Nataka kumng'oa Vita Kawawa (jimbo la Namtumbo) kupitia CHADEMA... Ushauri pls!

Jiandae kwa uchawi maana bwana mdogo ni mchawi ile mbaya. Ana waganga kila kona ya nchi mpaka Uarabuni.
 
mwaka wa uchaguzi 2010 nusura aondolewe kwenye kura za maoni ccm na mama sijaona, kama sio jina la marehemu baba yake leo hi angekua kwenye kimgahawa chake pale millenium towers. wakuu wa ccm wakaamua kumpatia ubarozi wa japan mama sijaona ili dogo aendelea kuvimbisha shavu lake. dogo kwa kweli hakubariki namtumbo. mkuu tia timu utamng'oa tu. all the best
 
Kwataarifa yako hawezi peleka maendeleo kucha kutwa wanamjia Dar kubom mbunge wa watu anashindwa hata kufurahia posho zake, kinachomsaidia ni mkewe mchakarikaji
 
Wakuu wana JF na wachambuzi wa mambbo ya siasa....!

Nina lengo thabiti la kutaka kulikomboa jimbo la Namtumbo ili niweze kuwatumikia vyema wananchi wa Namtumbo na kuwaletea maendeleo.

Wiki lilopita nilikua huko jimboni kwa kazi maalumu na nilibahatika kupita ktk karibu maeneo mengi....kama vile Msindo, mawa, mlilayoyo, hanga, mputa, kitanda, mgombasi, nambecha, namtumbo yenyewe, suruti, mchomoro, ligera, mkongo, mtwara pachani, namabengo, lumecha hadi mtakanini(kijiji alichozaliwa mama yake Vita kawawa...na ndiko ukweni kwa marehemu mzee kawawa.......!

Kwa kweli hizo sehemu zote nilizopita wanamlaani sana mbunge wao kwa sababu amekuwa mchumia tumbo lake tu bila kujali maendeleo ya wapiga kura wake....mfano...

Hivi sasa ana majumba kadhaa pale namtumbo aliyeyajenga kwa kutumia pesa ya rushwa kutoka kwa wamarekani wanaochimba madini ya Uranium kule mbuga ya Seluu ila asipige kelele kule bungeni,

Wananchi wa namtumbo wakulima wa tumbaku...ni kilio tu mwaka huu...tumbaku imerudishwa toka morogoro hali yeye ni menyekiti wa bodi ya tumbaku tanzania.....

Shule nyingi za st.kayumba..maarufu shule za kata hazina madawati, majengo yamesimama kuendelezwa toka lowasa ajiuzulu kuwa waziri mkuu hadi hii leo....

Kuna baadhi ya vijiji hadi leo wanakunywa maji ya mtoni ambayo sio salama,

Miradi mingi ya afya imesimama toka project ya Tasaf ....hakuna kilichoendelea....!


Nipo huku Arusha lakini nia yangu ni kuikomboa Namtumbo kutoka chama cha ******* na hatimaye CHADEMA ichukue jimbo na kuleta maendeleo kwa wananchi.

NB: Huyu mbunge anaishi dar maeneo ya mikocheni hapo kajenga gorofa yake anakula kuku, huku namtumbo wananchi hawamjui toka wakati wa kuomba kula....sio kura.....hadi hii leo, na akifika huishia kuleee namtumbo ofisini kisha huabiria ndege ya wazungu (watu wa madini ya uranium) na kurudi Dar!

Kifupi wananchi hawampendi kabisaaaa.....nataka kuikomboa namtumbo via Chadema.....Naomba ushauri wako nianze vipi au nitoke vipi ili kuli...ng'oa gambaz huko Namtumbo!!!


karibu kwa ushauri/Maoni yako.

Kama kweli umeamua kufanya hivyo, consider him as your enemy first, keep him closer and make him your friend. Mshauri projects za kufanya kwa manufaa ya wananamtumbo, mwambie uko tayari kujitolea kwa manufaa ya wananamtumbo na yeye pia. Abraham Lincoln alipata kusema I destroy my enemies my making them my friends. Mkiwa marafiki, utajua silaha zake, mkiwa marafiki hatakudoubt alikuona unawasaidia wananchi wa jimboni kwenu kwa kuwapa mwamko mpya. Then come 2015, una unfold makucha yako, mwenyewe atatamani ardhi ipasuke kwani utakuwa umetokea jikoni na wananchi wameshakujua.
 
Chagua chama kwa kuangalia matokeo ya 2010, angalia CUF au Chadema nani alikuwa anamfuatia CCM,
 
Nitakupa sapoti ya kutosha, nakuahidi kuchukua likizo kwa ajili ya kukusaidia kwa sababu na mimi ni mtu wa kule ila kwa sasa siishi kule... All the best Kisaka!!
 
mh! Jamani! Vita ni jirani yangu kabisa! Hilo ghorofa mbona silioni? Napita tu mpaka baadae!


Ni jirani yako wap?? Mikocheni au??

Anyway, siyo lazima aishi kwenye hilo gholofa ndiyo liwe lake?? Lamda hapa cha muhimu mleta hoja atuwekee walau na kaushahidi kadogo!!
 
ni jirani yangu mikocheni na ni mtu asiependa makuu! Wala sioni ufisadi wake kwa maana mkewe ni mchakalikaji sana. Na nyumba yao si ya kutisha ukilinganisha na majumba ya eneo hili. Tatizo yuko kwa kina *******.
 
Tumechoka na majina kujirudia bora ukamtoe tujue moja.ukitaka support tutakupa hata through mpesa.
 
Mm nataka nipambane na wewe ktk chama utakachogombea,, vp ntakuwa nimefanya makosa?
 
....sina uhakika lkn nilisikia huyu aliwekwa kwa fitna ili kumtoa yule former naibu waziri, prof. ambaye sasa ni mgonjwa sana ! My guess, unaweza kufanya kautafiti flan flan through watu wa karibu ktk hiyo familia ya mbawalla ambao nina uhakika hawakufurahishwa kabisa za rafu alizochezewa ndg yao ! In otherwords unaweza kupata nyeti za ndani ili ikifika muda basi unakuwa na B 52 za uhakika, so next time ukiwa hapo Namtumbo fika nyumbani kwa prof. kusalimia, au ukiwa DSM !

Goodluck...
 
Hauna Jina, Hauna Sababu, Unatangaza bila kusema utaisadiaje hilo jimbo Vita Kawawa analoliongoza

Unatafuta Umaarufu tu humu ndani ya Jamii Forum haitoshi...

Unakuwa tu kama hao watu wa CCM; kujitangaza ili kupata baraka na hata kama haufai...

Nenda kijijini ujionee mwenyewe matatizo ya Wananchi na Utokwe na Majasho sio ndani ya internet Cafe kupigwa na kaupepo
 
Wazo ni zuri,zingatIa ushauri wa RUV ACTIVIST,Sisi tumeshamaliza kazi Hanga,Mputa na Kitanda.Tuwasiliane kwa 0758921871 tuendelee kujenga chama,Karibu
 
Back
Top Bottom