Nataka kugombea ubunge Karatu 2015

Ameona mwanga wa radi nje akadhani kumekucha!ahaaahaa rudi kalale dogo,kukikucha utaamshwa tu,tutakwenda pamoja,hatuwezi kukuacha bwana mdogo sawa eeh?

Lori!Una uhusiano wowote na Lori wa CCM ambaye kwa miaka zaidi ya 20 sasa anagombea kwa CCM Karatu na kupigwa chini. Kaa chini utafakari ila ninavyojua hali ya siasa kwa Karatu bado una safari ndefu
 
hilo jina la Lori linafanana na la mgombea ubunge wa magamba aliyepigwa chini na mch Natse 2010,je una uhusiano naye?isije ikawa amekutuma halafu uje kujitoa dakika za mwisho na kuliachia gamba jimbo!
 
Nivema ukaanza na kuset mizizi kwanza kabla hujaamua kupanda juu. Hivyo ni vyema ukajipanga kisiasa na kiutendaji hasa kwa kuainisha ulivyojipanga kuingia , ulivyojipanga kuwatumikia wananchi husika na msukumo wa kugombea unatokawapi?

Au kama mpaka muda huu huja set mabo basi ni vyema ukaanza na kuset mambo kwenye nafasi ndogo kama serikali ya mtaa au yakijiji (kutokana na uchache wa muda) then ukifanikiwa uitumie hayo mafanikio yako kama stage ya kuelekea mjengo. Huu ni ushauri tu waweza uchukua ukiona vema na pia waweza utupa mbaaliiiiiiiiiiiiiiiiii km hauja kidhi vigezo vyako
 
Peleka tangazo hili ITV huko ndiko wanakotangazia nia!.. Kwa sasa CDM ipo kazini kuandaa kata na majimbo yote kwa ajili ya uchaguzi!... Makamanda wa UKWELI wa taelekeza nguvu zao kujiandaa kuchukua majimbo yaliyo mikononi mwa MAGAMBA!...
 
Mkuu wenzako wanapigwa Mabomu kwenye M4C wewe unakula kiyoyozi UDSM halafu uachiwe jimbo kirahisi rahisi tu????
 
Gwarugwe, achana na hiyo plan haraka sana, endelea na profession yako. Unless kama unataka kugombea udiwani, otherwise nina hofu na nia yako ya dhati. Usije ikawa umetumwa na magamba kuharibu mipango ya M4C
 
View attachment 63521

JINA-Moses K. Lorri
NATIONALITY-Tanzanian
EDUCATION-BED PSYCHOLOGY 2008 UDSM
CURRENT POSITION-College tutor
PLACE OF BIRTH-Endallah village in Karatu district.
POLITICAL PARTY-CHADEMA.
AGE----31 years old

Ndugu zangu watanzania,naomba kuchukua nafasi hii kuwajulisha kwamba nimeamua kuchukua uamuzi mgumu kugombea ubunge katika jimbo la karatu kupitia chama cha demokrasia na maendeleo.Lengo hasa ni kuwatumikia wananchi wa karatu kwa uadilifu. Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa kwanza ni haki yangu kikatiba na pili nina uwezo wa kutosha kwa kushirikiana na wananchi wa karatu ili tuweze kuleta maendeleo kwa pamoja.Naomba vijana wote wa kitanzania kuniunga mkono kwa hili ninalotaka kufanya.

AHSANTENI SANA

Maliza kulipa mkopo wa HELB kabla ya kuingia katika siasa. Kumbuka, siasa si hasa. Hata hivyo, JF wote hawatoki jimbo la Karatu; inawezekana ukakosa kupata maoni wakilishi ya wananchi wa Karatu.

By the way, kwa nini unataka kukimbia "wito" wako wa ualimu?
 
hongera sana ila hapo si kuna mbunge au?na ana mapungufu gani na uliwasiliana na uongozi kabla ya kusema haya?na je unaona ni muda sahihi wa kusema hayo kwa sasa?na je hauna njia nyingine ya kulisaidia jimbo lako zaidi ya kugombea ubunge?
Nijibu

safi sana kijana, tunataka watu kama wewe. Tupo pamoja kamanda.
 
nimejidhihirishia kuwa naweza kugombea,kwani mnanikubali

Mkuu mbona hujibu hoja za watu????, au ndiyo unatumika... Nadhani kwa analysis niliyoifanya tangu umeweka uzi huu ni kwamba tabia zako ni za viongozi wa CCM, kwa huwa hawapendi kujibu maswali yanayoulizwa.

Kama si kosei tangu 1995, CDM imekuwa madarakani karatu, je unajilinganisha vp na wabunge waliopita???

Umeshawahi kuwa nani ndani ya Chama au ndiyo unataka kugombea ubunge kwa mara ya kwanza????

Na kama sikosei umesoma UDSM katika miaka ile ya mapambano na Bodi ya mikopo je ulishawahi kufanya nini???

Kama hutayajibu maswali haya na mengine yaliyoulizwa basi WaTZ tutakuwa tumefahamu wewe hufai kuwa Mbunge wa Jimbo ambalo limeitoa TZ katika Ufisadi, na Unyanyasaji wa kutisha.

Vinginevyo Nyinyi ndiyo wale mamluki wa CCM ambao hutumiwa kukidhoofisha CDM.
 
nimejidhihirishia kuwa naweza kugombea,kwani mnanikubali

Mdau,
naamini mpaka sasa umeshajidhihirishia kuwa chama hicho kina wenyewe. Usijitokeze tu ukataka kugombea ukidhani yaliyoandikwa kwenye katiba ndiyo yanayotekelezwa. Chama kinachofuata katiba yake kipo kama hilo ndilo ulitakalo...
 
Nenda Karatu ukatangaze nia yako huko, watu watakupima na kuona kama unafaa zaidi kuliko Mbunge aliyepo sasa watakuchagua au kama utakuwa msindikizaji aka mbeba gitaa, wapigaji wengine; itajulikana pia. Wana Karatu na chama chako ndio waamuzi wa mwisho.
 
Kama hauna undugu na Slaa au Josephine au Mbowe au Mtei au Ndesamburo, sahau.
 
Kama hauna undugu na Slaa au Josephine au Mbowe au Mtei au Ndesamburo, sahau.

kama kagasheki na familia yake,makamba na januari,mwinyi mstaafu na husein,abdalah mwinyi.VITA KAWAWA,RASHID KAWAWA,ZAINAB KAWAWA.
 
KARATU SECONDARY, WANAMATATIZO YA MAJI, ndiyo yakuoga na Kunywa hayo.....Victim ni mi mwenyewe tulivyogoma Wakatupiga Mabomu ya Machozi, sasa sijui wadogo zangu huko hali ikoje

178076_450293108327752_137217764_o.jpg
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom