Natamani Watanzania wayasuse makampuni ambayo Rostam na mafisadi wenzake wana hisa

theophilius

Senior Member
Nov 19, 2010
150
54
Hivi kwa nini Watanzania wanaochukia rasilimali za taifa kuibwa na mafisadi tusichukue hatua dhidi ya mafisadi, angalau wale wanaojulikana. Tunaweza kuanza kwa kususia bidhaa na huduma za makampuni ambayo ama rostamu na mafisadi wenzake wanamiliki (au kuwa na hisa) ambayo kwa kadri habari zinavyoendelea kujipambanua, rasilimali (wafanyakazi/magari/fedha) za makampuni hayo zinatumika katika vitendo vya kifisadi.

Ikiwa watanzania wataonesha chuki dhidi ya Vodacom, New Habari na mengine wanahisa wasafi wengine wa makampuni hayo watafukuza mafisadi kutoka makampuni hayo vinginevyo yafe kwa kukosa biashara hapa nchini.

Vinginevyo, mafisadi hawa wataendelea kupeta wakichota huku na huku kwani hakuna anayeweza kuwapeleka mbele ya sheria maana wameitia serikali mfukoni, ni budi sasa 'Nguvu ya Umma' itumike na kwa hakika ikifikia mahali ikatumika watakimbia wenyewe nchi na litakuwa funzo kwa wengine!
 
Aisee, hii ni idea nzuri sana. Naunga mkono kwa asilimia 100. Tuanze kwa kutonunua magazeti ya fisadi rostam.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom