National Committee For Constitution Reform (NCCR)

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
472
Ni katika msingi huo, NCCR- Mageuzi kama chama cha siasa ambacho asili yake ni madai ya katiba mpya kuanzia uasisi wake kwa maana ya Kamati ya Taifa ya Madai ya Mabadiliko ya Katiba (National Committee For Constitution Reform (NCCR) iliyoketi tarehe 11 na 12 Juni 1991 na baadaye kujibadili kuwa chama cha siasa mwaka 1992).

Je vijana wa NCCR hamuoni sasa ni wakati muafaka wa kubadili jina la chama chenu, kwa kuwa mchakato wa katiba mpya umekwisha anza, au mnasubiri hadi katiba mpya ipatikane.
 
hoja ime bakwa na ccm!nccr ndio wa anzilishi wa madai ya katiba mpya
 
Sr. Magdalena,
Jambo haliwi mpaka limekuwa, na ijapokuwa mawingu ni dalili za mvua, mvua haijanyesha bado na inavyoelekea huenda ikanyesha ndivyo sivyo.
 
NCCR sio chama,
Ni kamati tu kama kamati zingine za msiba, harusi, kitchen party, n.k
Ndio maana hawaeleweki eleweki
 
Sr. Magdalena,
Jambo haliwi mpaka limekuwa, na ijapokuwa mawingu ni dalili za mvua, mvua haijanyesha bado na inavyoelekea huenda ikanyesha ndivyo sivyo.

Acha kuongopea watu mkuu,
Vitu vingine unaweza kuamua kuving'ang'ania vikakugeuka baadae,
We mwenyewe uliona huko kamatini "sio" ukaamua kujiweka kando,
Sasa unatetea nini tena?
 
Kuna NCCR mbili, Moja ni ya yule bwana mchagga, mambo ya pwani na ya CCM yamemuelemea, na kuna NCCR ya wana harakati. Hii iko hai na itadumu, ila ile NCCR CCM itakufa soon
 
Mkuu umekosea kidogo. NCCR -Mageuzi haikuwa na nia ya kudai katiba mpya na hata kirefu chake umekikosea kidogo. hiyo inaitwa National Committee for Construction and Reform -Mageuzi na sio Consitution kama ulivyoandika. Lengo lao ilikuwa ni kudai mabadiliko katika mfumo wa siasa na katiba ilikuwa ni kipengere kidogo tu ndani ya madai yao ya mabadiliko. Lakini ulicho sahihi ni kwamba ilikuwa ni kamati tu ya kudai mabadiliko ya mfumo wa siasa na baada ya mfumo kubadilika kamati ikajigeuza na kuwa chama cha siasa.
 
Acha kuongopea watu mkuu,
Vitu vingine unaweza kuamua kuving'ang'ania vikakugeuka baadae,
We mwenyewe uliona huko kamatini "sio" ukaamua kujiweka kando,
Sasa unatetea nini tena?
Kumradhi Shark,
sijakuongopea wewe wala awaye yeyote. Hiyo habari ya kujiweka kando ilipotoshwa. Mimi ni mwanachama hai wa NCCR, na usitarajie iwe vinginevyo. Baada ya NCCR kubadilishwa kuwa chama, neno Committee liliachwa, badala yake neno lililoko kwa msajiri ni Convention.
 
Mkuu umekosea kidogo. NCCR -Mageuzi haikuwa na nia ya kudai katiba mpya na hata kirefu chake umekikosea kidogo. hiyo inaitwa National Committee for Construction and Reform -Mageuzi na sio Consitution kama ulivyoandika. Lengo lao ilikuwa ni kudai mabadiliko katika mfumo wa siasa na katiba ilikuwa ni kipengere kidogo tu ndani ya madai yao ya mabadiliko. Lakini ulicho sahihi ni kwamba ilikuwa ni kamati tu ya kudai mabadiliko ya mfumo wa siasa na baada ya mfumo kubadilika kamati ikajigeuza na kuwa chama cha siasa.
Meneno aliyotumia Sr. Magdalena yanarejea katika ukweli wa historia ya NCCR-Mageuzi (chimbuko lake)
 
Kumradhi Shark,
sijakuongopea wewe wala awaye yeyote. Hiyo habari ya kujiweka kando ilipotoshwa. Mimi ni mwanachama hai wa NCCR, na usitarajie iwe vinginevyo. Baada ya NCCR kubadilishwa kuwa chama, neno Committee liliachwa, badala yake neno lililoko kwa msajiri ni Convention.

Ilipotoshwaje tena mkuu??
Nakumbuka wewe ndie ulietuambia kua unang'oka uongozi (sio uanachama),
So kama ni issue za kupotoshana basi wewe ndie ulietupotosha!!!
 
Ilipotoshwaje tena mkuu??
Nakumbuka wewe ndie ulietuambia kua unang'oka uongozi (sio uanachama),
So kama ni issue za kupotoshana basi wewe ndie ulietupotosha!!!

Ndugu yangu Shark,
Aking'oka mtu uongozi wa chama hatakiwi kusema lolote kuhusu chama ambacho yeye anaendelea kuwa mwanachama hai?
 
Ndugu yangu Shark,
Aking'oka mtu uongozi wa chama hatakiwi kusema lolote kuhusu chama ambacho yeye anaendelea kuwa mwanachama hai?

Heshima mbele sana mkuu Kahangwa.
Mabadiliko ya sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya yamepitishwa leo na bunge la JMT, je bado hamuoni ni wakati muafaka wa kubadili jina la chama, napendekeza kama lingekuwa la kiswahili, na hakika wanachama wengi wa NCCR hawajui kirefu chake na wala kinasimamia nini...
 
Hamna kitu hapa, iimarisheni NGO yenu, watu kama akina Kafulila hawawezi kuishi humu.
 
Heshima mbele sana mkuu Kahangwa.
Mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yamepitishwa leo na bunge la JMT, je bado hamuoni ni wakati muafaka wa kubadili jina la chama, napendekeza kama lingekuwa la kiswahili, na hakika wanachama wengi wa NCCR hawajui kirefu chake na wala kinasimamia nini...
Sr. Magdalena,
Ahsante sana kwa swali lako. Naomba kulijibu kama ifuatavyo;
NCCR iliyoundwa mwaka 1991 ndio ilikuwa kamati ya kitaifa ya mabadiliko ya katiba, yaani National Committee for Constitutional Reform.
Viliporuhusiwa vyama vingi mnamo mwaka 1992, NCCR-Mageuzi kilisajiliwa kuwa chama, lakini kikiwa si Kamati tena bali National Convention for Construction and Reform, yaani kama katiba ya chama inavyotafsiri jina hili; ni chama cha Mageuzi na Ujenzi wa Taifa.
Aidha nikutaarifu kuwa Halmashauri Kuu ya Chama ilipokutana mwanzoni mwa mwaka jana (2011), pamoja na mambo mengine iliruhusu mjadala wa kulibadili jina la chama kuwa katika lugha ya kiswahili, hivyo pendekezo lako linaendana kabisa na mchakato uliokwisha kuanza ndani ya chama.
Kumradhi, katika maelezo yako kuna kitu sijaelewa, umesema bunge limepitisha mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, ni yapi hayo?
 
Kahangwa=Mtatiro!! Right person in a wrong place! Mtatiro ndio anazidi kuchafuka! Kahangwa namuombea "aone" mapema! Bado tunamuhitaji!
 
Back
Top Bottom