nataka talaka

naomba mtu yoyote anayemjua mpelelezi yoyote yule atakae weza kunisaidia nataka amfuatilie mume wangu nataka nimshike live na mwanamke kwa sababu kila nikimshika kwenye simu anabadilika naombeni tafadhali nimechoka mwenzenu na uwongo wa huyu bwana kila siku

itakuwa vp ukimfuma ukakuta anapumuliwa...........maana umesema hata ile kitu haiulizii tena angalia...kama vp mkague kbs kwenye oo...kabla hujaanza tafiti
 
Dada kufumania sio suluhisho na mumeo kutoka nje ya ndoa hasa hasa mtaishia kudhalilishana tu na kumpa ushindi,
Km umechoka na huna mbinu za kistarabu za kumtuliza mumeo basi fungasha mabegi urudi kwenu.

Ungekuja na wazo la kuomba ushauri wa kujua chanzo cha tatizo la mumeo na namna ya kumtuliza ningeungana na ww ila hili la kutafuta suluhisho bila kujua chanzo cha tatizo mie mgeni.
 
Umejiuliza nini hasa wataka? Kama unahakika kua mumeo ana kucheat kuna tofauti gani na ukimfuma.... au labda naomba kujua what difference will it make? Na je upo tayari kuyapokea matokeo hasa ukipata ushahidi wa uhakika?

Alafu jamani kwanini ujiite Unlucky? Ikiwwezekana badili jina, hilo ni kama wewe mwenyewe wajitia mikosi.... Pole na pressure za ndoa dear...

Umewahi kunisemea bibie ! Hivi mtu uzae mtoto umwite Mwizi then ajekua Mwizi kweli , au umwite Malaya na awe Malaya ! Utamlalamikia nani ?
 
naomba mtu yoyote anayemjua mpelelezi yoyote yule atakae weza kunisaidia nataka amfuatilie mume wangu nataka nimshike live na mwanamke kwa sababu kila nikimshika kwenye simu anabadilika naombeni tafadhali nimechoka mwenzenu na uwongo wa huyu bwana kila siku

Kuna mwenzio keshapoteza maisha sababu ya huo mchezo. Unapiteza muda wako na pesa zako bure tu! Unampeleleza so what? Ivi unafahau kuwa hivyo unavyomfuatilia ndo anapata chance ya kukuumiza?

Naomba nikushauri vitu viwili.
  1. Kama unaona jamaa yako si mwaminifu kabisaa na kwamba anakucheat na hana mapenzi kwako basi fanya kati ya haya
  • Achana nae
  • Na kama wampenda saaaaaaaaaaaaaaaaaana and you think there is no way ukamuacha, basi endelea nae na uwe mvumilivu sana huku ukimwomba Mungu wako kama ikiwezekana kikombe cha UKIMWI kikuepuke.
2. Kama unaona jamaa yako anakupenda ila tu tamaa za kijinga zinamsumbua basi BE VERY EXPENSIVE TO HIM.

Ni huo tu ndugu
 
mpendwa dadangu,

kwanza,
hakuna mwanaume mnyama hapa duniani, tena mbele ya mwanamke, hakuna!

pili,
tangu mwanzo Mungu allimuumba mtu mume na mtu mke na akaona kuwa ni vyema. kwa hiyo mtu atawaacha wazazi wake na ataishi na mke/mume wake nao watakuwa mwili mmoja hadi kifo kitakapowatenganisha. Mungu anachukia kuachana!

tatu,
jukwaa uliloweka mada yako si muafaka, ungepeleka jukwaa la sheria

nne,
hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza kutoa talaka hapa nchini. talaka inatolewa mahakamani pekee.

tano
kama unaihitaji unapaswa kwenda huko ila kiutaratibu unaanzia idara ya ustawi wa jamii katika halmashauri yako nao watakuelekeza kwenda baraza la usuluhishi wa ndoa na familia ambako mtaitwa wote wawili (wewe na mumeo) kusuluhishwa na huko waambie bila kutafuna maneno kuwa unataka talaka na uwaeleze sababu za kufikia uamuzi huo, nao watakupa barua ya kwenda kufungulia shauri lenu mahakamani. huko mahakamani hakimu akiridhika kuwa ndoa yenu imevunjika kabisa kiasi cha kutoweza kurekebishika, basi atatoa hati ya talaka unayoitaka. atatoa nakala mbili, moja yako na nyingine ya mumeo. pia katika hati hiyo, kutakuwa na maamuzi juu ya mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja, malezi ya watoto na matunzo yao baada ya talaka na uamuzi kuhusu mahari!

ubarikiwe sana mpendwa,

Glory to God!

Dada uliyetoa mada, nafikiri ms.judith kaeleza vizuri na kwa ufasaha, sasa umeshafahamu pa kuanzia, kazi kwako kuamua talaka au utunze ndoa yako na watoto.
Kumbuka unapofanya maamuzi ni lazima ukubali matokeo yake, tulia na ufikirie tena kama hicho ndicho unachotaka.
Otherwise pole sana na mwenyezi mungu akuongoze.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom