Natafuta spare za ford escape/mazda tribute

dommidee

Member
Aug 17, 2008
18
1
Wadau habari zenu,
Natafuta spare za ford escape, kwa mtu anaejua zinapatikana wapi au alienazo naomba anisaidie.
Natafuta shockups, clutch plates,
 
Kuna mama ana duka la spare za mazda na ford pale tabata. Kama unatoka ubungo, ukishapita mataa yanayokwenda tabata, endelea kama unaenda buguruni angaliaa upande wa pili wa barabara yaani unaotoka buguruni kuja ubungo, utaona kuna kituo cha basi na nyuma/pembezoni mwa hicho kituo kuna duka kubwa la pale blue limeandikwa mazda na ford... Unaweza kupata au kumuagiza akakuletea ndani ya muda mzuri...ila ana bei sana... Anasema vitu vyake vyote ni genuine... (Sina uhakika na siwezi kuthibitisha) japo binafsi nimeshanunua air cleaner ya Mazda MPV...
By the way, hiyo tribute ni auto au manual? Vipi unaweza kunipa mrejesho wake kidogo, kwani nafikiria kuichukua 2.0 manual...ila nikifikiria spare ndio nasita.
 
Actually mi naendesha ford maverick ambayo ni sawa kabisa na ford escape, ni manual 2.0. Ni gari nzuri kwa kweli,nimesafiri nayo sana sema sasa mashock up hayo yananizingua ila asante sana kwa ushauri
 
Waone cmc automobiles, pale opposite maktaba complex, azikiwe. Watakuwa na ufumbuzi.
 
mkuu ulipata spare kwa huyo mama buguruni? na Plan kuagiza Ford escape 2.0 lakini naogopa ishu za spare parts..vipi kwenye ishu ya service oil filter zinaingiliana na gari zingine?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom