Nataka kufungua kampuni yangu hapa nchini, nisaidieni haya ili niyatekeleze kwa uelewa mkubwa!

Mkuu, nimeelewa vizuri asante sana. Nimepata fomu ya brela na nimeona ada za usajili zinavyoenda. Ila sipajapata ufafanuz let say kampuni ina mtaji 10Mn kodi za TRA inakuwa ngapi?

kodi ya kupeleka TRA inategemea na faida uliyopata,mtaji na mahesabu ya kampuni yako yatatumika ku'estimate tu hyo kodi,
kwa start up company kama hujaanza biashara bado lakiniTIN ushachukua unawaandikia TRA barua mapema kuwaeleza hujapata faida bado,vinginevyo wanakupiga penalty,so unatoa taarifa mapema
Utakapoanza kupata faida,kampuni inakuwa charged corporate tax ya 30%,inayobaki (profit after tax) ndo yako
Pia kuna kiwango cha kusajiliwa kama VAT trader,yani unakuwa unaikusanyia serikali VAT,hapa ni biashara ikikua hadi kufikia turnover ya 40 mil KWA MIEZ 3,au 10m kwa mwezi kama sikosei,
kama kuna lingine uliza nikiweza nikupe clarification vizuri
 
Wana JF naomba mnisaidie.Nataka kuanzisha kampuni nikiwa Singida,je nifuate hatua gani au niende ofisi gani
 
Hakikisha unaandaa vitu vifuatavyo. Memorandum of understandinh, TIN, LESENI, Jina LA kampuni, vngne wadau wataongezea. Kila lakheri mkuu
 
1. Buni jina la biashara
2. Ingia website ya brela na angalia kama jina hilo limeshasajiliwa - Name search (Kama ni limited company, Jina hilo lazima liwe na neno limited mwishoni. Sijui ni kwa nini lakini sheria yetu ya makampuni ndivyo inavyotaka)
3. Andika barua fupi ya name search kwa mkurugenzi wa mamlaka ya usajili wa makampuni na majina ya biashara (BRELA). Ni vizuri ikapelekwa kwa mkono ili upate majibu kesho yake tu. Unaenda nayo Jengo la ushirika ghorofa ya nne, inagongwa muhuri halafu unaipeleka ghorofa ya sita kwa ajili ya approval
4. Kesho yake unaenda kuchukua majibu, ambapo kama uliisha fanya name search kwenye website yao na ukajua kuwa jina hilo halijasajiliwa na mtu mwingine, manake ni kwamba jina hilo litakuwa approved. Ila mamlaka inasajili jina kwa kirefu au kifupisho chake, usijeandika vyote. Mfano unaweza kusajili either Tanzania Cigarette Company Limited au TCC Limited. Huwezi Kusajili Tanzania Cigarette Company (TCC) Limited
5. Hiyo company name ikashakuwa approved unaandaa Memorandum and Articles of Association. Hizi ni nyaraka zinazosimamia mahusiano ya kampuni yako na watu wengine (Memorandum), na mahusiano ndani ya kampuni yako (Articles). Nyaraka hizo unazipeleka ghorofa ya sita chumba namba 612 ambako wanakupigia mahesabu ya hela unayotakiwa kulipa kwa ajili usajili ya kampuni yako. Kuna stamp duty, registration fees na kitu kingine nimesahau. Malipo hayo yatategemea na mtaji wa kampuni ni shilingi ngapi na idadi kopi ya nyaraka unazopeleka BRELA kusajiliwa (Yaani unapeleka copy ngapi za Memorandum na Articles, na hii itategemea na kampuni itakuwa na directors wangapi). Kwa mfano kama mtaji wako ni milioni kumi za kitanzania, ada zote ni kama laki tatu hivi. Pia kuna form za kujaza ambazo utapewa brela na utaziwakilisha pamoja na hizo memorandum.
6.Ukishapigiwa hesabu ya hela unazotakiwa kulipa, unalipa kwenye account ya BRELA (Mi naijua ya CRDB) halafu unapeleka pay-in slip ya benki pamoja na hizo nyaraka zako BRELA ghorofa ya sita ambapo watazipokea na kukupa risiti yao.
7. Baada ya siku nne za kazi unaenda kuchukua cheti cha usajili wa kampuni yako pamoja na copy zako za memorandum. Unaanza taratibu za kutafuta TIN na VAT certificates TRA pamoja na kufungua account bank.
Kama una maswali zaidi nipim au nicheki whatsapp 0775122255.

Goodluck
 
Kama masiara vile kumbe ndo napata ujuzi...,mi nilikuwa napitapita tu humu mkuu lakini kwa hii simple explaination nimekusoma vyema.

Thanks alot..,ndo faida ya kushare mawazo na ma great thinkers.
 
The law define a company as a fictitious but a legal person that can enter into cotracts,own properties,incur libilities,sue others,be sued by others.The last word of the name of the name of the company should be limited to serve as a reminder to the people dealing with the company that the liability of members is limited,thus in case of financial collapse of a company does not affect the social status and financial position of its shareholders.Nilikuwa naweka point no 2 clear.
 
Wakuu nafungua kampuni, na mtaji let say 4m,,kampuni ya ujenzi...nakunakazi nimepewa ya kusapply material..naweza kukopa benk? Wataitaji nini wanikopeshe?
 
I hope boniface utakuwa umepata elimu kubwa, Kila mdau amejaribu kukusaidia kadiri alivyojaliwa kujua. Unfortunately sisi leo ndo tunaiona post yako, na nadhani utakuwa umefanikiwa katika suala lako. Jambo la msingi kujua hapa ni kwamba, ndani ya jukwaa hapa unapewa road map, ukitaka jambo lako lifanyike kwa standard nzuri watafute wataalam watakusaidia. Suala la kuandaa ,MEMART si rahisi kama watu wanavyokwambia chukua template na fanya edditing. Kuna technicalities nyingi sana katika uandaaji wa MEMART ambazo hata wanasheria ambao hawana uzoefu huo wanazikosea sana. Si tu kwamba MEMART iko katika standard nzuri kiusajili lakini je kiutendaji wa kampuni ikoje? na hapo ndipo wengi wanapochemka.
Lakini jambo kubwa zaidi, watafute wataalam (Business consultant) andaa maswali yako ya kutosha, kaa nao wakushauri kwa mapana na marefu kabla hujafanya chochote. Baada ya hapo utajua nini cha kufanya.
Karibu Anjoa Company Limited kwa ushauri na huduma katika masuala ya biashara kama usajili (jina la biashara, kampuni au NGO). Pia tunatengeneza michanganuo ya biashara na kuandaa mahesabu), Tunatoa ushauri na huduma ya namna ya kuanzisha na kuendesha taasisi ndogo ndogo za mikopo, n.k
Wasiliana nasi: Simu 0759-692024 au 0688510564 au
Email: info@anjoa.co.tz au anjoa_limited@yahoo.com
Au fika ofisini kwetu: Dar es Salaam, Kinondoni Manyanya, Mtaa wa Togo, Tiger tower 2and floor (jirani na Togo tower)
 
Anjoa on tumieni mchanganuo was gharama ya kufanya hiyo kazi had I nakabidhiwa certificate mkonono mwangu nipo mkoani.Tuma hapa madegedenis@gmail.com
 
Wanasheria ndio wanajua trchnivalities za kufungua kampuni,kama utatumia hao wa kinondoni its for your own detriment!
 
Kwenye kufungua kampuni suala la share capital wengi huweka kwa maandishi tu (Norminal Share Capital) lakini ukija kwenye uhalisia katika vitabu vya mahesabu kiwango cha share zilizolipiwa huwa ni pungufu (Paid up Share Capital) athari mojawapo ya kuwa na norminal share capital kubwa ni kulipa pesa nyingi wakati wa usajiri wa kampuni maana Brela wataangalia kiwango cha share capital. Suala la bank kukupa mkopo halina uhusiano wa share capital bali ni dhamana ulizonazo pamoja na mzunguko wako wa biashara inngawa watahitaji kujua wakurugenzi waliopo katika katiba ya kampuni (MEMART). Faida za kuwa na limited company ni kwamba liabilities zinabebwa na kampuni mfano kodi (corporate tax) inalipwa na kampuni na kuna baadhi ya matumizi ya wakurugenzi yataingizwa kama matumizi ya kampuni nimekutajia machache kati ya mengi na uzuri wa limited unao uwezo wa kufanya biashara na taasisi yoyote yenye ukubwa wowote tofauti na sole proprietor.
Sina shaka ulishafungua kampuni yako na inafanya vyema sokoni mpaka muda huu
 
Back
Top Bottom