Natamani kuwa kama TV ya nyumbani kwetu

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,683
8,829
Uuuuwi nimeguswaaaa na huu ujumbe NATAKA KUWA KAMA TV YA NYUMBANI KWETU

Mwalimu mmoja wa somo la Kiswahili katika shule ya msingi aliwataka wanafunzi wake waandike Insha kumuomba Mungu chochote ambacho wanahitaji awapatie. Baada ya kumaliza mwalimu akakusanya Insha zoote walizoandika wanafunzi wake.Akazibeba na kwenda kuzisahihishia nyumbani kwake.
Alipoanza kuzisahihisha akakutana na Insha ya ajabu iliyoandikwa na mmoja kati ya wanafunzi wake. Insha ile ilimsisimua sana. Mume wake aliporudi kutoka kazini kamsogelea mkewe na kumuona akilia, Mume akamuuliza “nini kimekutokea?, nini kinakufanya ulie?”

Mwalimu akamuambia mumewe “soma hii ni moja kati ya Insha ya wanafunzi wangu”. Mume akaanza kuisoma, iliandikwa kama hivi ifuatavyo:

“ Ooooh Mungu! Nifanye kuwa Televisheni, ninataka kuishi kama Tv ya nyumbani kwetu.
Televisheni ya nyumbani kwetu inathamani kubwa sana. Familia yetu yote hukaa wameizunguka wanavutiwa sana nayo kwani wanavutiwa nayo sana. Tv inapozungumza wazazi wangu huisikiliza kwa furaha sana. Huwa hawapigi kelele kwenye Tv, huwa hawapigani na Tv, huwa hawaichapi Tv, hivyo nataka kuwa kama Tv.

Tv ndiyo kivutio kikubwa sana nyumbani kwetu. Nahitaji kupata uangalizi maalumu kama inyopewa Tv kutoka kwa wazazi wangu. Hata kama haifanyi kazi, Tv inathamani kubwa sana.

Baba na mama yangu wanaporudi nyumbani haraka sana hukaa mbele ya Tv, wanaiwasha na kutumia masaa mengi wakiitazama. Tv imeiba muda wa baba na mama yangu, hivyo nitakapokuwa Tv watatumia muda wao kuwa namimi.

Wanapoitazama Tv wazazi wangu hucheka sana na kutabasamu mara nyingi, hivyo nahitaji wazazi wangu kucheka na kutabasamu namimi pia. Hivyo naomba Mungu unifanye kuwa Tv.

Chamwisho kabla sijamaliza kama nikiwa Tv nitahakikisha nitawafanya wazazi wangu wawe na furaha sana. Mungu sitahitaji kingine zaidi. Ninahitaji tu, kuishi kama Tv ya nyumbani kwetu, hivyo naomba unigeuze kuwa Tv.

Baada ya kumaliza kusoma ile insha Mume akasema “Mungu wangu, masikini mtoto huyu, anajihisi mpweke, hapati uangalizi na upendo wa kutosha kutoka kwa wazazi wake, mbaya sana”
Macho ya mwalimu yakajawa na machozi zaidi, akamuangalia mumewe kisha akasema “MTOTO WETU NDIYO ALIYEANDIKA INSHA HIYO”.
Mungu atusaidie watoto wetu wasitake kuwa simu zenye whatsapp au Televisheni.

Share ujumbe huu kadiri uwezavyo kwa watu wengi ili waupate na wapate kukumbuka zaidi kuwa watoto ni zawadi, watoto ni furaha, watoto ni mafanikio, hivyo tuwapende na tuwe nao karibu sana ili kujua mambo mengi yanayo wahusu na wakue katika mazingira mazuri yenye tija kwa maisha yao ya baadae.
 
Mimi natamani niwe km tv yetu ili watoto wangu wanifurahie na kukaa wakiniangalia mimi tu. Naomba niwe km tv inayoonesha cartoon!!!!!
 
Nimeipenda hii story....
Nimechukua kitu....
Nitamfanya mwanangu awe TV yangu...
Nitamfanya mwanangu awe Smartphone yangu...
Asante kwa kushare...!
Asante kwa kula vizuri na wenzio....
 
Je uliweza kuwa kama tv weekend hii? TV hutulia tuli nyumbani
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom