Nataka kugombea ubunge.

Soma kwanza. Bado unapata shida sana kuandika hata Kisawahili, utawezaje kusoma miswada ya Kiingereza?
 
Nindoto yangu kugombeya ubunge maishani mwangu,kwasasa nasomea ualimu, mwaka wa mwisho,namaanisha 3rd yr kuanzia october 8, nawaza. na natamani sana kuwa mkombozi na mtetezi wa wanyonge maisha yangu yote ila tatizo sijui nitaanzia wapi ili kutimiza ndoto hii.Wadau,wanasiasa nisaidieni mawazo hapa niko sirious kugombeya ubunge katika jimbo moja hapa Tz je niwapi pakuanzia,
Kwanza itabidi niwe na pesa kiasi gani ili nigombee huo ubunge?

kutokana na fani nayo isomea na jun mwakani natumaini nitakuwa nime maliza je nitakuwa sahihi kugombeya?

Je ninini chauongeza au kujiandaa kielimu kiuchumi ama kisisiasa ili niwe kamili.
Mheshimiwa mtarajiwa,
Ili kuwa Mbunge kuna mengi sana ya kujifunza... kwanza lazima ufahamu Mbunge ni mwanasiasa na hakuna chuo chochote kinachotoa elimu ya Ubunge. Kwa kuanzia unaweza kufanya haya yafuatayo:
1. Anza sasa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hapo chuoni kwako anzia mwakilishi wa darasa hadi uraisi wa chuo..hii inategemeana na muda wako hapo chuoni
2. Jichanganye hata kwenye mambo ambayo huyapendelei.. sehemu za kijamii...kugombea nafasi mbalimbali za uongozi popote upatapo nafasi kuanzia mwenyekiti wa kamati za maandalizi ya sherehe za kijamii hadi kwenye vilabu mbalimbali vya michezo... jipitishepitishe kwenye vilabu/ Baa toa ofa za vinywaji watu wakujue..kumbuka siasa haina dini.
3. Jifunze kutokuwa na misimamo wala kutunza kumbukumbu za nyuma yaani kama leo uko CCM ukasema CDM ni wachawi halafu ukakosa nafasi ya kugombea ndani ya CCM kisha ukaamua kuhamia CDM basi usisite kusema CCM ni wanga.
4. Jitolee kufanya kazi mbalimbali za kijamii... hamasisha utunzaji wa mazingira eneo ulilopo..hamiasisha watu wapande miti, walinde vyanzo maji nk. pia kuwa mbele kwenye shughuli zote za kutetea haki..kama maandamano nk.... usiogope virungu vya polisi.
5. Angalia mapungufu ya kiongozi ambaye unataka kuchukua nafasi yake jaribu kuwaeleza watu mapungufu hayo na vipi unadhani unaweza kutoa suluhisho......
6. Jitunze pia ujiheshimu hasa ukiwa kwenye mwanga..na njia pekee ya kujionyesha hivyo ni kwenda kwenye nyumba ya ibada...chagua kukaa sehemu ya mbele kabisa..lakini usijitambulishe nje ya nyumba kuwa wewe ni dhehebu gani.
7 Jifunze kuwa na ustahimilivu na usiwe na jazba yaani kama umetukanwa basi usirushe ngumi wala kwenda kufungua mashtaka isipo kuwa na wewe unatakiwa ujibu mapigo kwa kutukana....hayo ndiyo maisha ya kila siku ya mwanasiasa.

Mheshimiwa mtarajiwa..... kama una nia ya kweli kwamba unataka kuwatetea wanyonge na si tamaa ya marupurupu wanayopata wanasiasa au nafasi ya kufanya ufisadi...anza kuwatetea kwa nafasi utakayo kuwa nayo ya ualimu....wafundishe vijana wetu waelewe jitolee muda wako wa ziada waelimishe wale wazito kuelewa hapo utakuwa. umewatetea kiasi cha kutosha.
Kama ni mchamungu basi nakushauri ubaki kwenye kazi yako..... kwani kazi ya ualimu ni kazi ambayo rahisi kwenda peponi/Mbinguni kuliko kazi ya siasa ambayo kila siku unajilimbikizia dhambi na mwisho wake unaishia motoni.
..........yapo mengi sana.........tena sana
 
Good idea. Jipange, ubunge hausomewi hata kama uko kama Lusinde, uongozi hausomewi bali ni kipaji kama Nyerere, maamuzi hayajadiliwi hata kama utakuwa kama Jk. Unavyoishi ndivyo utakavyokuwa kama Obama. Be strong in +ve minds. Go ahead.

Hakuna patent ya ubunge wala urais. Zote ndoto tu.

Mkuu umenivunja mbavu sana
 
Pamoja na madhaifu yako,nakushauri ujiamini mana hapa tu ambapo id yenyewe ni hidden umeshindwa kutaja hata jimbo.pili kuanzia hapa chuoni kwako uwe karibu na watu pia nenda kwenye ofisi za ccm zilizopo karibu na hapo onana na kiongozi yeyote mwambie unahitaji kujua abc za namna ya kuwa mwanachama safi na hatimaye uwe kiongozi mhm hasa mbunge.kama upo 3rd yr hujui chochote ina mana hata gs ilikupita pembeni,ds pia na hata taarifa mbalimbali za mambo hufatilii.
 
Kama kweli unauchungu na nchii na kwamba unataka kulete mageuzi yenye tija na maendeleo katika nyanja za kiuchumi, siasa na jamii kwa ujumla nakushauri ukimaliza chuo nenda ukafundishe watoto wa Watanzania kokote utakapopangiwa.Maana utakuwa unawakomboa kifikira, ila kama umeona taaluma yako hailipi na unatamaa ya madaraka na miposho basi ingia kwenye siasa maana siasa inalipa.
hengo umemjibu vema watu wengi wanafikiri nchi inajengwa na viongozi wa kisiasa kumbe hata mama lishe anayepika karibu na jengo kubwa linaloendelea kujengwa ana mchango mkubwa sana katika ujenzi wa Taifa hili kuliko wale wabunge wanaolala bungeni au kupinga hoja zote za wapinzani
 
Last edited by a moderator:
Yawezekana mtoa hoja ni mtu mwenye nia,uwezo na kusudi jema kwa taifa lake lakini ana mapungufu madogo madogo ambapo kama JF inavyonilea mie pia naye aweza kuja kuwa mtu mzuri japo nimepata shida kuelewa ni vipi anataraji kumaliza degree pasipo kufaham kuandika vizuri.Lakini hajachelewa naamini tunajifunza kwa makosa na hakuna mkamilifu.
Mkuu uongozi ni karama je, unayo?Naamini katika kusoma kwako umepitia Elimu ya Msingi,Elimu ya sekondari ya Kawaida,Elimu ya sekondari ya juu na Pia chuo kikuu ambapo ndipo unakaribia kumalizia ama elimu yenye mahusiano ya kukufikisha hapo,sasa naamini toka huko ulikotoka una historia ya kuwa kiongozi hivyo naamini utaweza na Mungu akusaidie ufikie ndoto yako lakini isiwe ndo ajira unaitaka(i mean ufanye siasa ndo inaprovide mahitaji yako muhimu utapotea mbaya just fanya siasa kama sehem ya kuchangia ujenzi wa Taifa lako),nakushauri jifunze kupitia ambao wapo ktk siasa lakini pia watazame wanavyojieleza nawe uanze mazoezi ya kuzungumza kwenye Public.
Yatambue matatizo ya eneo lako na uone uwezo wa kukabiliana nayo then chama utachogombea watakupa nafasi endapo wakikuona kama una mvuto wa kisiasa na pia kama ni competitive.JIPANGE MKUU
 
DU!jamani naomba muwe wapole, pia tumieni lugha nzuri kidogo kwani halikuwa lengo langu kukosea namna ile.Najua kwasehemu nimewakera na ndio maana nawaombeni msamaha,kumbukeni kwamba nimeomba toka kwenu ushauri na sikutarajia kupokea matusi na kukatishwa tamaa kama wengine walivyo sema. Kwa hili nimejifunza nitajitahidi kuwa makini sana wakati mwingine.
Yote mlio nishauri nimeyapokea na nitayatendea kazi.
Lakini kila mtu anao uhuru wa kutoa mawazo yake;hivyo basi mwenye kunishauri anishauri mwenye kukosoa anaweza kufanya hivyo kwasababu. ameona makosa kwangu na mkosaji huadhibiwa.
 
Back
Top Bottom