nataka talaka

unlucky

Senior Member
Aug 9, 2011
199
56
naomba mtu yoyote anayemjua mpelelezi yoyote yule atakae weza kunisaidia nataka amfuatilie mume wangu nataka nimshike live na mwanamke kwa sababu kila nikimshika kwenye simu anabadilika naombeni tafadhali nimechoka mwenzenu na uwongo wa huyu bwana kila siku
 
tatizo la fumanizi huwa ni maamuzi.Kabla huja embark kwenye hiyo odyssey huwa umekwisha kata na shauri kuwa 'nikmbamba live,haya ndo yatakuwa maamuzi yangu',sio unajiendea tu kufumania.
 
wakike bei tutaelewana jamani mie niko kwenye shida na wala sitanii hapa ndo mana nimekuja jf kuomba msaada bwana amevuka mipaka nia yangu nimuone live ndo hapo nitashika uongo wake
 
Kama umeshahakikisha kwamba ni kicheche siumwache unataka umfumanie then wht. Au unasubiri mpaka akuletee kale kaugonjwa ambako hakatibiki,anywei rest in peace jast in case..
 
jamani wapenzi habari zenu naomba msaada mimi nanyanyasika sana na nimevumilia sana na mume huyu mnyama naomba msaada nataka talaka hataki kutoa niende wapi ambapo nitasaidiwa pamoja nipate haki yangu na watoto wangu ambao ni wadogo kabisa
 
Naskia Bakwata wana tume maalum la kusaidia in that case.
 
wakike bei tutaelewana jamani mie niko kwenye shida na wala sitanii hapa ndo mana nimekuja jf kuomba msaada bwana amevuka mipaka nia yangu nimuone live ndo hapo nitashika uongo wake

Wakike akikuchukulia yeye bwana ako? Usiangalie yanapoishia macho yako, fikiria na mbele zaidi
 
mpendwa dadangu,

kwanza,
hakuna mwanaume mnyama hapa duniani, tena mbele ya mwanamke, hakuna!

pili,
tangu mwanzo Mungu allimuumba mtu mume na mtu mke na akaona kuwa ni vyema. kwa hiyo mtu atawaacha wazazi wake na ataishi na mke/mume wake nao watakuwa mwili mmoja hadi kifo kitakapowatenganisha. Mungu anachukia kuachana!

tatu,
jukwaa uliloweka mada yako si muafaka, ungepeleka jukwaa la sheria

nne,
hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza kutoa talaka hapa nchini. talaka inatolewa mahakamani pekee.

tano
kama unaihitaji unapaswa kwenda huko ila kiutaratibu unaanzia idara ya ustawi wa jamii katika halmashauri yako nao watakuelekeza kwenda baraza la usuluhishi wa ndoa na familia ambako mtaitwa wote wawili (wewe na mumeo) kusuluhishwa na huko waambie bila kutafuna maneno kuwa unataka talaka na uwaeleze sababu za kufikia uamuzi huo, nao watakupa barua ya kwenda kufungulia shauri lenu mahakamani. huko mahakamani hakimu akiridhika kuwa ndoa yenu imevunjika kabisa kiasi cha kutoweza kurekebishika, basi atatoa hati ya talaka unayoitaka. atatoa nakala mbili, moja yako na nyingine ya mumeo. pia katika hati hiyo, kutakuwa na maamuzi juu ya mgawanyo wa mali mlizochuma pamoja, malezi ya watoto na matunzo yao baada ya talaka na uamuzi kuhusu mahari!

ubarikiwe sana mpendwa,

Glory to God!
 
yani huyu si mume mnyama nyie acheni tu mie nataka kuchukua action hii ya kufumania ili niprove uongo wake anaoleta kila siku ye anajifanya hana mwanamke wakati mie ananifan
ya kamambwa na nimeona msg za wanawake kwenye simu yake na sat sun anashinda nae siku nzima yaani natamani nijiue loo nimechoka
 
nenda bakwata kuna baraza la usuluhishi wakishindwa kuwasuluhisha wanampa mlalamikaji barua aende mahakamani,
 
yani huyu si mume mnyama nyie acheni tu mie nataka kuchukua action hii ya kufumania ili niprove uongo wake anaoleta kila siku ye anajifanya hana mwanamke wakati mie ananifan
ya kamambwa na nimeona msg za wanawake kwenye simu yake na sat sun anashinda nae siku nzima yaani natamani nijiue loo nimechoka
Ukisha mfumania ndo inakuaje sasa?
 
hiyo tume iko wapi manake si tulioana bakwata

Mmeoana Bakwata mkayamalize Bakwata. ukitaka kuyamaliza JF ukiolewa tena uje hapa tukuoze siku ukitaka talaka tutayamaliza hapahapa JF.

Kama kuna wazee wako au wake, nduguzo au wazee wenye hikma, ungeanzia hapo kabla ya kwenda mbali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom