Natamani Angekuwa ni Binti Yangu

[/B]

Mtoto ana A mpaka Bible Knowledge duh! Mambo ya bible tangu utotoni hayo.

Matokeo ya Immaculate. St. Marian Girls.

S0248/0032​
F​
IMACULATE R MOSHA
7​
I​
CIV-A HIST-A GEO-B B/KNOWL-A KISW-B ENGL-A PHY-A CHEM-A BIO-A B/MATH-A​

Haya tena, damu ya kichaga-mambo ya bidii kwa sana, Baba profesa mambo ya Sayansi(kuna somo la sayansi hana A?), mama CPA-Mhasibu huyo(Maths A) hapa ukitazama hapo juu kwenye matokeo inabidi yakubali yenyewe.

Chekechea St Ann, Sekondari St Marian. Jamani 1 jumlisha na 1 ngapi?

Mtoto anaongea nyumbani Kichaga na Kingeresa(English) na ndio hivyo tena akapata B ya kiswahili na A ya Kiingereza.

Milima ya morogoro imemchanganya ndio maana direction zinasumbua akapata B ya Geography.

Kumbe basi Mafanikio yanatokana na Mazingira na unavyoyatumia.

Mazingira(Including watu)+utumiaji mzuri wa Mazingira =Mafanikio
Mazingira yanasababisha sana tu tena sana kwa watoto kufaulu au kutofaulu katika masomo yao,angalia shule za serikali ni masikitiko unakuta mtoto ni mzuri tu kichwani ila mazingira mabaya yanamuaffect,sasa watoto ambao wanaitegemea serikali watafeli kila siku.
 
Mtoto ana A mpaka Bible Knowledge duh! Mambo ya bible tangu utotoni hayo.

Matokeo ya Immaculate. St. Marian Girls.

IMACULATE R MOSHA- S0248/0032-Female

DIVISION 1 POINTS 7

CIV-A HIST-A GEO-B B/KNOWL-A KISW-B ENGL-A PHY-A CHEM-A BIO-A B/MATH-A

Haya tena, damu ya kichaga-mambo ya bidii kwa sana, Baba profesa mambo ya Sayansi(kuna somo la sayansi hana A?), mama CPA-Mhasibu huyo(Maths A) hapa ukitazama hapo juu kwenye matokeo inabidi yakubali yenyewe.

Chekechea St Ann, Sekondari St Marian. Jamani 1 jumlisha na 1 ngapi?

Mtoto anaongea nyumbani Kichaga na Kingeresa(English) na ndio hivyo tena akapata B ya kiswahili na A ya Kiingereza.

Milima ya morogoro imemchanganya ndio maana direction zinasumbua akapata B ya Geography.

Kumbe basi Mafanikio yanatokana na Mazingira na unavyoyatumia.

Mazingira(Including watu)+utumiaji mzuri wa Mazingira =Mafanikio

Ndio unataka kusema kuwa waliosoma ST KAYUMBA na wakafeli ni mazingira magumu yamewasababishia?
 
Hongera binti!
Thats just the begining dear!..

Mh. PJ hilo laweza kuwa tishio kwa binti. Pengine ni bora ainuliwe moyo tu kwa kujua kuwa yuko on the right track bila kupewa hint ya urefu wa safari na mauzauza yake. ;)
 
Lakin kumbuka,Samaki mmoja akioza...................
Tunalaumiwa wanawake wote.
Hizi methali zingine hazina ukweli wowote,samaki mmoja akioza kaoza yeye peke yake kuna wengine wanadunda tu.
 
Hongera sana binti Imaculate Mosha maana umeyafunga tela mpaka mababa ya Mzumbe, Kibaha, Illboru n.k hongera sana natambua sana ufaulu wako umetokana na juhudi na maarifa.

now you are talking!!!!!!!!!!! nadhani umetumia b/fast ya masa

Mzee umeanza kuweka points, nimekugongea Thanks........nadhani unamchupa hapo wa Serengeti

anastahili hiyo thanks sasa
 
Ndio unataka kusema kuwa waliosoma ST KAYUMBA na wakafeli ni mazingira magumu yamewasababishia?
Inawezekana mazingira ni fresh ila kichwani hamnazo,Marian Girls kuingia hapo lazima interview na lazima ufaulu vizuri interview.Ulishaenda St marian siku ya interview utashangaa ni MAGARI YAMEPAKI yasiyo na hesabu ila wanafunzi wanaochukuliwa ni wale wazuri kichwani sasa jumlisha na mazingira mazuri mwisho wa siku Darasa zima ni one na two za kuhesabu.
 
Mazingira yanasababisha sana tu tena sana kwa watoto kufaulu au kutofaulu katika masomo yao,angalia shule za serikali ni masikitiko unakuta mtoto ni mzuri tu kichwani ila mazingira mabaya yanamuaffect,sasa watoto ambao wanaitegemea serikali watafeli kila siku.
Basi ni balaa.Kwa sababu nchi ishakuwa ya kibepari.Wenye nacho(UNTOUCHABLES) na wasio nacho.
Hebu tujikumbushe kidogo wimbo wa Banza.
Mtaji wa Masikini ni nguvu zake mwenyeeeeeeeeeewe X2
Hao wenye pesa hawakuzaliwa nazoooooooo
Jitumeeeeeee,fanya kazi,kwani kaziiiiiiiii ni msingiiii.........
 
Mkuu mimi huwa nawashangaa wanawake huwa wanabezana wao kwa wao na hii inawafanya wasiwe na umoja laiti kama wakisimama kidete wanaweza sana.

Ni kweli kabisa, na huwa nasikitika sana kuona mwanamke anayejitahidi akibezwa.
Frankly speaking, huwa nafurahia sana mwanamke fulani akiwa juu, na huwa natamani azidi kuendelea. Nakumbuka nilikuwa na wakati mgumu sana wakati Obama na Clinton wakigombea, ukweli nilitaka Clinton ashinde just because she is a woman.
kinachonishinda kwa wanawake tu ni Umbea na Majungu, hapo ndo huwa nakata tamaa sana. maana kila mkikaa wadada watupu ni kama mpo kwenye kipindi cha LEO TENA, ha ha haaaaaaa
 
Basi ni balaa.Kwa sababu nchi ishakuwa ya kibepari.Wenye nacho(UNTOUCHABLES) na wasio nacho.
Hebu tujikumbushe kidogo wimbo wa Banza.
Mtaji wa Masikini ni nguvu zake mwenyeeeeeeeeeewe X2
Hao wenye pesa hawakuzaliwa nazoooooooo
Jitumeeeeeee,fanya kazi,kwani kaziiiiiiiii ni msingiiii.
........
Hapa tunaongelea mwanafunzi mzuri tu kichwani yupo shule ambayo walimu ni form six failure,then wakati mwingine hakuna kabisa waalimu hana pesa za kwenda mjini kusoma tuition.Na mwisho wa siku mtihani ni wa taifa hawajali mwanafunzi fulani hakuwa na waalimu,Chakula nacho cha shida maharage yameoza,Mwanafunzi yupo motivated ila mazingira yanamblock.Sijui wizara ya elimu inafanya nini?
 
Ni kweli kabisa, na huwa nasikitika sana kuona mwanamke anayejitahidi akibezwa.
Frankly speaking, huwa nafurahia sana mwanamke fulani akiwa juu, na huwa natamani azidi kuendelea. Nakumbuka nilikuwa na wakati mgumu sana wakati Obama na Clinton wakigombea, ukweli nilitaka Clinton ashinde just because she is a woman.
kinachonishinda kwa wanawake tu ni Umbea na Majungu, hapo ndo huwa nakata tamaa sana. maana kila mkikaa wadada watupu ni kama mpo kwenye kipindi cha LEO TENA, ha ha haaaaaaa

Wanaume nao washaanza kushika hii kasi ya umbea.Kuna wanaume ni wambeya balaa.mfano zile nyimbo zetu ambazo nyingi (sio zote tafadhali)zimejaa umbeya(taarabu) wanaume zamani walikuwa hawaimbi lakini siku hizi nao wamo.
 
Inawezekana mazingira ni fresh ila kichwani hamnazo,Marian Girls kuingia hapo lazima interview na lazima ufaulu vizuri interview.Ulishaenda St marian siku ya interview utashangaa ni MAGARI YAMEPAKI yasiyo na hesabu ila wanafunzi wanaochukuliwa ni wale wazuri kichwani sasa jumlisha na mazingira mazuri mwisho wa siku Darasa zima ni one na two za kuhesabu.

Idadi yao 84. Division One 79 na division Two 5.
 
Mosha ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa Resto Mosha wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro na mama Agatha Mosha Mhasibu wa NSSF mkoni humo.

Like Father Like Daughter!

Vitu vingine ni vya ukoo jamani!
 
Inaelekea wewe hupiga vilaza Makonzi teh teh teh

kilaza MPOLE huwa namwonea huruma sana na kwa kweli huwa najitahidi kadri ya uwezo wangu kumsaidia, kasheshe inakuwa kwa kilaza MJUAJI, ni yule ambaye hajijui kama kilaza, huwa nakosa tu uwezo wa kuchapa vibao, otherwise.......
 
Ndio unataka kusema kuwa waliosoma ST KAYUMBA na wakafeli ni mazingira magumu yamewasababishia?

Yaani mpendwa kuna Div 4 nyingi tu st Kayumba ambazo ukizifua ndani ya mazingira mazuri unapata Div 1 point 7. Mifano hai ipo.

Mtoto analea watoto wenzake, akirudi nyumbani ni House geli kwa mjomba, kuosha vyombo, kupika, kufua, kusafisha nyumba mpaka wakati wa mitihani. Anachelewa kulala, anawahi kuamka siyo kwa ajili ya shule, Kazi za nyumbani. Kisha awahi foleni ya daladala, pesa ya matumizi shuleni ni nauli ya daladala peke yake, kwa hiyo akiweza kutembea kilometa kadhaa asubuhi na jioni anapata hela ya muhogo mchana.

wakati akimsikiliza mwalimu anawaza jinsi alivyochoka na namna atakavyotembea kutoka posta mpya mpaka kiwalani, au Arusha Meru mpaka sakina, au Nyamagana mpaka kileleni kwa mlima kayumba mwanza kwenye nyumba yetu inayoning'inia ikichungulia ziwa victoria, au mwanjelwa mpaka Uyole, au Mwenge mpaka Singidani ziwani, au Tabora mjini mpaka Uyui, au Segera mpaka kwa matuku.

Hapo bado Mjomba hajaanza kumshangaza kisaikolojia na kumjeruhi kwa kuanza kumwinda na kumnyanyasa kijinsia. Bado mwalimu kazimdodo naye hajajitolea kumfundisha ''tuishieni" bure, chumbani kwake kule nanihiino. Usisahau muuza mihogo na mihogo ya bure yenye chachandu ya kuvutia. Kondakta naye anajitolea kumsafirisha bure kila siku tena bila kusumbuliwa, anakuwa First Lady wa daladala hiyo. Wasamaria wako wengi wengine wasamaria wema, wengine wasamaria fisi.

Haya tangu waigie Form Four mpaka wanamaliza hesabu wamefundishwa Topic mbili tu za Form Four maana za Form Three hazikuwa zimekwisha na hazitarajiwi kwisha mpaka siku ya matokeo.

English wamesoma Riwaya moja tu tena kwa Imla. Mtoto hajawahi kumiliki kitabu chake mwenyewe tangu azaliwe.

Wazazi ndio hivyo tena aidha wamekufa au la wamefariki.

Halafu uniambie kuna Div 1 point 7 hapa.

Ndiyo maana Charity inahitajika sana humu duniani.
 
masanilo asante kwa hili neno la busara!!

nani kakudnganya wewe, hamna cha sura ya mbuzi wala sura ya malaika hapa. anyone ca have a smart brain despite of hw they look like tafuta factor nyingine relevant

Nasikia wenye sura ya kitimoto ndo balaa! First class mpaka anaaga dunia hahahah
 
Back
Top Bottom