Nataka kadi ya CCM rasmi

Kwa nini usubiri vibadilike na usiungane nao kuwabadilisha na badala yake unajiunga na CCM unayoita ovyo kuibadilisha. Unasema unawafuata NAPE, JERRY na vijana wengine machachari - hawa wamefanikiwa nini cha kujivunia ndani ya CCM.
Simpo, ukijiunga upinzani sasa hivi utakuwa na kazi ya kuwabadilisha. Ukishafanikiwa kuwabadilisha utakuwa na kazi nyingine ya kuibadilisha CCM. Utakuwa umezunguka sana na kuifanya kazi maba 2. Ukijimwaga CCM moja kwa moja unakuwa na zi moja tu, kuwabadilisha wao, kwisha
 
Burn,

I support and respect your decision. Tunahitaji watu ambao wanakiu kabisa ya maendeleo ya nchi hii kama wewe ambao wako tayari kuthubutu kugeuza mawazo yao kuwa vitendo.
CCM ni chama kikubwa na chenye mtandao mpana wenye wanachama wengi. Kinachotakiwa ni kuhakikisha unakuwa innovative, unajituma vya kutosha, unajenga uhimili wa kutoa ushauri katika ngazi mbali mbali za chama hasa baada ya kufanya researches za kutosha. Kwa vile utakuwa unaingia katika kundi jipya kwako, apply the scientific proven abc steps in forming a workable group ambazo ni Forming, Storming, Norming and Performing. Yeyote anayekwenda CCM kwa malengo ya kuwatumikia wananchi ana nafasi kubwa ya kuwafikia na mchango wake kuwanufaisha walengwa.
Hujachelewa!!!!!
 
Si kweli hata kidogo kuwa CCM ni chafu na inahitaji mabadiliko makubwa hasa kwa watu wasio na vision ya uelewa hali halisi ya nchi yetu na matokeo yake umeinarrow fikra yako kwa kiwango cha ajabu….Kunaweza kuwa kuna matatizo makubwa ccm lakini hakuna taasisi inayoongozwa na watanzania ikawa ni mfano wa kuiga kwa watu wengine.Uongozi uliotukuka kwa mara ya mwisho ulikuwa nchini mwetu dhama za mwalimu.
Hata wakati wa zama za mwalimu bado kulikuwa na viongozi wanafiki ambao hawajawahi kujulikana dini zao kwa kuzani mwalimu alikuwa ni mdini,walificha ideology zao na kujifanya waumini wa ujamaa kumbe ni mabepari wakubwa.Na hili ndio tatizo kubwa la watanzania kutokuwa wakweli hata pale pasipo na umuhimu.
Mimi naamini mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu yatapatikana kwa kuacha kupiga majungu,unafiki na uvivu wa kufanya kazi na ubinafsi,hizi sifa kwa watanzania haziwezi kuondoka kwa kujibadili sisi wenyewe bali kwa kuanzia kuwafundisha watoto wetu wakikuwa wawe ni jamii bora.
Uvivu wetu wa kazi sasa unajulikana Africa ya mashariki yote,hata ukienda baa ukakuta muhudumu wa kitanzania utashangaaa,unamtuma coca moto anakuletea sprite ya moto,akienda kubadilisha anarudi na coca ya baridi,akienda kubadili anarudi bila glass,akifata glass kasahau opener,dk kumi anahudumia meza moja,angekuwa mkenya unaona tofauti hio.Hawa waingeleza waliotutawala waliliongelea hilo dhidi ya watanganyika.
Sio ccm peke yake inahitaji mabadiliko bali watanzania wote kuanzia kwenye familia zetu mpaka viongozi wakubwa.Viongozi hawatoki hewani bali ni zao la jamii yetu na kama jamii ni mbaya hata viongozi wanakuwa ni wabaya pia.Na mtu angejua matatizo ya vyama vya upinzani hapa nchini angeliona akheli abakie CCM.
 
Burn,

I support and respect your decision. Tunahitaji watu ambao wanakiu kabisa ya maendeleo ya nchi hii kama wewe ambao wako tayari kuthubutu kugeuza mawazo yao kuwa vitendo.
CCM ni chama kikubwa na chenye mtandao mpana wenye wanachama wengi. Kinachotakiwa ni kuhakikisha unakuwa innovative, unajituma vya kutosha, unajenga uhimili wa kutoa ushauri katika ngazi mbali mbali za chama hasa baada ya kufanya researches za kutosha. Kwa vile utakuwa unaingia katika kundi jipya kwako, apply the scientific proven abc steps in forming a workable group ambazo ni Forming, Storming, Norming and Performing. Yeyote anayekwenda CCM kwa malengo ya kuwatumikia wananchi ana nafasi kubwa ya kuwafikia na mchango wake kuwanufaisha walengwa.
Hujachelewa!!!!!
Ahsante sana mkuu natumaini na wewe ni mmoja wetu sisi tunaokerwa na hali ya nchi yetu kwa sasa, ndio maana sikutaka kuwajibu wale walio hoji mimi ni nani hadi nikajipa uwezo wa kuibadilisha CCM, wewe ni jibu la uwezo huo kwani naamini ndani na nje ya CCM kuna pundamilia07 wa kutosha kubadili hali ya sasa.Mungu ibariki Tanzania ..Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Si kweli hata kidogo kuwa CCM ni chafu na inahitaji mabadiliko makubwa hasa kwa watu wasio na vision ya uelewa hali halisi ya nchi yetu na matokeo yake umeinarrow fikra yako kwa kiwango cha ajabu….QUOTE]

Hapo ndipo tunapishana mzee, mimi nafikiri kwa zaidi ya miaka arobaini chama kimeshindwa kuwaongoza watu kwenye maendeleo, ushahidi unaonesha wazi kuwa pamoja na vijihatua vidogo kuelekea kwenye maendeleo bado kundi kubwa la watanzania ni masikini na hizi hazikuwa ni fikra zilizoijenga CCM hapo awali..nadhani kwangu hilo ni tatizo kubwa. Hayo mengine ya kudai sijui wa tz ni wavivu ni sehemu tu ya kizazi cha CCM kutaka kukwepa majukumu, kuna tatizo la sera huwezi kutegemea nchi kuondokana na umasikini kwa watu wake kuuza baa kwa bidii.
 
baki huku huku kwa kuandika kama unaona ndio ukombozi kwako, maana kama huna chama andika kuwa mgombea binafsi
 
baki huku huku kwa kuandika kama unaona ndio ukombozi kwako, maana kama huna chama andika kuwa mgombea binafsi

Mkuu hilo la ugombea binafsi sidhani kama litasaidia sana, maana lengo si kuwa na madaraka ila ni kusaidia kubadili mfumo huu, na kwa kuanzia ni hapo kwenye kiini yaani CCM.
 
Back
Top Bottom