Natamani kuifunga jela mifupa yake

Taahira ni nani zaidi ya wewe? nisome nini wakti umeshindwa kujibu swali nilokuuliza?
Inawezekana ni kweli nimekuzidi utaahira...! Unaonaje kweli eehh!

Unaniuliza mimi eti usome nini! Biiiiig smile.
 
Kwi kwi kwi..naona unakazaaana kwelikweli kuyeyusha..nshakusoma bana kuwa swali HALIJIBIKI. Sina nyongeza.
 
Pole sana...!

Kama jibu ukuliona sina jinsi ya kukusaidia.

Nioneshe hilo jibu ambalo sijaliona..lol..otherwise it is time to allocate muda wangu kwa shughli zengine za maendeleo badala ya ku-converse with a spineless deluded muhamedan who happen to be useless & stupid too.
 
Inaonekana wewe na huyo mwarabu wako mnaelewana na mnashirikia vema.

Hilo lisikusumbue sana. Mwarabu ni wako bro, na bado anadai kuwa wewe ndiyo unafaa kuwa Mkata Michongoma wake, Mpishi, Msafisha Vyoo, Mtunzaji watoto na Maalim wake mtarajiwa kama ilivyopitishwa kwenye Quran. Anavyodai Mmanga, Tanzania nzima hakuna mtu mwenye mfano kama wewe.
 
Nyerere katika hotuba zake nyingi alizingizia "uchanga" wa Taifa la Tanzania wakati Waingereza wanaturuhusu kupandisha Bendera...

Mara nyingi utamsikia Nyerere akilalama "..tulikuwa na wasomi wachache..." ...e.t.c

But you wonder, Kwa nini alichukua trouble kupigania "Uhuru"?
 
yah, shule kushoto..then i would n't have 4 degrees on my belt..i guess..mtajibeba.

angalia sasa .. eti una degree nne .. tehetehtehe hapo kwenye red labda za mipasho.. nyie si ndio walewale kina mzee yusuph

BTW< "njiwa" kikwetu sisi inatranslate kama mtu anayepumuliwa kisogoni..

kama maana njiwa huko kwenu ni hiyo... sitokulaumu tena na uwezo wako wa kufikiri...
 
Kweli this is a home of great thinkers... Watu wanafikiria kuifunga jela mifupa??.. Na wengine wanasapoti... Bado kidogo watafikilia kui*********!
 
Natamani Kuifunga Jela Mifupa yake.

Salaam ndugu zanguni wapendwa ndani ya jukwaa hili la JF, ni matumaini mpo na siha njema kabisa. Leo nami najikita kwenye jukwaa la ili. kwa machache ambayo yalikuwa yanapita kama taswira ya picha ya kutisha mbele ya macho yangu, kiasi yakwamba naogopa hata kulala, maana hilo jinamizi ninalo liona kila nikifumba macho linatisha kweli kweli.

Wengi watashtuka na kichwa cha makala haya, Natamani Kuifunga Jela Mifupa yake. Naam ni kweli kabisa ndugu zanguni, natamani kweli na si uongo, kwani leo nimekaa na kutafakari mengi sana, haswa enzi zile za Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa... Nakumbuka sana enzi zile ambazo ndio kwanza tumepata uhuru, enzi za matumaini mapya, enzi za kufurahia uhuru tulio upata toka kwa Mwingereza, aliyepewa dhamana ya kutuangalia mpaka pale tutapopata uwezo wa kujitawala, enzi za kujivunia utaifa wetu.

Ni dhahiri kuwa usiku ule wa Desemba 9, 1961 wakati ilipokuwa inashushwa bendera ya Mwingereza na kupandishwa ile ya Tanganyika, wengi walitokwa na machozi ya furaha kila aliyeshuhudia alikuwa na yakini kuwa ule ulikuwa ndio mwanzo wa maendeleo ya nchi yetu Tanganyika.

Maendeleo ambayo yangekuja kuonekana katika hali bora zaidi za kiuchumi kwa taifa na mtu mmoja mmoja, nyumba bora zaidi, kilimo cha kisasa zaidi, usafiri bora zaidi na juu ya hayo elimu bora zaidi na kwa wote.

Kwa kweli matumaini yetu yalikuwa makubwa sana, kiasi ya kwamba wengi walikuwa wakitokwa na machozi ya furaha na matumaini. Matumaini ambayo leo hii yamekuwa ni ndoto za Ali Nacha. Wengi watashangaa hivi leo X-Paster anataka kusema nini, mbona hatumuelewi? Ni kweli kabisa unaweza usinielewe, kwa sasa ila kama utatafakari na kuchambua maisha ya Mtanzania tangia kupata uhuru mpaka leo hii, basi utashindwa kutambua, wapi tulipotoka na wapi tunaelekea na wapi tumesimama.

Lahiti tungalijuwa kuwa Uhuru ule ungetuletea mashaka haya nina ukakika kabisa mashujaa wetu wasingetumia mali zao na muda wao kuondoa ubaguzi wa kikoloni na hata ingekuwa tumepewa uhuru bila ya harakati basi hakuna ambaye angesheherekea kama ilivyokuwa siku ile ya uhuru.

Nakumbuka sana, baada ya uhuru mwaka 1961 viongozi wa nchi yetu tukufu walifanya mengi kwa nia ya kuendeleza nchi hii. Hapa kuna machache niliyoweza kuyakumbuka baadhi ya hayo ni kama ifuatavyo:

1961 - Uhuru wa Tanganyika

1962
- Jamhuri ya Tanganyika

1964
- Muungano Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa nchi mpya iliyokuja kujulikana kwa jina la Tanzania

1967 - Azimio la Arusha

1971 - Madaraka mikoani

1980s - Vita dhidi ya wahujumu Uchumi

Bila kusahau U.P.E, vijiji vya ujamaa, maduka ya kaya, elimu bure, kutaifisha majumba, mashamba n.k.

Kwa wakati ule nyimbo nyingi zilitungwa kupongeza kila hatua iliyochukuliwa. Kwa bahati nzuri miaka yote ya sitini na sabini iliwashuhudia Watanzania chini ya utamaduni wa kuheshimu na kuthamini sana viongozi wao, hivyo moyo wa uzalendo ulijitokeza wazi wazi.

Hali hii ilijitokeza hasa pale wananchi walivyozitii hata amri ambazo bila shaka hata serikali iliona tabu kuzitekeleza, mfano kuanzishwa vijiji vya ujamaa, kutaifisha majumba, mashule na mashamba ya katani, pamba n.k.

Tuliambiwa na tukaamini kuwa Tanzania haiwezi kuwa huru hadi Afrika yote iwe huru. Serikali yetu tukufu ikiongozwa na fikra sahihi za mwenyekiti ilitumia kila uwezo uliokuwa nao kufikia lengo hili. FRELIMO, MPLA, ANC, SWAPO walifaidi sana msimamo wetu huu.

Tuliambiwa Idd Amin ni nduli anayetumiwa na mabwana zake ili kuzorotesha harakati za ukombozi wa Afrika. Tulikubali hili watu walitoa mali na roho zao kuikomboa ardhi yetu na kumpa adhabu kidogo ndani ya mipaka ya nchi yake.

Haya yalifanyika bila mtu yeyote kuhoji kwa vile wengi walidhani kufanya vile ni katika harakati zile zile za kutuletea maendeleo.

Wazalendo wale ambao enzi zile walijulikana kama Makabwela, yaani watu wa kipato cha chini, leo hii tunajulikana kwa jina la Walala Hoi, na haswa wanaoishi mikoani wanaweza zaidi kuona kile ninacho kizungumza... Si ajabu uko mikoani na haswa ukitembea siku ya soko au gulio ukamwona dalali akiuza kitanda cha kamba... karne hii.

Mimi bado najiuliza sababu ya huu umasikini ni nini haswa. Tulikuwa tunaambia kuwa ili nchi iendelee tunaitaji mambo manne, Ardhi, watu, siyasa safi na uongozi bora Je hivi vyote kweli hatuna hata kimoja!?

Nasema tena kwa sauti kubwa kabisa , serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere haikuwa nzuri kwenye mipango ya uchumi, ni bora tungeendelea kutawaliwa na Mwingereza, kuliko serikali hii iliyo hasisiwa na Mwalimu Nyerere. Nadiriki kusema kuwa Wakoloni walikuwa bora kuliko Nyerere kwa mipango ya uchumi mizuri kwa ajili ya nchi hii. Hao wakoloni tulio waondoa ndio hao hao waliotuletea mazao mbali mbali ya kiuchumi, kama vile Pamba, Katani , Chai, Kahawa, Korosho na kadhaa wa kadhaa, na haya mazao yaliletwa ili kutegemeza uchumi wa nchi hii, na ni kweli waliona mbali, kwani mazao hayo mpaka leo hii ndio yanasaidia nchi yetu, lakini cha ajabu serikali iliua mashamba yote makubwa na hata hao wakulima wadogo wadogo wa mazao hayo, serikali haikuwajali.

Kipindi cha utawala wa Nyerere kwa kweli ni kipindi ambacho serikali yake ishindwa kuendesha uchumi wa nchi. Hata pale alipo amua kuanzisha Azimio la Arusha kama njia ya kujikwamua kiuchumi, bado hatukuona nafuu yoyote ile kwa mlalahoi, au makabwela. Na Kwa bahati nzuri mtoto yule aliyejulikana kwa jina la Azimio la Arusha alimfia mikononi kabla hata mzazi wake hajafariki. Hata ile siyasa ya Ujamaa na kujitegemea aliyopanga na wachumi wake uchwara, nayo ikapata ugonjwa wa kifaduro. Nayo akaishuhudia ikimfia mikononi.

Sera za ujamaa na kujitegemea kwa kweli hazikuwa sera nzuri hata kidogo. Na hata alipo ambiwa kuwa sera ni mbovu, badala ya kufuata ushauri wa kitaalam, yeye akatumia sura na maumbile yake akichanganya na uongozi wake na umahiri wa kuzungumza na kuvutia kuzitetea sera zake mbovu mpaka nchi ya Tanzania ikaangamia. Kusema kweli Mwalimu Nyerere alikuwa ni mahiri sana kwenye kutoa hotuba za kuvutia na zenye kuleta matumaini mazuri, maneno yake kwa kweli yalijaa ushawishi wa hali ya juu sana. Lakini ukija kwenye matendo ya zile hotuba nzuri hakuna hata kijiji kimoja cha maonyesho kuonyesha kuwa alifanikiwa kwenye sera zake. Hivi leo hakuna kijiji hata kimoja ambacho kinafahidika na sera zile za ujamaa na kujitegemea.

Nakumbuka aliyekuwa rais wa Kenya enzi hizo (Jomo Kenyatta) aliwahi kumwambia wanahabari kuwa "kama unataka watendaji wazuri katika sekta ya mbalimbali njoo Kenya na kama unataka wahutubiaji wazuri kila eneo liwe la siyasa, uchumi, biashara, kilimo n.k basi kwenda Tanzania kamwambie Nyerere akupe anao tele

Ni kweli kwani ile siyasa ya ujamaa iliwaharibu sana viongozi wa taifa ili. Nyerere alitengeneza wahutubiaji wazuri si watendaji na wachapa kazi wazuri kwani karibia wote walipitia vyuo vya siyasa. Alipenda sana watu ambao kazi yao ni kuimba kwa nguvu hadi kufoka mate mdomoni kwa kusema "Zidumu fikra za mwenyekiti..." . Na wala sishangai maana hata leo na hata hao walio upande wa pili wenyewe wanajiita vyama vya upinzani wengi wanaiga tabia ya Nyerere ya kuwa wahutubiaji wazuri kuliko kuwa watendaji na wachapa kazi.

Na kwa kawaida sehemu yoyote ile maendeleo hayawezi kuja hivi hivi, lazima yafanyiwe kazi ili yapatikane. Kazi hiyo haitegemewi kufanywa na mwingine yoyote isipokuwa watawala na watawaliwa (serikali na raia).

Watawala ndio wenye jukumu la kupanga na kuratibu mipango na kutafuta njia za kusaidia utekelezaji wake ili watawaliwa waweze kufanya hayo ambayo yameshapangwa. lakini watawala wetu wale walikuwa kama wafalme, kazi yao ilikuwa kunyoosha vidole tu, bila kuonyesha mifano hai.

Mpaka leo hakuna ambaye anaweza kutuambia, ni ugonjwa gani uliotupata Watanzania, baada ya kutaifisha mashirika na mashamba. Tulikuwa na mashirika mengi tulio yaita ya Umma kama vile Viwanda vya nguo vya Urafiki, Sunguratex, Mwatex na kule Musoma pia kulikuwa na kiwanda cha nguo, ila sina uhakika kama bado kipo, tulikuwa na kiwanda cha kusindika nyama, Tanganyika Packers, kiwanda cha viatu kule Morogoro, na kile cha dar, pia kulikuwa na RTC na Ugawaji na mengine mengi. Yote haya leo ni marehemu na makaburi yake yashafutika kwenye ulimwengu wa Mtanzania.

Serikali yetu baada ya kutaifisha mashirika na makampuni na kukuta pesa nyingi kwenye hayo mashirika, wakaona bora kuanzisha vikundi vya sanaa vya mashirika ya umma. Vikundi ambavyo vilikuwa si vya uzalishaji mali, bali vilikuwa vinapata ruzuku kwa asilimia mia 100% kutoka kwenye hayo mashirika. Vikundi vingi kufikia mwishoni mwa miaka ya themanini 1980 vingi vilianza kudolola. Mashirika mengi yalianza kupungukiwa na uwezo wa kuviendesha vikundi hivyo kwa sababu nayo yalikuwa taabani kifedha.

Huwa najiuliza wakati mwingine, ni vipi bidhaa kama Pamba, Katani au bidhaa kutoka kwenye mashamba au makampuni ulio dhurumu, yaani umuuzie yule yule uliye mnyanganya, hivi inaingia akilini kweli!?

Fikra zangu zika ambaa ambaa,mpaka zile enzi ambazo JKT walishirikiana sana na askari polisi kulinda viongozi na kukamata raiya, kisa wamemkuta na dawa ya meno au kipande cha sabuni ya mchubuo (tulikuwa tunaita sabuni ya pundamilia). Ukikamatwa na dozen moja ya sabuni ni muhujumu uchumi, hakuna ruhusa ya kuweka wakili wa kukutetea...!

Nakumbuka ili kuangalia TV, mpaka kipindi cha sikukuu ya sabasaba kwenye banda la Yahaya Hussein, hii ni kwa wakazi wa jiji la DSM, Sijui uko mikoani hali ilikuwaje. Nakumbuka sana zile nyimbo za kina marehemu Mzee mzima Pepekale, Rechereau (tamka Rosherou) au Tabu Ley, Franco Luambo Makiadi Mzee wa o.k Jazz na wengine wengi.

Zaidi ya hapo kila kitu kilikuwa kwa foleni, nchi nzima shule za sekondari za kuhesabika kwa vidole vya mkono. Chuo kikuu kimoja tu, kama kimejaa basi, subiri mwakani au ndio basi tena. Ilifikia wakati hata ukiwa na gari zuri basi wewe ni bepari kila kitu kwa kibali, ukiona gari aina ya Benz basi hiyo ni mali ya Ikulu, watu binafsi si rahisi kumiliki gari kama hiyo yaani hata kuvaa suti ni ubepari. Nakumbuka mwaka mmoja aliyewahi kuwa naibu waziri mkuu salim Ahmed Salim, alikuwa Mtwara anahutubia wengi wa wale walio hudhuria walikuwa wamevaa majunia ya mbolea kama nguo.

Baada ya kutawala zaidi ya miaka ishirini na kushuhudia kila kitu kikishindwa na maji yapo shingoni, yanakaribia kuingia mdomoni, kiujanja ujanja na kiutu uzima akaamua kutoroka uongozi, ndio akamtupia Mwinyi maiti akitegemea miujiza ya kufufuliwa, alisha sahau kuwa enzi za wafu kufufuliwa zilisha pita... Akasingizia kuwa anangatuka mapema. Kumbe alikuwa ameshindwa kuendesha uchumi wa taifa ili.

Ndio maana leo hii kila nikikumbuka madhira ya utawala wake inanifanya nitamani kwamba mifupa yake ipelekwe gerezani. Kwani ni yeye aliyeasisi siyasa na sera mbovu dhidi ya taifa ili la Tanzania, na mpaka leo hatujainuka tena.
Pole sana X-Paster!
Japo wapo humu wameelimika kaw hilo...na wengine watakuchukia kwa hilo.
Zidi kutuwekea mambo ya zama hizo Baba!.
 
angalia sasa .. eti una degree nne .. tehetehtehe hapo kwenye red labda za mipasho.. nyie si ndio walewale kina mzee yusuph

kama maana njiwa huko kwenu ni hiyo... sitokulaumu tena na uwezo wako wa kufikiri...

Ya nne..1,2,3,4 nadhani unajua nne inaandikwaje..kwi kwi..nne tena za kueleweka tu sio za madrasa. Shukran za pekee kwa mama yangu aliyehakikisha sikanyagi madrasa maana ningeishia kua zuzu kama wewe.
 
Congratulation X-Paster 4 representing your thoughtful.
Ndivyo inatakiwa upunguze msongo wako.
Humu tupo tunaopata faida ya hayo...pia wapo ambao wanaumizwa na mawazo yako.
Wherefore ...i say to u ...go on Baba!
Ubarikiwe sana.
 
Ya nne..1,2,3,4 nadhani unajua nne inaandikwaje..kwi kwi..nne tena za kueleweka tu sio za madrasa. Shukran za pekee kwa mama yangu aliyehakikisha sikanyagi madrasa maana ningeishia kua zuzu kama wewe.

Abdulhalim mwenye degree nne utakuwa wewe bana acha kujitusi.... msomi utamjuwa kutokana na kile anachokiandika "Life is a b!tch and death is her sister says the dude with 4 Bachelor's degrees" "maana ya njiwa ni kupumuliwa kisogoni again says the dude with four degrees " labda kama ulizisomea china alafu za miezi 4
 
lol..naona ilmu nlokutajia imekuchoma sana, jitahidi na wewe unaeza ukazifikia hizo maarifat...zinapatikana baada ya bidii kidogo hazitolewi na kama pipi, na hazipatikani kwene mihadhara na majungu kama haya..kaka, ni hayo tu ..peace n' out.
 
Abdulhalim mwenye degree nne utakuwa wewe bana acha kujitusi.... msomi utamjuwa kutokana na kile anachokiandika "Life is a b!tch and death is her sister says the dude with 4 Bachelor's degrees" "maana ya njiwa ni kupumuliwa kisogoni again says the dude with four degrees " labda kama ulizisomea china alafu za miezi 4
Kaka wala usipoteze muda kijibishana naye, jamaa ni mtu wa mipasho jazz band...! Hana hoja, zaidi atakutusi tu.
 
X-Paster!
Endelea kutumwagia maelezo humu....tupo tunaokuelewa...pia wapo wasiokuelewa!
Naamin hilo walijua!
 
Back
Top Bottom