Nataka!!!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Ngugu mwanajf, baada ya kjadili mada iliyokuwa inazungumzia kile usichotaka(SITAKI), hebu sasa tujadili kile ambacho unataka kama ambavyo mimi:

1.Nataka Serikali inayojali watu na rasilimali zake kwa manufaa ya watu wake!

2.Nataka wabunge wanaosimamia haki na rasilimali za taifa bila kujali itikadi za vyama.

3.Nataka tume huru ya uchaguzi isiyopendelea chama kilicho madarakani.

4.Nataka Rais asiyekuwa ombaomba hata kwa vitu ambavyo vingeweza kuwa kwenye level ya uwaziri.

5.Nataka Rais anayetulia ofisini na si kuwa kama Vasco dagama!

6.
7.
8.... endeleza
 
Ngugu mwanajf, baada ya kjadili mada iliyokuwa inazungumzia kile usichotaka(SITAKI), hebu sasa tujadili kile ambacho unataka kama ambavyo mimi:

1.Nataka Serikali inayojali watu na rasilimali zake kwa manufaa ya watu wake!

2.Nataka wabunge wanaosimamia haki na rasilimali za taifa bila kujali itikadi za vyama.

3.Nataka tume huru ya uchaguzi isiyopendelea chama kilicho madarakani.

4.Nataka Rais asiyekuwa ombaomba hata kwa vitu ambavyo vingeweza kuwa kwenye level ya uwaziri.

5.Nataka Rais anayetulia ofisini na si kuwa kama Vasco dagama!

6.
7.
8.... endeleza

Ngugu ndio nini?
 
Nataka watanzania wenye mapenzi ya dhati kwa nchi yao bila kujali itkadi za dini chama na mila zao.
 
nataka JF iwe ni The Home of Great Thinkers ya ukweli, kusiwe na mamluki hasa kutoka zeutamu.
 
Nataka Jaji Mkuu aeleze ni kwanini kesi nyingi zinachukua muda mrefu kusikilizwa hadi kutolewa hukumu ilihali upelelezi unakuwa umekamilika kama alivyosema boss wa TAKUKURU Dr.Hosea hivi majuzi!
 
nataka watanzania wasiopendaa uzembe wala uvivu katika kufanya kazi zao..

nataka taifa linalojalii miiko ya uwajibikaji na sio unafikii wa dhamiraa..

pia nataka watumishi wa umma wanaojali kazi na mali za umma kwa manufaa ya taifa lao na sio nafsi zao...
 
Nataka viongozi waliopita wawajibishwa kutokana na kulisababishia Taifa letu Hasara kwa kuingia mikataba mibovu kama ya Richmond na mingine ya namna hiyo
 
Nataka viongozi walioko madarakani na waliokwisha maliza muda wao wawajibishwe kwa kuliingiza Taifa hasara kutokana na kuingia mikataba mibovu kama ya Richmond na mingineyo
 
Sio tu raisi anayekuwa ombaomba katika vitu ambav o vipo kwenye level ya Uwaziri, mimi nataka TAIFA Lisilopenda kuomba omba bali litumie fursa ya kuwa na wananchi wasomi na kuinvest kwa ajili ya maendeleo,
Nataka Taifa lisilo ombaomba bali litumie rasrimali ilizojariwa na mwenyezi Mungu katika kuzitumia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na vizazi vijavo.
Nataka TAIFA LISILO LA WATU WABINAFSI, ukitaka kutafuta kazi katika taasisi za umma basi lazima mjomba wako afanye kazi pale au awe yupo kwenye system, mfano MZURI BOT.
Nataka Taifa linalojali WASOMI na kuweka mipango thabiti ya kuwekeza katika RESEARCHES.
Nataka Taifa linalotenganisha SIASA na UCHUMI na linalojali mawazo ya wasomi na nataka TAIFA linalojali mawazo ya WANANCHI wake na sio kutumia FFU watu wanapodai haki zao (BRUTAL & REPRESSION LEADERSHIP).
Nataka TAIFA ambalo ukitaka kuwa MBUNGE, WAZIRI basi elimu ya chini iwe kuanzia DEGREE.

rom
 
nataka uwekezaji katika viwanda Tanzania
nataka Tanzania tuanze kutumia products zetu wenyewe badala ya ku-import asilimia kubwa
 
Nataka Taifa ambalo mtu akila Rushwa basi kesi yake inaendeshwa haraka na kuchukuliwa hatua za haraka ili alichoiba ba si kinarejeshwa kwenye umma na kuweka hadharani kuwa mtu yeyote atakaye kula rushwa basi adhabu yake ni KUNYONGWA.
Nataka Taifa ambalo mtu (Kiongozi) yeyote akihusishwa na kashfa anajiuzulu wadhifa wowote alionao kwenye Jamii tofauti na ilivo sasa.
Nataka Taifa ambalo Wananchi wake wako AGRESSIVE na tabia zozote za KUHUJUMU uchumi/Viongozi wanapotumia madaraka yao Vibaya au kula RUSHWA

Nataka Taifa ambalo VIJANA wake 2009/2010 wote watajiandikisha kupiga Kura kuchagua Viongozi wao, na Taifa ambalo Vijana wake wanaendana na NYAKATI, KIMAWAZO NA KIFIKRA. Muda unazidi kwenda na tunabaki palepale na Siasa za KIPUUZI.
 
Nataka wanaume nao waanze kuvaa sketi na magauni, maana wanawake tuko bize mno na suruali
 
Nataka rais aliye mcha mungu, mwaminifu kwenye ndoa yake na sio nyumba ndogo kila mtaa, mwenye mke mwaminifu na si fisadi.
 
Back
Top Bottom