sisame
JF-Expert Member
- Nov 1, 2016
- 365
- 320
Jamani mwenzenu tangu nimegraduate 2011, B.A Community Development, tena nina GPA nzuri tu, na ni mtu wa kujituma, lakini sijawahi pata ajira mahali popote, NGOs ni nyingi lakini sijawahi hata kuitwa kwa interview katika NGOs zote nilizoomba.
Japo naendelea kupambana na maisha ktk nyanja za kilimo na ufugaji lakini duuuh nikiwaona wenzangu wapo makazini (tena wengine nilikua nikiwabeba kwenye group assignments) napata shida nafsini mwangu to the extent that natamani kuchana vyeti vyangu vyoote nikae kama vile sikuwahi kwenda shule kabiiisaaaa.
Kuna wakati nilitembea maofisini katika ofisi ambazo nafahamu fika wanafanya shughuli zinazohusiana na maendeleo ya jamii nikiomba kujitolea buuureeee kabisa, nauli yangu, lunch yangu, wao wanipe kazi tu niwe nazifanya, tena nitazifanya kwa moyo, lakini sikupata hata pahala pamoja!
Nina mapenzi makubwa sana na profession yangu lakini sasa navunjika moyo, najiuliza nini kinasababisha nisikubaliwe hata pale ninapokua tayari kufanya kazi bure (Volunteering), nimefunga na kuomba kwa kila hali, sasa nimebaki kuhangaika na nafsi tu, nawaza kuchana vyeti vyangu vyote, na mabaki niyachome moto, iwe habari yangu ya shule imeishia hapo!