NATAMANI kuwa kama LEMA...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Ingawa si rahisi sana, kiukweli natamani kuwa kama Godbless Lema. Ingawa yeye amezaliwa Arusha na mimi Pwani, haijalishi. Pamoja na kuvuliwa Ubunge wa Arusha Mjini haonyeshi kutetereka.

Anaendelea na mkakati wake wa ukombozi wa Taifa hili.Anaendelea kupigania utu na heshima ya watu wote.Mwenzangu Lema ana mizizi ya kibiblia na mimi yakisheria.

Alikuwa mmoja wa Waanzilishi wa Taasisi ya Kijamii iliyojulikana kama 'Msaada wa Haraka toka kwenye Biblia' pale Arusha.

Godbless Lema husema kile anachokiamini na kukisimamia. Mwenzangu Lema ni mtii kwa viongozi wake wakuu wa chama chake.Si mropokaji nje ya vikao. Amejaliwa sauti 'ya ushindi'. Nilibahatika kuisikia kipindi chote cha kampeni ya Ubunge 2010 pale Arusha nilipokuwapo. Amethubutu kumwambia ukweli hata Rais wa nchi.

Nina shaka na uwezo wangu. Nitaweza kweli? Lakini najipa moyo...
 
Hakuna lisilowezekana chini ya jua, jipe moyo na uthubutu pia kwani maneno ya kwenye PC tu utaishia kusomwa na kina TaiJike tu.
 
Yes, he is good! Ni mkweli na ana speech za kugusa mtima. Nilimsikiza wakati fulani, to be honest nilitoa machozi na mwili ulinisisimka....nikampenda sana.
 
Formula ya kuwa kama Lema si ngumu sana ni (Confidence,Courage, Critical thinking, Analysis, Ethics)=Lema.
 
Ni rahisi sana kuwa kama Mh.Sugu kuliko kuwa kama Lema. Kumbuka moja ya sifa zake ni kujipeleka mwenyewe Jela! je wewe unaweza?
 
Ila mkuu una uwezo wa kustahimili gerezani hata kwa siku1? Mkuu unaweza ukamchana live Rais? Unaweza kuwa mwanasiasa na mwanaharakati pasipo ndumba na ushirikina? Uan ujasiri? Una msimamo? Kama unaweza kutimiza kati ya hayo machache basi uje kwamba U CAN'

long live lema.
 
Kauli kama hii inatufariji sisi wana Mabadiliko wakati huu tunangojea matokeo ya rufaa ya kamanda wetu.
Ni wachovu wa kufikiri wachache tu ndio bado hawataki kutambua nguvu ya kamanda wetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom