Natamani kuivunjavunja line yangu ya Tigo

meeku

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
569
108
Kama kuna vitu vinanikera ni ma-sms yanayoyumwa na kampuni bila utaratibu. Kwanza kwa siku unatumiwa sms zaidi ya 20 halafu zote ni utumbo mtupu. Ukinunua muda kwa tigopesa lazima zije sms kama 5 au 6. Zote zimebeba ujumbe wa kipumbavu. Kwani hawa Tigo wanafikiri hatuna muda wa kufanya kazi au tutakuwa tunasoma ma-sms yao ya kipuuzi. Kama hawatabadilika ni bora nikae pembeni. huu ni upuuzi.
 
Mimi jana niliitafuna line yangu ya tigo mbele ya meneja wa tigo pale mlimani city hawana maana kabisa TIGO
 
Mimi jana niliitafuna line yangu ya tigo mbele ya meneja wa tigo pale mlimani city hawana maana kabisa TIGO

Binafsi wao wanadhani kuwa ni jambo la maana kwa vile linafanywa na komputer lakini wanapaswa kujuwa kuwa ni kero. Nimekuwa mteja wa tigo miaka mingi lakini sasa naona inafika mwisho. sms nyingine za kipuuzi hswa " ndugu mteja endelea kupata huduma" au ukicharge vocha watakutumia sms 5 za umefanikiwa na upuuzi mwingine usiokuwa na tija.
 
Afadhali nyie!mi kila siku wanakwiba hela zangu kwenye simu!yani kama sio kuwa watu wengi ninaowasiliana nao wanatumia line ya tigo ningeshahama!lol
 
Na tena siku hizi wanatumia namba kawaida za simu zao wanapiga ukipokea unakuta wanatoa tangazo,wewe unajua ni mtu anakupigia du! Wanakutumia tigo promo saa tisa usiku dunimeacha tigo muda yaani wanakera mi nilishindwa vumilia kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
mi wananikera na matangazo yao ya kulazimisha, nampigia mtu simu wananipa tangazo kwanza afu eti ndo simu inaita, inakera.
 
Unakuta mwenyewe upo bize na mambo yako, mara simu zinaingia message, unatoa kusoma chapu chapu labda ni za muhimu sana,, aaagh! kumbe TIGO PROMO, Kero sana, wananimalizia chaji yangu kushinda na delete mimeseji isiyo na maana kila siku
 
Kwa kweli tigo ni tatizo kubwa sijui kama inaongozw na watu wenye akili au maji,kwani unampigia
mtu simu wanaweka tangazo lao inaweza kukufanya kujua simu haiko hewani kumbe ni upuuzi wa
hawa jamaa na matangazo yao ya kipuuzi.
 
Kama kuna vitu vinanikera
ni ma-sms yanayoyumwa na kampuni bila utaratibu. Kwanza kwa siku
unatumiwa sms zaidi ya 20 halafu zote ni utumbo mtupu. Ukinunua muda kwa
tigopesa lazima zije sms kama 5 au 6. Zote zimebeba ujumbe wa
kipumbavu. Kwani hawa Tigo wanafikiri hatuna muda wa kufanya kazi au
tutakuwa tunasoma ma-sms yao ya kipuuzi. Kama hawatabadilika ni bora
nikae pembeni. huu ni upuuzi.

Halafu huku mikoani internet yake k.e.n.g.e tu! mi najitoa!
 
Tigo wezi sana, usiombe ujiunge na huduma yao ya XTREME utajuta, watakukata ile shilingi 450, kama kawaida halafu sasa pasipo wewe kujuandani ya hayo masaa 24 XTREME kabla hata haijamalizika utaona kabalance kanapungua taratibu. Mwisho wa siku unakuta umechomolewa hata shilingi 200.
 
Tigo wezi sana, usiombe ujiunge na huduma yao ya XTREME utajuta, watakukata ile shilingi 450, kama kawaida halafu sasa pasipo wewe kujuandani ya hayo masaa 24 XTREME kabla hata haijamalizika utaona kabalance kanapungua taratibu. Mwisho wa siku unakuta umechomolewa hata shilingi 200.

umenikumbusha kuhusu haya ma-ringtone. hujaomba kuwekewa unashangaa wanakuletea sms kuwa umekatwa pesa kwa ajili ya ringtone. Hawa staff wa tigo, nadhani ndo maana hata vijana wa mjini wanasema tigo ni -nnya. hovyo kupita kiasi.
 
Mi tangu kitambo niliwaweza na matangazo yao. Nili add kwenye screen list kwa hii simu yangu. So, huwa sipati huu usumbufu. Poleni sana wana JF.
 
Mi walikuwa na katabia ka kunitumia vijihabari mshenzi fulani hivi na wakati sijawahi kujiunga na huduma hiyo.Ukiweka ka voucher ka 2000 tu,wanakazana kutuma vijihabari vyao na kila sms 1 ni sh.300,ukizubaa tu wanakomba pesa yote.Halafu salio likiisha unaanza kupata makumi ya sms zikiku-alert kwamba uongeze pesa kwani salio lako liko chini ya sh.100.
 
kama kuna mbwa tena koko TIGO ni mbwa koko. Ninawachukia kiasi kwamba sitaki hata kuwasikia. Simcard yao niliitupa chooni kwa hasira. Majizi wakubwa hao. Matangazo ya kipumbavu na kuiba pesa kwenye simu kwa kitu ambacho hujajiunga nacho. Sijui TCRA wako wapi.
 
Mi tangu kitambo niliwaweza na matangazo yao. Nili add kwenye screen list kwa hii simu yangu. So, huwa sipati huu usumbufu. Poleni sana wana JF.

Nikitaka nipate namna na mimi niwablock. Mkuu kama una njia ya kuwa-block naomba uweke hapa jamvini kwani wanakera kuliko kawaida. Naamini staff wote wa tigo ni mambumbumbu. Wanafikiri kututumia sms ndo watauza? kama nitashindwa kuzuia nami naitupa line ya tigo chooni.
 
Tigo ni mafila.uni kabisa... nina shaka wanawatumia watu wa TCRA maana nimelalamika sana kwa TCRA lkn hakuna any action.

Wanaingiza customers kwenye service pasi kujiunga, na ukilalamika hakuna refund yoyote. Wananeemeka kwa rushwa to TCRA na ukimya wa Watanzania. Lkn ipo siku watafunga hiyo kampuni yao... wapumba.vu wakubwa.
 
Mengi mliyosema wadau mko sahihi..nilishawahi kujiunga na vifurushi vyao vya internet kama mara tatu, lakini niliambulia kuliwa pesa yangu bila kuunganishwa,nikaenda katika moja ya ofisi zao wakaniambia pesa haiwezi kurudi,kuokoa nguvu na muda nikaona nijiweke pembeni kuepusha msongamano..now nilikohamia angalau..
 
Back
Top Bottom