Natokwa na mapele kama vijipu mashavuni

alexmahone

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
482
405
Msaada tafadhali
Nimekuwa na tatizo la kutokwa na mapele mashavuni.Hali hii ilianza pindi nilipoanza kuota ndevu.,Ila haijalishi ninyoe kwa mkasi,kwa wembe mpya,kwa mashine,kwa magic powder na hata nisiponyoa ndevu huwa yananitoka tu.Nikiyakamua yanatoa usaha kidogo na damu nyingi,then vinabaki vidonda.
Nimejaribu kutumia sabuni mbalimbali.,safi cream,majani ya aloevera na nimekunywa maji yake.Nilishawah kuonana na daktari anaehusika na ngozi akanichoma sindano maeneo hayo yenye mapele,sifaham ni dawa gani aliniwekea lakini bado yanaendelea.
Dawa zote hizo nimetumia kwa nyakati tofauti.
Kwa wengi wanaoniona huwa wananishauri nisitumie wembe,nawaitikia kwakuwa najua nishajaribu yote na hakuna tofauti.
Nilishapima HIV nikidhani yawezakuwa ni mwanzo,lkn sina.Nimefikiri pengine ni allegy ila napata taabu kutambua ni nn kinanidhuru.Natamani nigoogle lakini sijui niandike nini kwny headline.
Mwisho nimeamua kuja hapa jamvini..
Nawasilisha..
 
Kifupi ngozi yako ni sensitivu sana.
Yatakuja kuacha tu yenyewe, ni mapito tu ya ukubwani.

Pole sana mkuu.
 
hiyo ni staphylokoka skin infection, hao wadudu hua wako juu ya ngozi sasa mtu anaponyoa wanaaingia ndani kupitia michubuko na kusababisha vipele vinavokua na usaha. cha msingi ni kwamba epuka kunyoa mara kwa mara(kama sio sharobaro), au kabla ya kunyoa paka kwanza spirit kisha subiri muda ndo unyoe, pia kuna dawa ya kupaka mupirocin, au wadudu hao ni sugu sana wa dawa kama dawa ya kumeza nunua cloxacillin (dose sikumbuki), ukitaka kugugo weka stphylococcus skin infection
 
Thnx mkuu.,kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom