Natafuta Nyimbo za zamani za Taarab

mtwangio
chura
nimezamaaa kwa mapenzi
ni bure zenu fitina, si wala hatuzijali
 
Da zamani raha,mpambono wa Hadija kopa na marehemu Nasma Hamis ulikuwa si mchezo, kaona mambo huku taarabu imo,huku uswahili kwetu akina dada/mama wacha watiane vidole.....lakini vya macho ilikuwa burdani sana..
 
Napenda ule ulioimbwa na toti natanga na njia, sijui nitaupata wapi.
 
usichokoze mapenzi, kwani ni khatari sana. wengine hamuyawezi kwa fani hiyo hamna, waloyaanza kwa enzi wapita wakisonona. kiitikio. wako wengi wamekonda ijapokuwa vizungu, kwa kila mwenye kupenda ajue ana donda ndugu. beti ya pili. seuze wenye pumzi na hali zilizonona wakijifanya wajuzi kwa maneno ya kunena wakiyapanda mabenzi na ndege kila aina. ah othman sood na muungano hiyo.
 
Napenda ule ulioimbwa na toti natanga na njia, sijui nitaupata wapi.
Umenikumbusha mbali sana. Nikiwa na umri was miaka 11 nliwahi msindikiza mama sehemu inaitwa Mtupie, Chumbageni basi wee huo wimbo ulikua ukiimba redioni na msusi anaimba kwa hisia nikajikuta naupenda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom