Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
- Thread starter
- #21
Sr. Magdalena,
Ahsante sana kwa swali lako. Naomba kulijibu kama ifuatavyo;
NCCR iliyoundwa mwaka 1991 ndio ilikuwa kamati ya kitaifa ya mabadiliko ya katiba, yaani National Committee for Constitutional Reform.
Viliporuhusiwa vyama vingi mnamo mwaka 1992, NCCR-Mageuzi kilisajiliwa kuwa chama, lakini kikiwa si Kamati tena bali National Convention for Construction and Reform, yaani kama katiba ya chama inavyotafsiri jina hili; ni chama cha Mageuzi na Ujenzi wa Taifa.
Aidha nikutaarifu kuwa Halmashauri Kuu ya Chama ilipokutana mwanzoni mwa mwaka jana (2011), pamoja na mambo mengine iliruhusu mjadala wa kulibadili jina la chama kuwa katika lugha ya kiswahili, hivyo pendekezo lako linaendana kabisa na mchakato uliokwisha kuanza ndani ya chama.
Kumradhi, katika maelezo yako kuna kitu sijaelewa, umesema bunge limepitisha mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, ni yapi hayo?
Mkuu Kahangwa heshima mbele sana,
Nilimaanisha sheria ya mchakato wa mabadiliko ya katiba, nimebadilisha kwenye post yangu, na nashukuru kwa kunirekebisha.
Nadhani itakuwa jambo la busara sana kufanya mchakato wa kupata jina jipya, tena la kiswahili ili mtanzania wa kawaida aelewe chama kinasimamia nini na kina amini nini, na mabadiliko haya yangefanyika haraka ili muweze ku rebrand jina hilo na watu kulizoea kabla ya 2015, naamini chama chenu kikiwa strong kama CDM itakuwa ni jambo jema sana kwa mstakabali wa taifa letu, na je unaweza kutueleza japo kwa kidogo makubaliano mliyo tiliana sahihi na CDM ni yapi na nyinyi kama chama mnadhani yatawasaidia vipi? Kwa kuwa kubwa linalozungumzwa ni ufutaji wa kesi ya mwenyekiti wenu na mbunge wa CDM kawe.