Natamani Kuwekeza Kwenye Movie Industry Hapa Tanzania

Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,707
638
Hakika mambo niliyoyashuhudia leo wakati watanzania tukihitimisha safari ya mtanzania mwenzetu Steven Kanumba, yamenipeleka kwenye fikra nzito za utajirisho. Nilikuwepo viwanjani Leaders na baadaye makaburi ya Kinondoni. Ule umati wa watu uliokuwepo na simulizi za wananchi wale wa kawaida sana niliowaona,yamenifanya nitambue kuwa watanzania kumbe ni wapenzi sana wa tasnia ya Filamu, hususani filamu za Kiswahili za Kitanzania.

Nimeona huu ni mtaji wa kutokea kama nikijiweka sawa. Ninatamani kuwekeza kwenye hii fani...na Inshallah naomba Mola anisaidie. Kuna pesa nyingi sana katika burudani hii ya filamu hapa Tanzania, ambayo naamini, hakuna mtu aliyechukulia hii fani serioulsy hadi leo yamefunguka haya yaliyofunguka.

Wananchi wa Tanzania wanapenda sinema zao...Lakini wanachokipata nadhani hakikidhi haja... Unahitajika uwekezaji hapa...
 
Ni kweli wapo wanaopenda.., lakini sijui ni wangapi wananunua na wangapi wanasubiri copies za jirani au ni wazee wa piracy.., vile vile wanachopata sidhani kama kinakidhi... (nadhani acting ya bongo leave a lot to be desired)
 
Nakubaliana na wewe STAW, kuwa unahitajika utafiti, kujua unayosema kama wanunuzi ni wangapi, na wanaofanya piracy pia ni nani (wanaosababisha kipato cha wasanii kisikidhi)...huo ndio ninaouita uwekezaji, pamoja na kuboresha mazingira ya usanii wenyewe. Kuna pesa hapa...
 
na pesa nyingi wanapata (so called wadosi) wasanii wanabaki kushangaa.., ila tasnia ya movie bongo ina matatizo yafuatayo;-

Kwanza movie za kibongo hazina uhalisia na bongo watu wana-act mambo ya nje na sio vitu vinavyotokea bongo ili watu waweze ku-relate. (kwahio movie siongelee mambo ya kitanzania, vitu kama historia yetu, story kama za kina Mkwawa, matatizo yanayowapata watanzania kila siku n.k.)

Pili kwa kutengeneza pesa sana inabidi wasanii waangalia wanatengeneza movie kwa ajili ya nani (target viewers) sio kujaribu ku-target kila mtu wana-end up targeting no one.., kwahio kuwe na categories za movies kwa ajili ya soko la ndani pia watengeneze movie kwa ajili ya soko la nje (huko ndio kuna pesa zaidi sababu ya buying power ya watu huko ni kubwa)

Takupa mfano wa movie El Mariachi.., jamaa alitengeneza movie kwa ajili ya soko la nyumbani tu na kwa pesa kidogo.., ila Colombia Pictures walivyoiona wakaipenda and the rest is history (dunia nzima sasa wanaijua hii movie).

Kwahio mkuu wabongo inabidi waanze kuangalia quality na sio quantity na movie iwekewe mpaka subtitles na kila kitu au hata kuwa dubbed in different languages, watumie online media kuji-advertise.., na sio kutegemea mama mwanaisha au mama mariamu ndio anunue movie zao
 
Soko la Movie za Bongo limeshaanza kufika nje...Burundi wananchi wa kule wanajifunza/wanaboresha Kiswahili kupitia Bongo movie, Rwanda ni vilevile. Lubumbashi DRC pia wanakamata sana movie za Bongo...soko la ndani na la nje pia lipo. Msisitizo na mkazo kwenye quality na umakini unahitajika kama unavyo shauri. Soko la Afrika Mashariki lina wateja zaidi ya Milioni Mia na Ishirini.

Huo ni mtaji tosha, na segment zote zipo East Africa...angalia watu wanavyomiliki simu za aina tofauti... Bakhresa, alianzia na Shikirimu....na ali target lower class wakati anaanza...sasa hivi anatiririka karibu Afrika yote...ni mpiango tu...na pa kuanzia papo... Tumeona na tumeshuhudia!!
 
Naona cha maana zaidi movie za bongo ni kuongeza quality..., binafsi sipendi kuziangalia sababu story zake zipo shallow, dakika kumi za mwanzo unaweza kujua movie itakwendaje, ukiangalia moja ni kama umeangalia zote..., wenzetu unakuta producer mmoja ana movie kama tano tu au chini ya hapo maisha yake yote (sababu hataki kuwa associated na kazi mbovu), pia unakuta mtu kazi moja tu inamtoa.., tunameona movies kutoka nchi za kawaida zinahit worldwide mpaka kuwa nominated kwenye oscar (city of god, hii movie ya Brazil ambayo iliongelea uhalisia wa huko brazil)

Kwahio cha maana mkuu ukiwekeza hapa nakushauri weka msisitizo kwenye plot nzuri.., tuna vitabu na hadithi nzuri sana zinazoongelea issue za bongo, (kwanini msitumie hizi stories kama plot ?), tanzania ina history katika ukoloni, kwanini tusiwe na movie ya kuongelea story yetu from an african perspective..?, (tumeona movies kama Shaka Zulu, although this was from colonials perspective).

Tuna mengi ya kuongea na kuweza kuonyesha na yote hatuyaoni tunaona uhalisia ambao mwingi sio culture yetu, huu ubabe ubabe na violence ambazo hazitokei. Kwahio mkuu lets tell our stories and lets make it unique.., (tunajua wachina wana kung fu, wahindi wana arranged marriages, sisi tuna nini ?)
 
Back
Top Bottom