Nationmedia Tanzania kufungiwa?

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
58,768
78,437
wajameni hali ya mambo inavyoendelea naskia tetesi kuna maagizo ya kulifungia mojawapo ya magazeti kati ya The Citizen au The East African! Kuna nguvu kubwa inaelekeza hayo yafanywe ikumbukwe The Citizens washapewa onyo hivi majuzi na Wizara ya Habari na Michezo! Yetu macho tushuhudie kinachofata maana kuna uwezekano mkubwa wa wiki hii viongozi husika kuitisha Press maelezo! hasa kuhusiana na habari inayomhusisha RA moja kwa moja na Dowans! Nae mhusika anatarajiwa kutoa press wiki hii!
 
Kwa hali tete kisiasa nchini ambapo jamii wanaiona CCM bundi katikati vindege msituni, busara zinaelekeza kwamba chama hiki hakiwezi kujichongea adui zaidi katika jamii yetu safari hii kwa jina la VYOMBO VYA HABARI.

Vyombo vya habari ni adui ambayo ni hatari sana serikali kucheza nayo maana wa kupoteza zaidi hapo ni serikali zaidi. Hasara ya kwanza itakua ni ajira zaidi waka tatizo mojawapo linaloing'oa CCM hivi sasa ni kushinwa kwake kuzalisha ajira kwa vijana.

Pili, kwa uzoefu juu ya vyombo vya habari vinavyofanya kazi zao, hatua hiyo huenda ikaharakisha zaidi kifo cha CCM kwa hofu ya vyombo vingine ya kwamba siku yoyote na wao wataondolewa hivyo ni heri kufanya kila waliwezalo kuhakikisha kwamba serikali inaondoka kwanza.

Tatu, ikumbukwe kwamba Mhe Kikwete anarejea nchini na majeraha mapya kwa madai kwamba AMEONEKANA KUUNGA MKONO SERIKALI KUUA WANANCHI WAKE NA KUWANYIMA WAFIWA KUPATA HAKI MAHAKAMA YA KIMATAIFA ICC.

Msimamo huo aliouchukua Kikwete imetafsiriwa na wadadisi wa mambo kwamba ni sawa na kusema kwamba pindi tutakapombana juu ya mauaji ya wenzetu kule Arusha na Mbarali basi naye wenzake wammunge tu mkono kuzima sauti zetu zisisikike.

Kwa lugha nyingine, maraisi madikteta waonekana kuteka mikutano ya EAC na AU kama vyombo vya kutumika kuminya sauti huru za vyama vya upinzani katika nchi zao na kusaidiana katika hila mbalimbali dhidi ya matu wanaowaongoza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom