Natafuta Mganga wa Kienyeji Aliye Mkweli

Natafuta mganga wa kienyeji aliye mkweli.
Kwanza sijui kwa kumpata, na wala sijui sifa za mganga wa ukweli, ila wale waendao kwa waganga naomba mnisaidie kwa hili.

Shida zangu hasa ni:-
  • kuliteka jimbo la uchaguzi wa kijiji nilichotoka ili nikautwae ubunge wa jimbo hilo.
  • kumtimua bosi wangu hapa idarani maana amekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wafanyakazi wote, anamtumikia zaidi muhindi na anasahau hata kukutetea haki zetu za msingi.
  • awe mshauri wangu wa mambo yajayo na kunisomea alama za nyakati.
Niko tayari kumpa kiasi kinono yeyote atakaye nisaidia kumpata mganga mwenye sifa hizi.

Naomba uanze kusoma Bibilia na kusali sana ili umrudie Mungu wako.
 
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu , amfanyaye kuwa ngao na kinga ya maisha yake.
Yaabuduo sanamu adhabu yao ni motoni,
wapiga ramli ni motoni moja kwa moja.
Mungu akupe jicho la rohoni ili upate ufahamu na kuijua haki na mapenzi yake mungu
 
Mnyakyusa wa ujiji!!!!!!!???????
Bora ungesema kuwa wewe ni mnyamanyafu tungekuelewa.
Maana wamanyamanyafu kwa uchawi tu , wahajambo, hadi wafipa wanawaogopa.
 
mganga wa kweli ni Mungu tu!mgeukie Mungu wako vyote utapata kupitia kwake!
 
sumbalawinyo kaka yangu, acha kuamini nguvu za waganga kwani kuna mganga pekee naye ni yesu


uwe hodari na moyo wa ushujaa, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote ....ndipo utakapofanikiwa sana kila uendako .....na ndipo utakapostawi sana
 
pita morogoro road, pale jangwani kuna kibao cha mganga kutoka naijeria, fuata mshale, natumai utafika unakokusudia...kila la kheri na nguvu za giza...lakini kama wewe ni ccm, mtafute mbunge wako na umuulize yeye alifanyaje?
Si sili umu jamvini utafurahi,na siku utachukia kweli,hii nimefurahi sana
 
Back
Top Bottom