNYIKA ni kiongoz makini na ndio mana akawa heading yk na ndio mana tunamwambia Mh. Mnyika uzi huohuo. MAGUFULI ATUOMBE RADHI WATANZANIA.

Tunazungumzia nauli kupanda kutoka shillingi mia hadi mia mbili, na katika my original post, nimeelezea kwa uwezo wangu wote binafsi naona tatizo lipo wapi. Vinginevyo hakuna anaekataa kwamba wananchi wana hali mbaya, lakini wapo wanaopinga (mimi nikiwa mmoja wapo) vitendo vya baadhi ya viongozi kutumia hali hizo mbaya za wananchi, kisiasa.
 
Ninamheshimu sana Mchambuzi,lakini nashawishika kusema ameingia kichwa kichwa katika vita dhidi ya Chadema,na ndio maana mashambulizi yake yote ameyapeleka kwa Mnyika.Ninachomshangaa anafanya fitina zake kwa kuangalia ongezeko la nauli za abiria tu.Lakini hamfikirii kijana aliyepandishiwa gharama ya kusafirisha guta kutoka 200 hadi 1800.Namshauri mchambuzi kama katumwa kumsafisha Magufuli kwa kumchafua Mnyika kakosea sana.Magufuli hana tofauti na Lyatonga Mrema katika papara za uongozi.
 
Back
Top Bottom