Natafuta mkopo naomba ushauri wenu

emmanuel1976

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
301
79
Kama mjuavyo system ya mabenki yenu juu ya ukopaji ni ngumu sana, hadi uwe na hati ya nyumba au shamba nk. Bahati mbaya mie sina vitu hivi, ninayo mashamba ambayo hayana hati bado, ninao hata mradi wa shule ndogo na nimejenga madarasa kadhaa ila sijapata hati bado na niko hatua karibu na mwisho na kwa hali ya tz huwenda ikachukua mwaka mzima hati kutoka. Nimejaribu kukopa pesa ili niendeshe mradi wangu huu na miradi mingine imeshindikana katika benki zetu za kitanzania. Jamani naomba ushauri wenu, nifanyeje kwani nahitaji kati ya milioni 100-200
 
milion 200??? huna security yoyote! unawaza mbali sana jaribu kureview plan yako uanze kidogo then upande taratibu
 
miradi ninayofanya inahitaji pesa nyingi ila sina hati za mashamba, nyumba na viwanja....nafuatilia hati ila nahitaji fedha kwa haraka
 
Je Masha]mba yako na Shule ziko maeneo gani? Kunaposibility unaweza kuitazama ya kupata private investor ukaingia nae ubia..au mkopeshaji binafsi lakini hii riba yake huwa juu sana.
 
milion 200??? huna security yoyote! unawaza mbali sana jaribu kureview plan yako uanze kidogo then upande taratibu

Hapo sasa........na ngumu zaidi ni financial discipline once mkopo ukiingia....hapa ndio wahindi wanatushinda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom