Natetemeka/Kigugumizi nikiongea Kiingereza

Hahahah, lol mbavu sina mie kama hujui kizungu ushauri wa kutumia viroba ni upuuzi utaendelea kubonga broken bila kua na aibu sasa kama sio kujiabisha nini?

Pombe inamsaidia yule anaeijua hiyo lugha ila hana confidence mbele za watu... Ila kama huna unachokijua hata ukinywa kreti zima la bia unajisumbua... Tatizo waTz tunafikilia kwa kiswahili halafu tunataka kuiwasilisha fikra ya kiswahili kwa kiingereza kitu ambacho ni ndoto za mchana ndio maana unakuta mtu anaongea kiingereza mbele ya kadamnasi ghafla anatokwa na maneno ya kiswahili kwa kua hiyo ndio lugha anayoitumia kufikiria kabla hajatamka neno anatafsiri kwa kiingereza mwenyewe ndio analitoa kwa kadamnasi ndio maana wengine wanadai wanapatwa na kigugumizi kumbe ni kwa kua kuna process kibao zinafanyika kichwan kwake kabla hajatamka neno la kiingereza.. pia
You can learn how to speak a proper and fluent english by first leaning how to talk to yourself and answer yourself (personal dialogue) if you can manage this excise you can make it
 
Kuna siku nilienda ofisi fulani nilikuwa na shida na marketing manager katika hiyo ofisi kubwa tu.
Baada ya kumweleza secretary kwa ufupi akaenda kuniitia bwana.
Yule jamaa alikuwa mzungu inaonesha anatokea london mjini kabisa kwa akina blair, kingereza chake kilikuwa hakieleweki yaani anacharaza kama cherehani, labda akiongea ufanye kuandika kwanza. Yaani ilikuwa aibu pale.
Ili kujinasua, nikatema yai broken mfulululizo bila kumpa nafasi ya kuongea halafu nikasema thank you, nikamwambia secretary utamwelekeza vizuri kama nilivyokwambia eeh!
Ndio maana hiyo lugha siipendagi kabisa.

Lol!!
 
Ha ha ha ha
 
Tatizo ni "UNAFIKIRI KWA KISWAHILI HUKU UNAONGEA KIINGEREZA"

mimi sio mzuri sana wa lugha hiyo ila kama unataka kuijua..jitahidi kujiwekea mazingira ya kukijua zaidi kama kuangalia tamthilia
 
Maana lazima niielewe hiyo lugha kiufasaha. Maana job cheo kimepanda na nakutana sana na watu wanaoongea hiyo lugha nisije kuzidi kutia aibu.
 
Wadau hii hali inanikuta nikitaka kutema yai sijui kwa nini tena nikiwa kwenye kadamnasi napata ubaridi zaidi. Msaada jamani naaibika mwenzenu.
watu wengi kingereza kigumu kuna jamaa mmoja nilimuona juzi alikuwa anahojiwa nilitaka ingia chini ya uvungu kwa aibu jamaa is too good lakini alivyoongea kingereza nikaona tunapaswa kulishikia kidete kuanzia chini
 
Kiingereza ni lugha muhimu katika kazi na kujifunza mambo mengi hapa ulimwenguni. Mwenye upeo mkubwa wa lugha hii anao uwezo mkubwa vile vile ya kufanya na kujifunza mengi. Kujua lugha yoyote ni kujifunza kwa kusema, kusikiliza na kuandika yaani kujifunza kwa vitendo ni njia nzuri yenye mafanikio makubwa ya haraka. Kwa hiyo ningekushauri ufanye mazoezi mengi bila hofu wala haya kwani hawa ndo maadui wakubwa katika kujifunza. Hata ukikosea husione aibu endelea na husisite kujiunga na wanaojiendeleza katika maeneo ya kujifunza Kiingereza mbali mbali si lazima British Council.
 
Pole sana ni hali ya kawaida hiyo mkuu haswa kwa watu wasiojiamini,iwe kutokana na matatizo ya kimaumbile ambayo hayaonekani au athari za malezi au ajali miaka mingi iliyopita sasa leo nakupa dawa isipokusaidia utani PM ili nikushauri namna ya kunipata au kupata wataalam wa ushauri(matatizo ya kisaikolojia)kama utakuwa unapatikana mbali na nilipo mimi,maandalizi ya kabla ya kuongea weka sauti yako vizuri(iwe kwa maji ya kunywa au kukohoa),kumbuka kuvaa nguo zinazokupa kujiamini bila mashaka yoyote(zinakutosha vizuri,sio kubwa wala ndogo kwako),kabla ya kuongea SHUSHA PUMZI NDEFU SANA MARA MBILI INATOSHA KABISA,penda kuongea taratibu bila pupa iwe kama bwebwe na kama unafikiria ila bwebwe zisiwe kama za Kitwanga Mabia
USIOGOPE KUKOSEA KWANI NDO SEHEMU YA KUJIFUNZA
 
MGOGO! Ngoja nifanye mazoezi maana j4 nakutana na wazungu fulani lazima nijiweke sawa. Mimi nipo Halmashauri fulani (Jina kapuni) sasa hao wazungu wanataka kuja kuwekeza lazima tuongee nao kwa kina! Daah Aisee namlaumu Babu wa Taifa hili kwa kukazania KISWAHILI tu. Ona sasa tunavochoreka na Digrii zetu za SAYANSI. the the the kibao. Najuta kusoma Bsc.
 
Hahahah, lol mbavu sina mie kama hujui kizungu ushauri wa kutumia viroba ni upuuzi utaendelea kubonga broken bila kua na aibu sasa kama sio kujiabisha nini?

Pombe inamsaidia yule anaeijua hiyo lugha ila hana confidence mbele za watu... Ila kama huna unachokijua hata ukinywa kreti zima la bia unajisumbua... Tatizo waTz tunafikilia kwa kiswahili halafu tunataka kuiwasilisha fikra ya kiswahili kwa kiingereza kitu ambacho ni ndoto za mchana ndio maana unakuta mtu anaongea kiingereza mbele ya kadamnasi ghafla anatokwa na maneno ya kiswahili kwa kua hiyo ndio lugha anayoitumia kufikiria kabla hajatamka neno anatafsiri kwa kiingereza mwenyewe ndio analitoa kwa kadamnasi ndio maana wengine wanadai wanapatwa na kigugumizi kumbe ni kwa kua kuna process kibao zinafanyika kichwan kwake kabla hajatamka neno la kiingereza.. pia
You can learn how to speak a proper and fluent english by first leaning how to talk to yourself and answer yourself (personal dialogue) if you can manage this excise you can make it

Ila tuwekane sawa hapa jamani, Wanajamvi [ JF ] USINYWE POMBE UKAENDA MBELE YA UMATI hata kama wajua kutema YAI, utaharibu mambo mengine kutokana na pombe zako hizo sijui kiloba/mzinga au mbunduki mmii sioni mantiki ya pombe na kuongea katika umati wa watu au kutema YAI, ILA WEWE FANYA TU MAZOEZI YA KUONGEA UTAWEZA SIO KILA MTU ANAEONGEA KATIKA UMATI/JOPO LA WATAALAMU ANAKUWA KANYWA POMBE ILI KUONDOA AIBU....

WE JIFUNZE PUBLIC SPEAKING NA ONA NI JAMBO LA KAWAIDA KUONGEA NA WATU/ KIKUNDI

JAMBO LA MUHIMU HAPA , HEBU ELEWA MADA UTAKAYOZUNGUMZIA [MASTER YOUR TOPIC/THEME]

Pia, Tafuta kituo ujiendeleze usione aibu hii lugha ilikuja kwa meli huku Tz hivyo usione sooo , kujifunza hata kama uko mkubwa au boss.

Mi niitoka Tz 2014 nikaenda masomoni nikajifunza kifaransa sasa hivi nagongo vizuri sana kifurenchi hivi na sikuwa na uoga. Nimetumia mwaka mzimana miezi mitatu kujifunza.

Ila pombe, utavuanguo au utajivua nguo bure mbele ya kandamnasi aiseee kwa kueleza pumba ukifikili uko sawa , maana umeshaharibu utashi wako wa kutathimini mambo!!

Asanteni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom