Nataka kumfungulia........ Mashtaka

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
Naomba kujua kama naweza kumfungulia mtu mashtaka kwa niaba ya NCHI/JAMHURI.
Nasema hivyo baada ya kuchoshwa na ngonjera za serikali,kuwa ushahidi haujakamilika kumfikisha mtuhumiwa mahakamani
 
Last edited:
Nafikiri unaweza as a concerned/affected individual and u have evidence. Disaini ya Mtikila style, au sijakuelewa?
 
Nafikiri unaweza as a concerned/affected individual and u have evidence. Disaini ya Mtikila style, au sijakuelewa?

Kimsingi unaweza kabisa kumfungulia mtu yeyoote yule mashitaka nchini Tanzania.

Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa hicho unachomshitakia kina public interests (malahi ya Umma). Kwa mfano mtu anachafua mazingira, mtu anaiba mali ya umma, mtu hatimizi wajibu wake aliopewa kisheria(kwa mfano Waziri wa Mambo ya ndani anweza kushitakiwa kwa kushindwa kuwalinda raia kama vile ile issue ya Albino).

Ukitizama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara) katika Ibara ya 27 inasema hivi;(nanukuu).....

(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.
(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao. (mwisho wa kunukuu)

Kwa hiyo kama inavyobainishwa na Katiba ya Nchi yetu ni wazi kuwa ni jukumu la kila mwananchi kulinda na kudumisha mali ya Umma wa Watanzania. Kimsingi na kwa mujibu wa sheria hii mama,kila Mtanzania anayo mamlaka ya kufungua kesi katika mahakama yenye uwezo wa kisheria ili mradi tu dhana kuu ya kesi hiyo iwe ni kulinda maslahi ya Umma (for the public Interests).

Kesi za namna hii ndizo kama zile ambazo Mheshimiwa Mtikila amekuwa akizifungua dhidi ya Serikali tangu miaka ya tisini.(naungana na Kaniki) Hili linadhihirisha kuwa inawezekana. Hivyo naomba kutofautiana na Kang.
 
Nawashukuru wote walio changia,
SASA,MBONA BW.MENGI HAWAFUNGULII MASHTAKA WALE MAFISADI PAPA NA ANADAI ANA USHAHIDI?au naye haitakii MEMA NCHI HII TANZANIA?
 

Mkuu Kang, sivizuri kusema tu......Hauwezi......toa hoja ya kwanini hawezi kumfungulia mtu mashtaka kwa niaba ya Jamhuri...ili umsaidie zaidi mtoa mada na sisi wengine kwa ujumla!
 
Ninadoubt kama inawezekana labda katiba irekebishwe maana kuna kukwama mahala fulani ktk ufunguaji hii kesi.
 
swali lako halieleweki vizuri, lakini kama untaka kufanya kama Kenn Starr alivyofanya katika kesi ya Bill Clinton haiwezekani. Pia naomba kutofautiana na mpandafarasi, kuhusu kesi anazo fungua mtikila dhidi ya serikali.


Utaratibu wa kuwashitaki watu binafsi ni tofauti na ule wa kuishitaki serikali na sheria zinazotumika ni tofauti.Tukiongelea makosa ya jinai watu wenye makosa watashitakiwa na serikali, na utaratibu utakao tumika ni ule ulioko kwenye Criminal Procedure Act. 1985 , R.E 2002


Kuhusu kesi anazofunguaga Mtikila dhidi ya serikali utaratibu unaotumika ni ule ulioko ktk Government Proceedings Act no 40 , 1967 as ammended in1974.
 
Nawashukuru wote walio changia,
SASA,MBONA BW.MENGI HAWAFUNGULII MASHTAKA WALE MAFISADI PAPA NA ANADAI ANA USHAHIDI?au naye haitakii MEMA NCHI HII TANZANIA?[/
QUOTE]

Sasa umeeleweka mkuu, lakini approach yako mbovu watu wamekwisha choka na hoja za hao wapumbavu.Wanajadili masuala ya kitaifa na huo ushabiki unazo thread zake zina majina hayo hayo ( MengiVsRostam etal). Ukitaka wakufuate wewe badili kichwa cha thread yako kuwa Kwa nini Mengi hawafungulii mashtaka mafisadi? watakuja wengi tu.. mchana mwema kama upo bongo.
 
Ni serikali peke yake inayoweza kufungua criminal case, mtu yoyote anaweza kufungua kesi ya madai (civil case) lakini hiyo haina kifungo sana sana utalipwa hela.
 
Yes, Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai inaruhusu kumfungulia mtu kesi na ukaiendesha binafsi/ wakili wako badala ya utaratibu wa kawaida wa kutegemea ofisi za Serikali kama vile TAKUKURU na DPP.

Hiyo inaitwa 'private prosecution' ila hatari yake ni kwamba DPP bado anairatibu, so kuna hatari ya ukifungua tu (kama sheria inavyokupa haki) naye akaifuta (kama sheria naye inavyompa haki) kwa kile tunachoita nolle proseque (kutoona haja ya kuendelea kushitaki).
 
Yes, Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai inaruhusu kumfungulia mtu kesi na ukaiendesha binafsi/ wakili wako badala ya utaratibu wa kawaida wa kutegemea ofisi za Serikali kama vile TAKUKURU na DPP.

Hiyo inaitwa 'private prosecution' ila hatari yake ni kwamba DPP bado anairatibu, so kuna hatari ya ukifungua tu (kama sheria inavyokupa haki) naye akaifuta (kama sheria naye inavyompa haki) kwa kile tunachoita nolle proseque (kutoona haja ya kuendelea kushitaki).


Hivyo siwezi kuwafungulia mashtaka wale watuhumiwa wa UFISADI PAPA?Kwani kesi yao ni ya Jinai au Madai?
 
yes, sheria ya mwenendo wa mashitaka ya jinai inaruhusu kumfungulia mtu kesi na ukaiendesha binafsi/ wakili wako badala ya utaratibu wa kawaida wa kutegemea ofisi za serikali kama vile takukuru na dpp.

Hiyo inaitwa 'private prosecution' ila hatari yake ni kwamba dpp bado anairatibu, so kuna hatari ya ukifungua tu (kama sheria inavyokupa haki) naye akaifuta (kama sheria naye inavyompa haki) kwa kile tunachoita nolle proseque (kutoona haja ya kuendelea kushitaki).


poa mkuu
 
Unaweza kufungua mashtaka ila kitakachokushinda ni endapo utahitaji nyaraka toka ofisi fulani k.m. bank statement ya RA/RM, utazipata kwa kutumia mamlaka ipi? Automatically utajikuta umeipeleka kesi TAKUKURU au Polisi ambao wana mamlaka kisheria kuamuru benki au idara/ofisi yoyote kutoa nyaraka. Kwa hiyo unaweza kuona kuwa sheria imeruhusu private prosecution lakini kuna hiyo limitation. Wewe jiulize kama unaweza kumhoji RA/RM ili upate maelezo yake yakatumike kama ushahidi mahakamani, atakuuliza wewe ni nani? Polisi? etc. So, while it is legally allowed it is unfortunately practically impossible to do so.
 
Back
Top Bottom