Natafuta Rafiki, sibagui rangi, dini wala kabila. PO BOX 11317 ARUSHA. Mnakumbuka enzi hizo?

Pat Gucci

Senior Member
Jun 7, 2011
140
19
Zaman utaftaji wa marafiki ulikua kwenye magazeti tu, sio cku hizi kwenye maFacebook, twitter etc.Hiyo ilikua miaka ya 9O mwishoni wakati huo nlikua mdogo. Kulikua na Mjomba angu alitoa address zake kwa gazeti(jina la gazeti ckumbuki) na kipindi hiyo kulikua hamna cha kuweka namba zako simu wala cha Email sababu hizo mambo zilikua hazijaingia Bongo, kwa hiyo kila cku anapga safari kwenda Posta Office kuangalia barua kama kuna mtu kajitokeza ili wawe marafiki, ila sa hivi ukimuuliza anasema udwanzi! teh! teh! teh! TAIFA LIMEPIGA HATUA...
 
hata ile pia ilikua ni "Hatua" .
Nakumbuka mimi nlikua nawatafuta jamaa wa nje ya Nchi.
Teh teh teh!.
 
na enzi za rafiki wa kalamu (penpal) my bro alikuwa na rafiki wa kalamu mjerumani bro alimtumia vinyago yeye akamletea bro kamera ya picha wakati ule picha zake kubwa zikiitwa 110 halafu black and white. basi bana nikiwa form two mwalimu wetu wa english akatuletea mabarua kibao ya penpal akatugawia mimi nikapata ya mmarekani flani hivi sehemu ya barua nayokumbuka aliandika yeye ni sophomore at Tuolumne University US kwenye hobby anapendelea Heavy metal music bwana weee hapo nikapagawa na u form two wangu wakati ule akina MC HAMMER, naughty by nature, ll cool j, saltn peppa, NWA, RUN DMC wanatamba kinoma nikajua ngoma zao hizo ndo heavy metal music. kwanza nikaandika apart from skul part time nafanya u dj kwenye club nahisi nilipo haribu zaidi ni pale niliposema kwamba i also like heavy metal music, the likes of mc hammer ll cool j yaani sikupata jibu hadi leo jamaa aliona longolongo hiii
 
Back
Top Bottom