Natafuta miziki hii ya zamani

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Naomba kama kuna mtu anaweza kunisaidia nikapata miziki hii au hata michache ya zamani ambayo nikuwa naipenda sana. Baadhi siijui majina lakini nitaandika mashairi yake:

  1. Nyimbo ziliimbwa na SALNA Brothers ya Tanga, mfano Ufitina, au ule wanaimba ''Nipeni pole miye jamaa, nipeni pole miye, matatizo mengine twajitakia wenyewe alinikuta sina kitu lakini tulielewana.......................nipeni pole.........
  2. Nyimbo alizoimba Fresh Jumbe akiwa New Urafiki Jazz Band: Mfano ule: Kuna maneno nimeyasikia kwa majirani ya kwamba una mpango wa kumuoa mke mwingine, nami nakuchunguza bwana na wala sitachukua hasira............usiniache mpenzi eeh ooh Mary eeh elewa wafitini mama si watu wazuri mamaaa
  3. Nyimbo zote alizoimba Nico Zengekela alipokuwa na ile bendi ya Juma Kilaza (Cuban Marimba??) Mfano Jackie wa Mapendo, Mama Hisani etc
  4. Nyimbo za Marquis kama: Hamuwezi Kunyamaza,
  5. Nyimbo zote za mwisho kurekodiwa na Kurugenzi Jazz Band ya Arusha - chini ya akina Suli Bonzo, Dogo dogo etc
  6. Morogoro ndio kwetu- MADEVERA sound.
Nawakilisha kwenu
 
Mh wacha kabisa umenikumbusha mbali sanaaa najua hapa huwezi kosa naomba ningeze list
1. Rose waua -Kilwa jaz
2. Shida - Mbaraka
3.Msafiri kafiri
4.Edita
5.Baba anna
6.Nalia Machozi
7. Shemeji shemeji - cuban
8.Mshichana wa elimu - kabaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom