Natafuta mchumba wa kuishi nae maisha ya ndoa (mke)

Apr 3, 2011
27
13
Wapendwa akina dada wa Jf na wana MMU ( LOVE Connect), poleni na pilika za hapa na pale.

Mimi najitokeza hapa kwa lengo la kutafuta mchumba (binti ambaye yupo very serious) mwenye nia thabiti kama yangu - kutaka kuishi maisha ya ndoa.

A: SIFA ZANGU.

1. Nina miaka 33, Elimu yangu ni ya chuo kikuu.
2.Mkristo wa Romani Catholic,
3. nimeajiriwa serikalini, na naishi mkoa wa ruvuma (Songea mjini).
4. Namshukuru mungu kuwa kipato changu kinaniwezesha kuyamudu maisha vema.

B: SIFA ZA MCHUMBA (BINTI NINAYE MTAKA).

1. Awe na umri usio zidi miaka 30.
2. Asiwe ameolewa na kuachika au kuzaa mtoto before.
3. Awe na elimu AT LEAST kidato cha nne, with a Certificate in hand (Minimum division four pts 28).
4. Sibagui dini, kabila wala rangi.
5. Awe mtu anayejipenda, msafi, anayependa usafi muda wote, anayejiheshimu na kuheshimu watu wengine.
6. Awe tayari kuishi popote pale nitakapokuwa nafanyia kazi (not to be far with me).
7. sio lazima awe ameajiriwa au kuwa mfanyakazi, ninachohitaji ni mke mwema mwenye upendo na amani.

NB: Hakuna binadamu ambaye ni mkamilifu kwa vitu vyote, hivyo kama kuna mtu atakuwa interested nami basi naomba tuwasiliane kwa njia ya PM, au kama hawana access na PM basi aniandikie barua pepe : brown.plus@yahoo.co.uk


Nawatakia kazi njema na mungu awabariki kwa yote mema.

Lumecha Orijino
 
Songea yote hujaona mwanamke anayekufaa ukamuingia uso kwa uso? Au tatizo lako ni uhaba wa msamiati? Kuomba mwanamke alete maombi kwako ni sawa na kumuomba akutongoze. Kuwa jasiri.
 
Usijali utapa aliye mbora kwako na mungu pia,muombe yy aliye juu atakupa lililo jema.usiumizwe na maneno makali ya baadhi ya wanajamii.
 
Ur wrong hata kwenye msiba,au vita watu wanakutana na kuwa wapenzi.sembuse kwenye jamii mtazamo wako sijaukubali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom