Natafuta wakili mzuri

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,275
391
Mimi pamoja na familia yangu, tumedhurumiwa ardhi na mwekezaji! Story ilikuwa kama ifuatavyo:
Mama yetu aikuwa na ardhi iliyoanzia barabarani na kwenda umbali wa mita kama 400 hivi hadi kufikia ufukweni. Mwaka 1995 Mwekezaji kutoka australia alikuja na kufanya makubaliano na mama yetu ya kukodoshana eneo.
Baada ya muda huyu mzungu ameweka mawe eneo na anadai ni la kwake ameuziwa na serikali. Kwa sasa mama yetu amefariki na alichotuachia ni karatasi za makubaliano ya kukodishana shamba na mwekezaji na sio kuuza.
Naomba wana jf mnielekeze wakili mkweli na madhubuti ili tupate haki yetu.
Kwani tulishakwenda mabaraza ya ardhi, kwa mkuu wa wilaya lakini kote tumegonga mwamba, jamaa anatoa rushwa na hakuna haki iliyopatikana
 
Nenda Jengo la Ushirika Mnazi mmoja Basement floor utakuta kuna Ofice ya Advocate S.E. Shayo namin atakusaidia! Usitangulize rushwa maana ni mcha Mungu!
 
Nenda pale amani place jengo lililo opposite na movenpick kuna kampuni mbili kubwa za uwakili. Moja inaitwa crb legal na nyingine hii inamilikiwa na wakili maarufu muhaya anaitwa rwechungura na nyingine inaitwa fb attorneys hii inamilikiwa na muhindi na ina wakili mmoja wa kihaya ambaye pia ni maarufu anaitwa ishengoma lakini pia hapo hapo ipo kampuni nyingine ya uwakili inaitwa exor attorneys ila yenyewe bado ni changa kwa hiyo ndugu chaguo ni lako kwani nina uhakika watakuwa na msaada mkubwa kwako kama ukiwa kweli uko serious!
 
Back
Top Bottom