Natafuta watu/mtu makini wa kusoma naye Chartered Institute of Marketing CIM-PGD

JF Marketer

Member
Jan 3, 2009
80
34
Ninataka kuchukua kozi ya masoko inayotambulika ulimwenguni katika ngazi ya Uzamili kwa njia ya masafa. Nimepata Kituo kinachoendesha masoma haya kutoka Kenya.

Kwa ujumbe huu, ninawaalika watu/mtu makini anayemaanisha kweli na kujituma kwa dhati kujiendeleza kitaaluma ajiunge nami ili tushirikiane katika kusaka elimu hii. Elimu ya masafa si mkate wa siagi. Inahitaji adabu na utiifu mkuu katika matumizi ya muda. Hii lazima itoke ndani ya nafsi ya mhusika maana hakuna wa kukushurutisha.

Mimi niko Dar na muda wangu wa kusoma ni kuanzia saa 11 Jioni. Pia naweza kusoma katika siku za mwisho wa wiki. Kama upo tayari kujiunga nami basi tuwasiliane:

View attachment Post-Graduate Fee's breakdown-1.pdf

Barua pepe: upegra@gmail.com
 
Wana JF,
Vipi, mbona hakuna jibu?!
Inamaanisha watu hawasomi Jukwaa la Elimu au ni kwamba tunapenda sana Siasa na Udaku!
 
Wana JF,
Vipi, mbona hakuna jibu?!
Inamaanisha watu hawasomi Jukwaa la Elimu au ni kwamba tunapenda sana Siasa na Udaku!

Ndugu tumeiona sio wote tuko kny MARKETING ungekuwa unafanya CFA ningekutafuta!
 
Wana JF,
Vipi, mbona hakuna jibu?!
Inamaanisha watu hawasomi Jukwaa la Elimu au ni kwamba tunapenda sana Siasa na Udaku!

Watanzania wengi hatupendi hayo masomo ya kusomea online.Na hilo tangazo la kutoka kuwa kuna online course Kenya inayotmbuliwa pia linaogofya.Baadhi ya Watanzania i wamelizwa na wakenya kuna watanzania wana maoni kuwa ukiuliza wanaigeria wa Afrika mashariki ni akina nani watakwambia wakenya.Anyway wakenya wana kazi ya kuwadhibitishia baadhi ya watanzania kuwa wao si wanigeria kwenye deals ziwe za kibiashara n.k
 
kingadvisor,

Ni utapeli upo lakini katika hii kozi iliyo chini ya Chartered Institute of Marketing-United Kingdom (CIM-UK) kufanyiwa utapeli lazima kwanza na wewe uwe punguani! Unapojisajiri unalipa ada ya uanachama moja kwa moja CIM-UK. Unachokilipa Kenya ni ada ya masomo kwa njia ya masafa.

Na hiki chuo cha Kenya kimesajiliwa na CIM-UK kama accredited training center. Unaweza kulithibitisha hili kwa kusoma Prospectus zao kwenye mtandao Search results
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom