Natafuta Rafiki, Mchumba

Msihofu sana jamani kuhusu vigezo, vigezo vyangu havitishi saana kama huyo anayetaka wale wanaotokea Mwanza tu, au yule anayetaka Wangoni na Wachagga tu, au yule anayetaka wenye Kazi zao tu!
Mie kuna baadhi ya vigezo ni vya kujadiliwa na yule aliye tayari kuwa nami, kwa hiyo mwenye vigezo vilivyo vingi kati ya vile ninavyotaka anitumie ujumbe tu, nami nitamjibu bila hiyana.
Mpaka sasa sijapata Pm yoyote.
Still searching.
 
Nakulilia Tanzania,
Naona huenda ikawa kama unavyosema mkuu, maana naona kule kwenye Pm kuko kimya kabisa.
Naendelea kuvuta subira.
 
Nakulilia Tanzania,
Naona huenda ikawa kama unavyosema mkuu, maana naona kule kwenye Pm kuko kimya kabisa.
Naendelea kuvuta subira.

PM yangu bado Kimyaaaaaaaaaa!
Kwamba hawapo wenye sifa hizo ama?
 
Hapa naona kuna hatari ya kununua mbuzi ndani ya gunia. Utafikiri umeuziwa mbuzi lakini kufungua gunia tu kichaa wangu utaona chatu anatokea. Balaa tupu na hapo habaki mtu tena. Rafiki huyo umtafutaye hapatikani kwa staili hiyo. Nenda kawaone wazazi wako wakusaidie kijana kama unaona umri umekwenda.
 
Natafuta rafiki wa kike (girlfriend) wa kubadilishana naye fikra na uzoefu wa mambo mbalimbali.

Wasifu Wangu

* Mfupi kiasi, 5'5 ft, Maji ya kunde
* Umri,miaka 28
* Ni mkristo
* Nina kazi
* Napendelea kucheza mpira wa miguu, kucheza pool table, kuogelea, kuendesha baiskeli, kufanya kazi kwa bidii, kusafiri, kusikiliza na/au kuandaa/kutengeneza muziki. Napenda pia mara chache chache kwenda baharini kupunga upepo.
* Ni mcheshi
* Napenda kujifunza mambo mapya
* Nashaurika katika mambo yenye mantiki.
* Makazi: Dar es Salaam

Ningependelea kupata rafiki mwenye sifa hizi

* Awe na umri usiozidi miaka 30
* Mrefu wa wastani
* Awe mweupe kiasi, (sio weupe wa mkorogo)
* Mnene wa wastani ama mwembamba
* Elimu, angalau kidato cha sita
* Awe mcheshi na mwepesi kujifunza
* Sibagui rangi ya mtu (kwa maana ya Uhindi, Uarabu, Uzungu, Uafrika ama Uchotara)

Mwenye sifa mwafaka anitumie PM kwa kujiamini kabisa, nitajibu bila kusita.
Nashukuru!

Mkuu Idimi

PM yangu bado Kimyaaaaaaaaaa!
Kwamba hawapo wenye sifa hizo ama?

Ningependa kuwa rafiki yako lakini napungukiwa na sifa mbili kati ya ulizotoa... Pole IDIMI!
 
Ningependa kuwa rafiki yako lakini napungukiwa na sifa mbili kati ya ulizotoa... Pole IDIMI!

Zipi hizo zijadiliwe mkuu?
Ziseme, huenda zikawa negotiable!
 
Sifa ya kwanza " umri usiozidi miaka 30''

Sifa ya tano " Elimu angalau kidato cha sita"
 
Sifa ya kwanza " umri usiozidi miaka 30''

Sifa ya tano " Elimu angalau kidato cha sita"

Una umri gani?
Na elimu je? Unaweza kuendelezwa, kama utakuwa tayari, namaindi sana mtu ambaye anataka kujiendeleza kielimu!
 
Tee tee teh,, hatimae mambo yameiva, Idimi huenda akawa amepata rafiki!! hongera Idimi.
Ram, poa sana umempa ndugu yetu ka hope kidogo ..let's hope it will end up well!
 
Halafu useme huna bahati Idimi,umeonyesha ubaguzi wa wazi, hivi kwani marafiki zako wote wapo less than 30 plus na wana vigezo vyako vyote ulivyotoa!! kwi kwi i doubt if you real need a friend or.......kama unatafuta rafiki just tafuta kweli RAFIKI ha ha ha!! good luck man!!
 
Tee tee teh,, hatimae mambo yameiva, Idimi huenda akawa amepata rafiki!! hongera Idimi.
Ram, poa sana umempa ndugu yetu ka hope kidogo ..let's hope it will end up well!
Kwi kwi kwi!
Ram atani-pm, nahisi atakuwa ndiyo mwenyewe huyu!

Halafu useme huna bahati Idimi,umeonyesha ubaguzi wa wazi kwani marafiki zako wote wapo less than 30 plus na vigezo vyako vyote ulivyotoa!! kwi kwi i doubt if you real need a friend or.....

Kwi kwi kwi!
Hapana shaka mkuu, Atapatikana tu, ndio maana nikasema hapo juu kwamba kuna baadhi ya vigezo vinaweza kuwa "negotiable"
 
Hujapata tu mkuu? nasubiri nione kama utapata na mimi niombe.Binafsi nataka wa kike kigoli asiwe ex wa Lyumba
 
Hujapata tu mkuu? nasubiri nione kama utapata na mimi niombe.Binafsi nataka wa kike kigoli asiwe ex wa Lyumba

Kwi kwi kwi!
We binadamu (mtu), acha utani mshikaji!
Akikusikia huyo mwombaji wa urafiki kwangu kwamba unamhisi alipita kwa Liyumba mtashikana makoti!
Bado naendelea na 'negotiations' na huenda mambo yakawa freshi muda sio mrefu. Ila sorry, sitaanika jina lake hapa wala detailz zake zingine, nitasema tu kuwa kapatikana!
Ningependekeza uendelee na maombi ya huyo umtakaye, hapa JF hakuna kitu kinaharibika
 
Hongera za awali mkuu!! kila la heri
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom