Natamani kuivunjavunja line yangu ya Tigo

Haya orodhesheni namba zenu mnazotaka mi nitawapatia Code ya huku kwetu.
Karibuni sana na mjisikie mpo nyumbani.
 
Kama unatumia simu ya Samsung ina option ya kublock namba kwenye sms, mimi nimeblock No zote za promo kutoka Tigo naishi kwa raha mstarehe.
 
Nina samsung inablock cm lakini sms zinaendelea kuingia
 

Nikitaka nipate namna na mimi niwablock. Mkuu kama una njia ya kuwa-block naomba uweke hapa jamvini kwani wanakera kuliko kawaida. Naamini staff wote wa tigo ni mambumbumbu. Wanafikiri kututumia sms ndo watauza? kama nitashindwa kuzuia nami naitupa line ya tigo chooni.

Hata ukiblock sms bado utakuwa hujamaliza mkuu...
Siku hizi wanakera zaidi pale unapopiga simu, unakutana na sauti ya limwanamke... "Ukinunua tigo intanet, utapata mda....." Linaongea hilo limwanamke kwa zaidi ya dakika 1, then linasema ..."samahani, namba unayopiga, inatumika kwa sasa"..!
Kweli tigo wanasababisha natenda dhambi kila siku maana nikipiga, nikaanza kusikia hilo li-ujumbe lazima natukana
 
Hamia airtel!
Kiukweli mi nina line zote, tigo sanasana ni kwa ajili ya kupokea cm, sipigi. Airtel nao wana tatizo kuwa hakuna stations za Airtel money mtaani, so ukitaka kuweka mda wa maongezi lazima ukanunue na kukwangua mi-vocha, tofauti na tigo na voda, unajinunulia kutoka akaunti yako...
 
HAWA TIGO NI MASABURI. hAWASOMI HATA HIZI JUMBE WAKAONDOA USHENZI WAO HUU? KAMA SIAPTI JIBU BORA NIIPUMZISHE HII LAINI MAISHA.
 
Kwa kweli tigo wanasumbua!? Hivi kama kutuma sms ni gharama, kwa nini wasiache kutuma hizo sms zao ili watupunguzie gharama cc wateja ? Tigo mnakera tena si kidogo. Ninyi mnadhani mnatangaza biashara kumbe mnaudhi wateja!!??
 
Jamani awa tigo awafai kabisa kwani unaweza kua na shida upo sehem mbaya ukakopa mda wa maongezi basi utajuta utatumiwa meseji ongeza salio kwenye sm yako nawakati una ile ela ulio kopa mi nawauliza inamana ile ela ulio kopa sio salio au? wanatuibia sana awa.
 
Mie huwa nazima cm usiku. Napoifungua asbh fastafasta napata sms mbili, moja yanKUNIAMBIA NIMEUNGANISHWA NA TANO PACK wakati sijawahi kuomba kujiunga na huduma hiyo na wala sijui inahusu nini. meseji ya pili ni kuniambia nimepata muda wa bure kupiga Tigo-Tigo. Pia sijawahi kuomba huduma hii.
Kinachonikera zaidi ni yale matangazo yanayosikika ukipiga cm unasikilizishwa kwanza matangazo afu mwisho unaweza kuambiwa unayempigia hayupo hewani!
Huduma kwa mteja ni tatizo jingine,unaweza kuwapigia cm siku nzima!
Jamani,hivi tukamlalamikie nani kwa haya?
Je waheshimiwa,mawaziri na wabunge wanatumia mitandao gani? Pengine wao hawakutani na haya? Maana hatuwasikii wakiyasema.
 
Hakika TIGO wanakera sana. Ukiwa nje ya nchi na unataka kupiga simu ya jamaa yako Tanzania ambaye yuko TIGO, omba Mungu hiyo simu unayopiga iwe On. Ikitokea hiyo simu haiko hewani utajuta kupiga hiyo namba, kwani ndani ya sekunde umeshaingizwa kwenye voice mail bila ya wewe kujua na unakuta pesa inakatwa nyingi tu, ambayo unaweza ukatumia kuongea kama dkk 3 hivi. Mimi nilidhani mwanzoni kwamba ni simu ya huyo ninayempigia ndiyo ameseti kwenye voice mail, lkn wapi? Kwani laini yoyote ya TIGO ukipiga na simu haiko on, wao wanakata pesa kwa kisingizio kwamba ubonyeze sijui nini ili ujumbe umfikie muhusika atakapokuwa on. Hakika TIGO wanakera sana. Sasa sijaelewa logic ya wao kukata pesa zetu kama simu ya unayempigia haiko on, na isitoshe line unayotumia na voucher siyo za kampuni yao ya TIGO. Sasa sijui ni kwanini wao wanatugombanisha na ndugu na kila ukitaka kupiga simu TZ na huyo muhusika yuko TIGO, unaanza kuwaza kama yuko hewani au la? au unamtumia sms kwanza kama yuko hewani akubipu ndipo umpigie. Tatizo linakuja kama huyo naye hana salio la kuweza kukubipu.

Hakika TIGO WANAKERA SANA kwa huduma zao. Ni tofauti kabisa na VODA NA AIRTEL, ukipiga na muhusika hayuko hewani inakupa jibu kwamba hayuko hewani na pesa haikatwi. Kwa trend ya miziki ya TIGO isiyokuwa na maombi toka kwa wateja, naamini hii hali inawapunguzia kwa kiasi kikubwa sana repuation katika jamii.
 
bAHATI MBAYA SANA HATA UKIPIGA CUSTOMER CARE NDO KABISA UTAMALIZA BETRI YA SIMU. hAWAPOKEI MANYANG'AU HAWA. UTASHANGAA UNAPIGA CUSTOMER CARE HALAFU WANAANZA KUKULETEA MATANGAZO YAO YASIYO MSINGI. KWANI HUKU JAMVINI HAWAINGII WAKASOMA HIZI KERO. NAANZA KUWAFANANISHA NA MAGAMBA.
 
Back
Top Bottom