Natangaza kugombea ubunge 2015 - ROMBO kwa tiketi ya CHADEMA

Ndugu Leyana, nakupa ushauri wa Bure kama wameku (wazee) wamekufuata, naona kuna shida nataka kujua wewe unataka kuifanyia nini Rombo, na je ndani yako kunasemaje kuhusu hiyo nafasi?? Hiyo ni ndoto yako au ya wazee waliokufuata?? I would like to hear your own dream and vision please!!!

Ndugu Mkenda,tangu zao la kahawa lianze kuyumba kwa maana ya ukame na bei duni katikati ya miaka ya 1990 rombo imechoka sana kiuchumi. Mkakati wangu ni kufanya migomba kuwa zao la biashara,kwa sasa kuna jamaa wa Poland nazungumza nao tufungue kiwanda cha mikeka kwa kutumia marawa ya migomba ambayo ni by-product. Mkuu kuna mengi tu ambayo nimeplan kwa kutumia taaluma yangu ya rural develpment.
 
Hongera kamanda tuwekee cv yako hapa na mipango yako utakayo wafanyia wanrombo ili tuanze kuidadavua.

CV yangu ni; Masters of Community development- Kenyatta vasity Nairobi 2010, Postgraduate diploma of Rural development-Dodoma Inst.of dev.planing 2008. Bachelor of PSPA- The Open vasity of Tz. 2007,Diploma in Animal Health [DAH]- Kabete-Uganda 2005.
 
Anza kwa kuonyesha jambo na si majigambo mkuu...umefanya nini ata kimoja tukuamini mzee
 
Mkuu mh. Selasin namheshimu sana hata 2010 nilimpigia kampen na niliwashauri waliokuwa wananisapoti kura wampe Selasin. Ninachotaka kufanya 2015 ni kutimiza haki yangu kikatiba na sio usaliti, ndo maana kuna periodic election. Hata CDM ikimpa tena mh. 30 ridhaa au mwingine yeyote mm sina fuvu tete nitawasapoti kwa 100% kuhakikisha jimbo haliendi kwa magamba!
 
Wewe hujaguswa na matatizo ya wananchi wa rombo bali umeguswa na matakwa ya wazee watatu wa rombo.
 
Hao ni wazee umri ushaenda na kiama kinawaita,vijana hatukupi kura full stop.
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani mbunge aliyepo Mh J.Selasini (chadema) alivyoshindwa kufanya kazi yake, mpaka anapata mpinzani ndani ya chama chake baada tu ya miaka 2 ya kipindi chake cha ubunge.
Hamna mbunge wa upinzani aliyewahi kuwa mbunge kwa vipindi viwili mfululizo and after all kutangaza nia ni kutumia haki yako ya kikatiba kama mtoa sred alivyofanya so hakuna connection na utendaji kazi wa mbunge wa sasa...
 
Ahsante kwa kutufungua macho na kutuambia kwamba na wewe unaungana na wananchi wengi wengine waliochoshwa na utendaji duni wa mbunge wako wa chadema. Huu ni uungwana wa hali ya juu!
 
Leyana Lesindamu Rombo kwa sasa siasa yake imebadilika watu wanahitaji maji, umeme na vituo vya afya vya kuwatosheleza tuambie manifesto yako ime adress vipi hili swala pili kuna siasa za kitarafa zimeibuka mfano mzuri watu wa maeneo ya Nanjara,Tarakea,Kikelelwa,Rongai kwenda hadi kamwanga wanahitaji mtu kutoka maeneo hayo awawkilishe umejiandaa vipi kukabiliana na changamoto hii na je wewe uanatokea maeneo hayo! Kama ndivyo waeleze wanarombo kama msukumo wako binafsi na hao wazee waliokufuata unatokana na changamoto hii au la!
 
una mawazo mazuri but kabla hatujakushaur ebu tupe background yako ya chama , unafanya nin kwa sasa ! una lipi unataka kuwafanyia Warombo ambalo halifanyika! na umejipangaje?
 
Kwanza, unaishi Kilindi, unawaza kugombea ubunge Rombo
Pil,i Mbunge wa Rombo ni CDM
Tatu, ulifuatwa na wazee watatu wanakuomba ugombee ubunge wa Rombo, which means tayari una kura tatu za hao wazee.
Natangaza rasmi 2015 nitagombea ubunge-Rombo kupitia CDM. Nimeamua kufanya hivyo baada ya kutafakari kwa mda mrefu maombi ya makundi mbalimbali ya jamii ya wana Rombo kugombea tangu mwaka 2005 na hivi juzi ujumbe wa wazee watatu wa Rombo walinifuata Kilindi-TANGA ninakofanya kazi wakinitaka nisiwaangushe 2015. Wadau nishaurini.
 
mkuu wazee watatu sijifagilii,ila nikuambie tu kwamba mm ni muumini wa demokrasia pana. Kama CDM kitanipa ridhaa nitawatumikia kama la nitamsapoti alieteuliwa kwa manufaa ya wana Rombo na chama kuepusha mpasuko usiokuwa na maslahi.

Hili ndo muhimu sana katika demokrasia ya kweli. Ila nakushauri katika mchakato wa kupeperusha bendera mtakua wengi kabla ya kupata ridhaa. Nakushauri uwe makini na kauli zako dhidi ya wapinzani wako, hii itakupunguzia maadui na itarahisisha usuruhishi pale patakapoonekana mgogoro. Kugombea haina maana kua aliyepo ameshindwa, anaweza akawa amefanya mazuri wewe ukaenda kuongeza mazuri zaidi. Kila la kheri katika safari yako.
 
Natangaza rasmi 2015 nitagombea ubunge-Rombo kupitia CDM. Nimeamua kufanya hivyo baada ya kutafakari kwa mda mrefu maombi ya makundi mbalimbali ya jamii ya wana Rombo kugombea tangu mwaka 2005 na hivi juzi ujumbe wa wazee watatu wa Rombo walinifuata Kilindi-TANGA ninakofanya kazi wakinitaka nisiwaangushe 2015. Wadau nishaurini.

Acha habari hizo. Unataka kugombea kwa sababu umefuatwa na "wazee watatu" au kwa sababu una cha kuifanyia Rombo. Weka sababu za msingi zinazokufanya ugombee hapa tuzijadili kama zina mashiko na sio mambo ya paukwa-pakawa.
 
Hongera kwa kutangaza nia hapa JF maana hata william malecela alitangazia nia ya kugombea EAST AFRICA LEGISLATIVE ASSEMBLY hapahapa bila kujua wengi wetu si wapiga kura!
 
Hongera mkuu! na mm hapa nipo natafuta mtu atakayekuwa tayari kwenda kumn'goa Rage tabora ili nimuunge mkono.
 
Mkuu unacheza na Rombo wewe. Yaani Mzee Pesambili alifanya kila kitu cha maendeleo kule Rombo. Alitumia uwaziri kupeleka miradi ya barabara mingi huko Rombo, akawalipa watu waliovunjiwa nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara lakini wapi. Joseph Selasini akaja akauangusha mbuyu. Siasa za Rombo ni ngumu mno na hazitabiriki. Waulizeni akina Sarakana wanazijua vizuri.

Ni kweli kaka Wananchi wa Rombo hawachezewi.

Tupo wengi mzee tutakaogombea.Mimi nina mpango wa kugombea au kuunganisha nguvu na Ben,ila bado mapema tunatafakari.
Ekellei,

Thanks
mkuu haina shida hata Ben kuna kipindi niliongea nae akaonesha hisia za k ugombea. Lakin kinachoitajika ninamna gani ya kuifanya mpya Rombo yenye matumaini kiuchumi na kijamii.

Leyana Lesindamu,

Hongera kwa kutumia haki yako kidemokrasia.Tujenge chama kwanza.Nina imani Rombo watajitokeza wagombea zaidi ya 30 hadi ifike 2015

Ila sikumbuki kuongea na mtu mwenye jina hili kuhusu jimbo la Rombo
 
Back
Top Bottom