Natafuta msichana wa kusaidia kazi za nyumbani

Natafuta msichana wa kati wa miaka 18-28 wa kunisaidia shughuli za nyumbani.Awe tayari kuishi hapo.Kwa mawasiliano na mazungumzo piga 0784 580 333

Tukiacha utani, siku hizi kazi kidogo kuwapata maana sehemu nyingi (soma Iringa, singida ..) wamejanjaruka wanataka kuendelea na shule. Uzaramuni bado kidogo ujanja haujaingia lakini si wafanya kazi na usafi wao (wa kila kitu) si mzuri sana.
Kuna jamaa alichukua tx iringa baada ya miezi mitatu binti akaitwa kwao akasome.

Lakini kwenye post yako hujafafanua mambo mengi, au ndio ufafanuzi kwenye simu?
 
Hivi una mtaka huyu msichana atoke uku JF? chunga sana usije jikuta unatafuta MKE mwenza ikidhani unatafuta msaidizi...... Na kama una watoto wadogo tafuta HouseBoy tu ila na wewe u jiheshimu kwa huyo HB usije mpa na kazi ambazo siyo zake. kama upo tayari mimi niko tayari kukufanyia kazi zako. kama umeridhika na malezo yangu ni PM tafadhali

kaka kama nakufananisha na shemeji yangu cjui ndo wewe?
 
Tukiacha utani, siku hizi kazi kidogo kuwapata maana sehemu nyingi (soma Iringa, singida ..) wamejanjaruka wanataka kuendelea na shule. Uzaramuni bado kidogo ujanja haujaingia lakini si wafanya kazi na usafi wao (wa kila kitu) si mzuri sana.
Kuna jamaa alichukua tx iringa baada ya miezi mitatu binti akaitwa kwao akasome.

Lakini kwenye post yako hujafafanua mambo mengi, au ndio ufafanuzi kwenye simu?

yaani hapo sifuri ziro kabisa. mambo yao hovyo hovyo sana.
hakuna mzazi anataka mtoto wake aishie kufua nepi siku hz bora aende sekondari ya kata huko basi.........
 
Invisible..... Nilikuwa nikipika cha mchana na usiku daily na mwenye nyumba ( mama yangu) anataka menu itofautiane kula siku!

Kuweka usafi wa nyumba na kumfulia mama mwenye nyumba na vitu Kama ma-bedsheat. Bahati sina ndugu wadogo kwa hiyo kazi ya kushughulikia watoto sikuwa nayo.

Siku ya mapumziko ni weekend lkn either sat or Sunday lazima nimtumikie Kama binti yake na siku moja ilobaki sister aliyekuwa form six anaingia yeye mzigoni

Mwisho wa mwezi bila ya kuulizwa nakatiwa cash yangu mpaka sister mwenyewe ananiomba pesa ya chips shule! Lol

Ninachoweza kusema ni ilikuwa good experience kwangu na ikiwezekana mwanangu pia nitampitisha ktk mgumo huo
 
Mimi haya ya mfanyakazi wa ndani siyataki kabisa. Kamwe sitakuja kuajiri mtu eti awe mtumishi wangu wa ndani. Nguo nafua mwenyewe (nadumbukiza kwenye mashine na kupeleka dry cleaner). Kupika napika mwenyewe au nakula nje. Kusafisha nasafisha mwenyewe. Sasa mtumishi wa nini hapo? Ni matumizi mabaya ya pesa kwa mtazamo wangu.

Kipi ambacho huyo mtumishi atafanya nisichoweza kukifanya mwenyewe? Kama ni muda, ni mambo ya time management tu. I have a can do spirit bana....If I want to I can do it....

Kwanza, kiubinadamu tu najisikia vibaya kumtumikisha mtu.
 
NN.. nadhani kuna kakakusumba kaina fulani bongo bado kwamba ukishaanza kufanikiwa tu basi chores zako za ndani tafuta mtu wa kukufanyia ati hadi kufua nguo! Mtu akishafinikiwa kidogo au hata asipofanikiwa sana lazima awe na mtumishi wa ndani. Why why why? Mimi nimeona hata mtu ambaye ni karani ofisini au mmachinga na yeye anataka kuwa na "mtumishi wa ndani"?
 
kuna hawa watu wanawatafutia watu wasichana wa kazi........0658183619 na 0753141320

Umetaja mchezo wa agencies umenikumbusha mbali sana. Mjini siku hizi watu wanaishi na dili hizi unajua inakuwaje. Anaweza kuunda genge la watu watatu akiwa ni yeye na wasichana wajanja wawili. Kukutafutia anakwambia anamtoa Iringa ulipe gharama za nauli + udalali wake. Anakuletea msichana kweli, anafanya kazi mwezi halafu anapigiwa simu mama yake kafariki Iringa, unampatia nauli na hela za matumizi, ndiyo imetoka hiyo. Ukikutana na dalali anakwambia yule msichana ameamua kubaki kwao kumuangalia baba yake ni mzee sana hajiwezi kwa ubinadamu unakubali na kutafuta mwingine yule anapelekwa sehemu ingine. Yaani kwa mwaka mmoja unakuta mtu kazunguushwa nyumba tisa au kumi. a lot of money hapo.

Cha muhimu ni kutokuwa na house girl kabisa, Kama kuna watu wanaweza anzisha biashara ya kupikia na kufanyia usafi wa ndani watu inakuwa bora zaidi kuita mtu week end anakusafishia ukiwa naye bennet then unamlipa chake anatimua.
 
NN.. nadhani kuna kakakusumba kaina fulani bongo bado kwamba ukishaanza kufanikiwa tu basi chores zako za ndani tafuta mtu wa kukufanyia ati hadi kufua nguo! Mtu akishafinikiwa kidogo au hata asipofanikiwa sana lazima awe na mtumishi wa ndani. Why why why? Mimi nimeona hata mtu ambaye ni karani ofisini au mmachinga na yeye anataka kuwa na "mtumishi wa ndani"?

mkuu...hii mentality ya kibongo huwa inaisha "ukisafiri na kukaa ughaibuni....i mean kukaa/kuishi sio kupita"......najua nitaanza kushambuliwa hapa..BUT IM PREPARED.
 
mkuu...hii mentality ya kibongo huwa inaisha "ukisafiri na kukaa ughaibuni....i mean kukaa/kuishi sio kupita"......najua nitaanza kushambuliwa hapa..BUT IM PREPARED.

Kwa sehemu kubwa uko sahihi kabisa!
 
NN.. nadhani kuna kakakusumba kaina fulani bongo bado kwamba ukishaanza kufanikiwa tu basi chores zako za ndani tafuta mtu wa kukufanyia ati hadi kufua nguo! Mtu akishafinikiwa kidogo au hata asipofanikiwa sana lazima awe na mtumishi wa ndani. Why why why? Mimi nimeona hata mtu ambaye ni karani ofisini au mmachinga na yeye anataka kuwa na "mtumishi wa ndani"?
Hivi kwa sisi tulio na watoto wadogo na tunafanya kazi watoto wetu tuwe tunawapeleka wapi kama tusipokuwa na Msaidizi?
 
Hivi kwa sisi tulio na watoto wadogo na tunafanya kazi watoto wetu tuwe tunawapeleka wapi kama tusipokuwa na Msaidizi?
Ndo nilichotaka kuuliza na mie hapo kwa wenye watoto inakuwaje tena wachanga maana wananza kazi mtoto ana miezi 3 je wafanyeje kama mnasema wasidizi na kupoteza ela?
 
Hivi kwa sisi tulio na watoto wadogo na tunafanya kazi watoto wetu tuwe tunawapeleka wapi kama tusipokuwa na Msaidizi?

case kama hii inaeleweka.....kuna wale hawana hata watoto ndio tunaowazungumzia hapa......
 
Hivi kwa sisi tulio na watoto wadogo na tunafanya kazi watoto wetu tuwe tunawapeleka wapi kama tusipokuwa na Msaidizi?

"Msaidizi"..anyway..shida kwa wale wanaoishi ughaibuni (Ulaya na Marekani) plse wasiwapotoshe ukwli bana . Ukiachilia mbali mazingira mazuri ya kuishi na kupata kirahisi huduma nyingine za kijamii, kuhusu watoto ughaibuni wapo watummishi hao waitwa "Baby sitters, Nannies, chidren cares/minders etc" ambapo wanaangalia watoto kwa mshiko mkubwa tu na ni kazi ya heshima inafanywa na wenye elimu maalumu pia!!.

Achilia mbali pia kuwa wapo wazazi wengi wanafanaya kazi kwa shift ambapo wengine wanaweza kutumia muda fulani kukaa na watoto kwa kubadilisha au unaweza kumpeleka mtoto hata kwa rafiki/ndugu wa jirani wakati upo kazini akashinda huko (hayo hayapo Bongo)!!

Hata masuala mengine kama kazi za ndani, si rahisi sana kukuta mtu anaekaa ughaibuni akawa na familia kubwa inayohitaji majukumu ya mtu zaidi ya mmoja. Hata kupika au kufua ni kama mazoezi tu. Kila kitu kinaendeshwa kwa technolojia . Kama unatumia mashine ya kufulia kama NN, au jiko la Umme kama MMK, au iwapo una kula vyakula vya "super market" kama Ngoshwe..haihitaji kuwa na mtumishi wa ndani.

Nyumbani kazi za ndani ni nyingi sana..kama unatumia jiko la kuni, unahitaki mtu wa kutafuta kuni, ukitumia mkaa..mtu wa kununua mkaa na mafuta ya taa kila kukicha..watu wanafanya kazi mbali na nyumbani, usafiri unasumbua..unachelewa kurejea kupikia familia (watoto)..ukirejea pengine umeme hakuna..mboga hakuna, maduka wamefunga ...maji ya kupikia chakua hakuna ...nk nk. Hayo yote mtumishi anaweza kusaidia.

Binafsi naona kuwa na mtumishi wa ndani sio kasumba bali inalazimishwa na mazingira..ila kwa wale wasiokuwa na kazi (mama wa nyumbani) hapo itatia shaka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom