Natangaza vita rasmi kati YANGU na WACHINA

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Mdugu zangu naomba popote mtakapokutana na Mchina mniite haraka ili nije nilipe kisasi. Nimenunua Nokia 6680. Simu ambayo nimekuwa nikiitafuta kwa muda mrefu sasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukamata network. Kwa ndani ya simu hii kulikuwa na kikaratasi kilichogundishwa vizuri kikiwa na maandishi 'made in Finland'. Tatizo la simu hii, kutwa nzima mpaka sasa nishachaji mara 3. Nikapata wazo na kubandua kile kikaratasi. Ndipo kwa ndani nikakutana na maneno mengine tena 'made in China' Hawa jamaa ni kweli pamoja na kuwa wana bindhaa bora hizi feki wanatuletea za nini?.
 
Sasa waliokuuzia ni wachina au wale shombeshombe wanaoenda china kununua vitu feki............maana nikikumbuka utumwa tuliuzana wenyewe kwa wenyewe.
 
Sasa waliokuuzia ni wachina au wale shombeshombe wanaoenda china kununua vitu feki............maana nikikumbuka utumwa tuliuzana wenyewe kwa wenyewe.

Acha nianze na walioniuzia kwanza kisha ndo nianze kuwasaka wachina. Nasikia siku hizi wanalangua hadi samaki pale feri.
 
Aaaah!! Kumbe umenunuwa K'koo. Jamaini, si ungekuja kwanza kuuliza hapa Jamvini. Pole, sina msaada.
 
Pole, lakini nimecheka sana, unajiamini nini na hayo majambia yako. Make japo wachina wanauza bidhaa feki, kwa kung-fu wako fiti, usije kupata hasara mara mbili!
 
Nimeonana na hawa jamaa na kuwapa vipande vyao. Naona kuna mchina hapa jirani muuza pikipiki alikuwa anatizama kwa jicho kali wakati natukana bidhaa za kichina live. Jamaa naona anajua kiswahili. Wamekubali kunibadilishia na kunipa nyingine ya bei ndogo kidogo hii iko bomba. Ila kuna kitu nimegundua, vikaratasi vya kuonyesha simu imetengenezwa wapi washenzi wanabandika wenyewe ili mnunuzi asijue ishu ni ya kichina. Hawa TBS likizo yao itaisha lini?
 
ha ha ha ha.....ni sime hiyo! Pole mkuu. kosa linaweza kuwa hata limefanyika hapa hapa nchini au kule hong kong wanakoenda wafanyabiasha. nasikia stika za made in Finland zinapatikana buree kwa wingi inategemea na uhitaji wako.
Nina bisu la kimasai lenye makali kotekote!
 
Ukitangaza vita na wachina utakuwa unakosea wewe tanganza vita na waliokuuzia pale kariakoo!
 
Back
Top Bottom