Elections 2010 Natamani sana mtu akanushe mambo haya kiuhalisia

TandaleOne,


  1. Kujenga Zahanati bila kujua kuwa watu wamezitumia hizo zahanati haiwanufaishi watanzania
  2. Kuongeza idadi ya vituo vya afya bila kuwa na takwimu watu wangapi wamepata huduma bora za afya haisaidii
  3. Idadi ya madaktari walioondezeka inahusu wale waliofanya kazi nchini au ni waliosajiliwa bila kujali wameenda kufanya kazi wapi?
  4. Matokeo ya idadi ya wauguzi kuongezeka ni nini?
  5. Baada ya kugwa vyandarua malaria morbidity imepungua kiasi gani? maana niliona watu wanatumia vyandarua kuvua samaki?
  6. Ongezeko la machine za ulizozitaja zimesababisha wagonjwa wangapi wkapata huduma bora za afya? na maisha kiasi gani yameokolewa kutokana na mashine hizo?
  7. HUKO KWETU WAZEE HUJISIFIA IDADI YA NG'OMBE HUKU WAKIENDELEA KUISHI MAISHA YA KIMASIKINI.NG'OMBE HALIWI MPAKA AFE NA HAUZAWI MPAKA KUWE NA KESI LAKINI HAWEZI UZWA KWA SHUGHULI ZA MAENDELEO.
  8. Tueleze outcomes ya hayo uliyoyasema ili utuondoe shaka la sivyo tutajua unahitaji msaada wa haraka.

Jamii inahitaji watu kama wewe.Critics.Ni changamoto ili kufanikiwa zaidi
 
naungana na Safree, mijitu mingi humu yanatoa maneno machafu badala ya kupinga kwa hoja, si heri hata Rev kakosoa toka 5% to 5.7% ambayo kwa ukaribu anaungana na mtoa hoja. Watu wa Chadema kwenye jamii forum, tuchangie hoja sio maneno machafu. penye ukweli tukubali, mabadiliko tuyafanye kwa kuboresha
 
Nakumbuka,mwaka jana kuna mtu mmoja muhimu pale muhimbili aliugua sana.akapimwa akaoneka kuna damu inavuja tumbo lakini kila wakijaribu kuangalia inatokea wapi haikujulikana.akazunguka hospitali mbili tatu zile za mahela mengi,mojawapo akaambiwa ana moyo mkubwa.baadae wenzie wakamshauri aende India akagoma,lakini baadae akakubali.kwa maelezo yake alipofika walimuuliza anatokea wapi?alipowajibu tza,walicheka sana na kusema wanajua.alikutwa tatizo lake ni uvimbe tumboni.sasa akauliza yeye ana uwezo wa kwenda India.Je watz wa kawaida inakuaje?Tandale One,Uwingi si hoja!
 
waacheni watz wataamua mbichi na mbivu, statistics za nchi hii zinamapungufu mengi sana, so inategemea hizo statistics alikozitoa zimefanyiwa kazi au la
 
:A S-danger::A S-danger::A S-danger:
 

Attachments

  • Dirty water.jpg
    Dirty water.jpg
    8.8 KB · Views: 22
  • Tanzania-192-setting-550W.jpg
    Tanzania-192-setting-550W.jpg
    38.6 KB · Views: 24
  • 22.jpg
    22.jpg
    28 KB · Views: 24
  • malibwi_water_children_op_.jpg
    malibwi_water_children_op_.jpg
    11.5 KB · Views: 25
Back
Top Bottom