Natafuta shule kwa Mtoto wa Miaka 3 (Boarding)

Hapana. Hii kitu haijakaa vizuri.
Huko ni kutaka kutaka kumwaribu mtoto wako.
Ushoga, Usengee, usagaji nk huwa unatengenezwa kuanzia utotoni pia. Boarding school mpeleke mtoto anayejitambua na kuweza kujiongoza mwenyewe. Tusikwepe majukumu kwa kisa cha kuwa Busy, ufahari, pesa nk. Tusilazimishe watoto wetu waishi kama watoto Yatima wakati wazazi wao wako hai.

Hivi ni mtoto gani mdogo anayependa na kujisikia furaha akiwa mbali na wazazi wake wazuri anawapenda?
 
Don't be too judgemental. Inawezekana kuna mazingira yanayopeleka hii kuwa the best option kwa sasa.

Kwangu mimi hakuna best option ya kupeleka mtoto wa miaka 3/4 kwa mtu husiyemfahamu. Sisi ni waafrika na kama waafrika tuna familia kubwa hivyo basi unaweza mpeleka mtoto kwa mama yako, mama mdogo, shanganzi, bibi, babu,kaka, dada, mtoto wa mjomba na au hata kuleta msichana wa kazi na kukulelea mtoto wako cha muhimu mtoto wako utakuwa unamuona kila siku au unampata mtu ambaye unafahamu na ambaye hawezi kumfanya mwanao kitu chochote..
 
Unatumia vigezo gani kukadiria gharama za service kama hii?
Japo nimeingilia hoja isiyonihusu lakini mtoto wa umri huo anahitaji matunzo yenye gharama kubwa zaidi... Kumbuka huyu si mtoto wa kula wali maharage.... na mara kwa mara huyu ni mtoto ambaye umri wake huhitaji uangalizi wa karibu zaidi... usafi wa mwili na mavazi na afya yake ni ya kuangaliwa kwa ukaribu zaidi.... Na unajua vyote hivyo gharama yake si ndogo....
 
Kwangu mimi hakuna best option ya kupeleka mtoto wa miaka 3/4 kwa mtu husiyemfahamu. Sisi ni waafrika na kama waafrika tuna familia kubwa hivyo basi unaweza mpeleka mtoto kwa mama yako, mama mdogo, shanganzi, bibi, babu,kaka, dada, mtoto wa mjomba na au hata kuleta msichana wa kazi na kukulelea mtoto wako cha muhimu mtoto wako utakuwa unamuona kila siku au unampata mtu ambaye unafahamu, ambaye unafahamu hawezi kumfanya mwanangu kitu chochote..
You are right. Huu ni umri ambao mtoto hujifunza kwa sana. Ni hatari kwa mtoto huyu kuadopt tabia za watu usiowajua. Si kila mtu ana upendo kivile... wengi wako kibiashara zaidi.
 
Kwangu mimi hakuna best option ya kupeleka mtoto wa miaka 3/4 kwa mtu husiyemfahamu. Sisi ni waafrika na kama waafrika tuna familia kubwa hivyo basi unaweza mpeleka mtoto kwa mama yako, mama mdogo, shanganzi, bibi, babu,kaka, dada, mtoto wa mjomba na au hata kuleta msichana wa kazi na kukulelea mtoto wako cha muhimu mtoto wako utakuwa unamuona kila siku au unampata mtu ambaye unafahamu, ambaye unafahamu hawezi kumfanya mwanangu kitu chochote..
Tatizo lako umetranslate mazingira ya familia/ukoo wenu na kuassume familia zote zipo hivyo. By the way, best option kwa mtu X sio lazima iwe best pia kwa mtu Y.
 
Hahhahahahahaha Mkuu ni mipango tuu Mwanangu nataka asome miaka Miwili Awali na chekechea baada ya hapo mambo yangu yatakuwa yamekaa sawa! Nitamtoa na kumsomesha Day huo ndo mpango wangu
Acha ujinga wewe.

Hakuna mtu atamtunza mwanao kama unavyomtunza.
Ataachwa na njaa. Ataachwa mchafu. Atapigwa. Atatukanwa. Anaweza hata kuwa sexually abused.
Muache hata kwa jirani anayeweza kusikiwa na watu kama huna ndugu. Kujua kingeereza kusikutoe utu.
 
Habarini Wana JF

Nina mwanangu nataka nimpeleke shule akawe anakaa huko huko ana miaka 3 anaenda mwaka wa nne

Naomba kuzijua shule zinazokuwa zinamfundisha mtoto kingereza kizuri kwa watoto wa umri huo na watoto wanakuwa wanalelewa huko huko i mean bording

Shule iwe Dar Es Salaam na ada isiwe inazidi Milioni Moja na Nusu! Naombeni msaaada
Hembu tafakati umri huo ungepelekwa ukatupwa boarding ungemthamini mzazi wako?Acha kukwepa majukumu mlee mwanao,umri wa boarding ni sekondari
 
Huko ni kutaka kutaka kumwaribu mtoto wako.
Ushoga, Usengee, usagaji nk huwa unatengenezwa kuanzia utotoni pia.
Nina binamu yangu shoga. Anasema alivyokuwa na miaka sita binamu yake alitaka kumbusu. Akamkatalia. Basi toka siku hiyo anapenda wanaume.

Sasa subiri mtoto wake mleta Mada aonyeshwe kupendwa na kujaliwa huko shule ndo aelewe.
 
Inawezekana mazingira yamefosi hiyo hali. Kuna mtoto hapa jirani yangu mama yake kaolewa na mwanaume mwingine na baba yake kaoa mwanamke mwingine. Mtoto hatakiwi pande zote na siku hizi kila ndugu anaangalia family yake tu hakuna anayetaka kujiongezea mzigo.
 
We mzazi timiza wajibu wako. Naomba nisimulie visa viwili tofauti usome uelewe ndipo utoe uamuzi.

Kuna Mtoto wa kike alizaliwa nje ya ndoa. Baba wa Mtoto kwa kumuogopa mke wa ndoa aliogopa kumpeleka nyumbani baada ya mama wa Mtoto kufariki badala yake akamuingiza Shule moja ya Academy hapa Dar, baada ya wiki mbili alipigiwa simu anaitwa Shule kuna tatizo alipofika akakuta kesi watoto wa kindergarten wamemkeketa mwanaye wakati wana cheza. Sasa wote ni watoto wadogo utawafanya nini?

Kisa cha pili ni watoto wa kiume walikuwa wanamtia vidole mwenzao wakiingia chooni.
 
Kwahiyo kila mzazi anaangalia kipozeo kwanza. Mtoto baadae!! Hopeless.
 
Mkuu nimeshafikilia mara kufikilia nimefikia uamuzo huo kama unazijua shule naomba nitajie!

Kweli wewe kufikiria hujui, kama mzazi umeshafeli je mtoto huyo atafaulu. Unataka shule nzuri ya boarding kwa milion tu!!!!
 
Mifano yte hyo umekuwa mbishi ka kitu gani...?! Umri huo ndo wa kumfunza mtot mienendo mema sasa mpelek hko wakamfunze vya kumfunza..!
 
We mzazi timiza wajibu wako. Naomba nisimulie visa viwili tofauti usome uelewe ndipo utoe uamuzi.

Kuna Mtoto wa kike alizaliwa nje ya ndoa. Baba wa Mtoto kwa kumuogopa mke wa ndoa aliogopa kumpeleka nyumbani baada ya mama wa Mtoto kufariki badala yake akamuingiza Shule moja ya Academy hapa Dar, baada ya wiki mbili alipigiwa simu anaitwa Shule kuna tatizo alipofika akakuta kesi watoto wa kindergarten wamemkeketa mwanaye wakati wana cheza. Sasa wote ni watoto wadogo utawafanya nini?

Kisa cha pili ni watoto wa kiume walikuwa wanamtia vidole mwenzao wakiingia chooni.
Yani!!

Mtoto wa dada yangu alivyoanza grade 1,shule ya day, siku akatuambia akiendaga chooni watoto wakubwa wanamwambia ainame wamwangalie huko nyuma. VERY BAD.

Yani kitendo tu cha mtoto kutokuwa nyumbani ni risk. Mtoto asiyejua kujitetea. Bora akae masaa machache, akirudi unamuuliza kashindaje. Mwenzetu ndo anampeleka semester nzima.

Kuna watu katili sana.
 
Back
Top Bottom