Nationalisation is back: Utaifishaji kwa manufaa ya umma!

Mkuu hizi ni mada ngumu kidogo kwa vijana wa kileo. At any rate sijui kama wengi wao wana kumbukumbu ya kupitia kwenye vitabu vyao vya historia ya uchumi wa Tanzania,hapa tumsubiri prof Lipumba kuelezea.
Hata hivo mimi naunga mkono urejeshaji wa mali ya umma,
Vijana wa kileo ni mbumbumbu au? Tutafikaje ikiwa mada mlizo na uwezo nazo ni ngono, mapenzi, muziki na michezo tu? Kama hamuwezi mada ngumu je changamoto ngumu kwenye ajira mtaziweza?
 
nadhani bado sana, elimu kwanza jamanh. Just imagine in next five years gesi na mafuta ndio itakuwa kila kitu hata madini tutasahau. Je tumejiandaa vipi? Tunasomesha watu au tunasubiri expert waje?
Utasomesha watu waje wafanye nini wakati sekta nzima umewakabidhi hao wafyekaji (sorry, wawekezaji)? Wakija wanakuja na watu wao ambao wanawaamini kuwa watawafichia siri zao. Kifua cha kuwalazimisha waajiri watu wako utakipata wapi?
 
vijana nimependa mko makini kiitikadi.... Nafikiri serikali imebanwa sana na hawa WTO, IMF, WB..tukivunja hii mikataba ya sekta ya madini na kwingineko kutakua ni kukiuka masharti ya hawa mabwana ya kutaka serikali isiingilie kati uendeshaji wa moja kwa moja wa sekta za kiuchumi kwa kuimiza ubinafsishaji. Sasa na huu umaskini wetu sijui itakuaje..Argentina walikiuka haya maagizo kwa sababu hawategemei sana hivi vimisaada vya nje na wanafanya biashara nzuri na majirani zao ukiachia mbali wana soko kubwa la ndani kwa bidhaa zao za viwandani. wenzentu wanaweza huu uthubutu, sisi hatuwezi, tukimchungulia Mugabe pale, tunaogopa...
Ni woga wetu (wa viongozi wetu) tu. Hawa jamaa ukikomaa na kujenga hoja zenye mantiki au kukubali kuvikosa vimisaada vyao wanaelewa haraka. Mtazame Bob Mugabe hapo Zimbabwe. Wamemsema, wamemuwekea vikwazo, wamemfungia asitembelee kwao (kama vile ni muhimu kwenda huko) bado amegangamara. Sasa hivi wananza kurudi wenyewe. Misaada wameanza kutoa, 'wawekezaji' wanapanga foleni kutaka kurudi Zimbabwe, n.k. Na bado Bob ameamua kutaifisha makampuni ya kigeni ili hisa kubwa ziwe kwa wazawa. IMF, WB, WTO, wote ni mawakala wa kuendeleza utegemezi wetu kwa wazungu na kuendelea kunyonywa. Tukithubutu kwa pamoja tunaweza. Tatizo mtu kama JK ukimwambia hivyo atakuona mwehu.
 
Labda ndo maana Kigoda is back ili aweze REVERSE aliyoyafanya bosi wake wa zamani Big Ben
 
mfumo wa serikali za america ni tofauti na za kwetu huku...sasa serikali yetu ya hapa itaifishe viwanda alafu msimamizi wake awe mkullo?? ni bora nione mzungu au mwekezaji wa nje anafanya kazi hapa kuliko nione akina mkullo na ngeleja wakiwa in charge....
Tatizo ni nyuso za watu, rangi na wanakotoka au tatizo ni uadilifu na utendaji? Kama akina Mkullo na Ngeleja wakiwa waadilifu na watendaji wazuri mie sino tatizo. Unachosema hapo ni kuwa kila Mtanzania asilia ana uwezo mdogo au ni mkosefu wa uadilifu. Sidhani.
 
Vijana wa kileo ni mbumbumbu au? Tutafikaje ikiwa mada mlizo na uwezo nazo ni ngono, mapenzi, muziki na michezo tu? Kama hamuwezi mada ngumu je changamoto ngumu kwenye ajira mtaziweza?

Mkuu jaribu kupitia mada nyingi humu JF, zinazohitaji critical thinking ni chache sana.

Mada zinazopendwa sana ni maoni tu ya mtu binafsi na matukio yanayotokea pande mbali mbali nchini na duniani.
Sidhani kama vijana wa kileo wanauwezo wa kuchambua mada za Das Kapital ya Karl Marx,Essays on Ujamaa ya Mwalimu na maadishi mengi ya kiuchumi na kisiasa.
Siwalaumu vijana kwa vile hawakuandaliwa, elimu ya soko huria inatawala leo.
 
Mkuu scenario unayijenga ni ile yamazingira endelevu kwa maanamya uwekezaji.
Nafikiri mtoa posti hapo juu hajasoma mazingira ya Argentina na Bolivia na sababu zilizopelekea kutaifishwa kwa makampuni y YPF na TDE ya Uhispania.

Sababu walizotoa ,serikali za Argentina na Bolivia, ni waekezaji hao kukosa KUWEKEZA, kwa maana ya kuingiza mitaji katika kampuni husika.
Kimsingi kampuni hizo zilikuwa sana sana zinafanya trading tu, na si kuwekeza.
Haya ndiyo mambo tunayoyaona hata Tanzania leo kwa makampuni mengu tuliyoyabinafsisha.

Pengine nakubaliana na wewe kuwa viongozi wetu wanakosa ubunifu katika kuendesha uchumi wetu, na wengine wanafikiri uwekezaji na wawekezaji lazima watoke Ulaya, Marekani au Uchina.

Watu kama Mengi kwa kiwango fulani lazima iwe benchmark ya muelekeo wa uwekezaji nchini.
Tuelewane kitu kimoja, kuna mawazo potofu kuwa capital inaweza toka nje ya nchi tu.
Mtaji na fedha iliyokusanywa na NICOL inaondoa mawazo hayo.

Kama tunataka kuendelea kiuchumi ni lazima tujiondoe katika ukoloni wa kujitakia katika mashirika kama WTO, IMF na hata WORLD BANK.
Kama mtu anafikiri naota basi anisaidie kuelezea jinsi wakubwa hao wanavyoweza kutukopesha kuanzisha viwanda mama vya kuzalisha chuma na vinginevyo ili tushindane kikamilifu na viwanda vya West.
Sana sana tutakopeshwa kulima just enough to be alive to serve the west na kubaki soko la bidhaa zao.
Watanzania tuamke kifikra.

The whole concept ya UWEKEZAJI assumes that our country does not have enough CAPITAL hence we provide attractive conditions for capital to flow and be invested in our country. Mimi naamini kabisa kuwa hiyo ni wrong assumption kwani nchi yetu ni tajiri sana wa maliasili na mali watu lakini hatujui jinsi ya kuvitumia kwa tija. You just imagine for a moment watu wanakuja nchini mwenu na briefcase tu na baada ya muda mfupi wanakuwa matajiri wa kutupwa; licha ya hivyo nchi yetu ingekuwa maskini kiasi hicho hizo pesa [ Shilingi Trillioni tatu] ambazo Shimbo amezificha angezitoa wapi? WE should fight this dependency mindset ili tuweze kujiendeleza kwakutumia utajili wetu tulionao badala ya kuwaachia wageni wafaidike kwa kigezo cha kuleta mtaji ambao hata sisi tunaweza kumobilize.
 
The whole concept ya UWEKEZAJI assumes that our country does not have enough CAPITAL hence we provide attractive conditions for capital to flow and be invested in our country. Mimi naamini kabisa kuwa hiyo ni wrong assumption kwani nchi yetu ni tajiri sana wa maliasili na mali watu lakini hatujui jinsi ya kuvitumia kwa tija. You just imagine for a moment watu wanakuja nchini mwenu na briefcase tu na baada ya muda mfupi wanakuwa matajiri wa kutupwa; licha ya hivyo nchi yetu ingekuwa maskini kiasi hicho hizo pesa [ Shilingi Trillioni tatu] ambazo Shimbo amezificha angezitoa wapi? WE should fight this dependency mindset ili tuweze kujiendeleza kwakutumia utajili wetu tulionao badala ya kuwaachia wageni wafaidike kwa kigezo cha kuleta mtaji ambao hata sisi tunaweza kumobilize.

Mkuu nakubaliana na wewe hapo kwenye red.
Mikakati ya kuongoza uchumi wetu ina lack creativity na muono wa picha nzima kiutendaji.
Suala la watu kuingia na briefcase na kutoka na mamilioni tumejionea, na si kwamba sisi ni mazezeta ila tu tumependa kuikubali hali hiyo kama nchi.
 
Hivi Mkuu Lole Gwakisa!

Naomba ufafanuzi kidogo, kuna stori nimekuwa naisikia eti kwenye historia ya uchumi wa taifa flani hivi, hiyo nchi ilifilisika kabisa hadi hazina yao iliishiwa kabisa na kubaki na vipande vichache sana vya dhahabu.
Nasikia mtawala wa nchi hiyo akaitisha mkutano mkuu wa wataalamu wazawa, wataalamu wote wa maeneo yote ya uchumi wa nchi, akawapa assignment kuwa wampe JIBU la dira ya nchi.
Nasikia hiyo nchi sasahivi ni inafanya vizuri sana na ni miongoni mwa nchi za "Ulimwengu wa kati"...!

Sasa naomba ufafanuzi kidogo, ni kwelli kuna hadithi ya namna ya namna hii??
Iwe kweli au isiwe kweli, je inawezekana kuwa na kitu cha kitaifa cha namna hiyo??
Mi nadhani kwa hali tuliyopo sasa tunahitaji muafaka wa namna hii...

Mkuu jouneGwalu unachosema kina ukweli ndani yake.
Nchi ya Tanganyika wakati wa uhuru ilikuwa na kipato,GDP, karibu sawa kama si kuzidi nchi kama Malaya(leo Malaysia),Indonesia,Thailand,Singapore na hata nchi zilizopita kipindi kigumu sana cha vita kama Vietnam(zote mbili).

Leo nchi hizi hazikamatiki kwa maendeleo.

Kuendelea kwa nchi ni lazima kuweka mikakati iliyoendelevu na kuifanyia kazi bila kutoa sababu za kushindwa.
Nchi yetu tunaridhika kuwa na viongozi wenye uwezo mkubwa wa kuelezea mattaizo yetu bila kuwa na uthubutu wa kutekeleza mikakati ya KULAZIMISHA maendeleo.
Kulazimisha maendeleo ni pamoja na kufanya kazi kwa nguvu zote-tabia mabayo waTanzania inatupiga chenga.
Wengi wetu wamezoea kulalamika na kutojijuhudisha kujiendeleza kiuchumi.
Wengi wananongelea dudu linaloitwa "serikali" lenyewe ambalo limejaa watu wavivu kupindukia.

Tanzania si nchi masikini hata kidogo , umasikini tulio nao ni kukosa maarifa kiuongozi.
Wachina wamekuja juzi hapa(kama wiki tatu zilizopita) na wameshangaa tunapojiita masikini wakati tumejaaliwa kila kitu.
Cha mjinga huliwa na mwerevu!

Hivyo basi kama mikakati ya maendeleo ingetayarishwa ili kila mtanzania kwa mfano angefanya kazi, ingalau kila mtu afanye kazi ya kuongeza kipatao kwa walu 10%, Tanzania ingepaa!
 
Hili halihitaji hata vitabu vya kihistoria wala uchumi kulifanya. Ni lazima tu lifanyike hata akija rais amabaye hajaenda shule. Hali halisi ya nchi hii inahitaji hili, na si tu utaifisha vyanzo vya uchumi bali hata wahujumu uchumi kama NGELEJA, KARAMAGI, LOWASA, KIKWETE, MKAPA, MAIGE, n.k
 
Back
Top Bottom