Nataka kuwa mfugaji nifanyeje?

guta2010

Member
Apr 12, 2010
7
0
Hi wapendwa wana JF mi nina shamba la ekali 16 nje kidogo ya jiji(Dar) nataka kufuga kuku na nguruwe but sina pesa ya kuanzia mradi huo.naomba mawazo yenu nifanyeje niweze kutoka katika maisha aya magumu.
 
Uza sehemu ya shamba upate mtaji wa kuanzisha hiyo biashara...Maana hata ukipewa mbinu za ufugaji kama hauna hela za kuwekeza ni kazi bure..
 
Fanya utafiti na kisha piga mahesabu ya bajeti ya mtaji wa kuanza kazi ya ufugaji: Gharama za ujenzi wa mabanda ya mifugo, gharama za mifungo yenyewe ya kuanzia, chakula cha mifugo at least kwa mwaka mmoja, matibabu . Kisha uza sehemu ya shamba lako na aanza kazi mara moja.
 
mkuu ... jitahidi uweze kufanya pilot project angalau kuku mia mbili wa mayai ..... halafu nenda kwenye microfinance bank kama access, Akiba NMB waonyeshe unachofanya lazima watakupa mkopo wa kuendeleza mradi ......
 
Hi wapendwa wana JF mi nina shamba la ekali 16 nje kidogo ya jiji(Dar) nataka kufuga kuku na nguruwe but sina pesa ya kuanzia mradi huo.naomba mawazo yenu nifanyeje niweze kutoka katika maisha aya magumu.

Usiuze sehemu ya hilo shamba eti ili upate mtaji, ukifanya hivyo utakaribisha matatizo kwa kuwa huyo uliyemuuzia huenda akaweka pingamizi usifuge na pengine akakushtaki. Tafuta namna nyingine ya kupata mtaji, unaweza ukatafuta hati ya eneo hilo ili uweze kupata mtaji katika benki.
 
Usiuze sehemu ya hilo shamba eti ili upate mtaji, ukifanya hivyo utakaribisha matatizo kwa kuwa huyo uliyemuuzia huenda akaweka pingamizi usifuge na pengine akakushtaki.
ni vipi amshtaki au amuwekee pingamizi wakati kila mtu atakuwa anamiliki sehemu yake? Au sheria ya ardhi ndio inasema hvyo?
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Back
Top Bottom