Natafuta mchumba wa kihangaza

silie

Member
Sep 1, 2011
14
2
Heshima yenu Wana JF,
Natambua penye wengi hakiharibiki kitu,mimi nimebahatika kupata elimu ya chuo kikuu na Mungu amejalia nimemaliza degrii ya pili na sasa nafanya kazi.Kipato changu ni cha kwaida nikimaanisha naweza kuyamudu maisha ya hapa na pale ndani ya jiji la Dsm.Tatizo langu ni moja, tangu nasoma nimekuwa busy saaana na shule nikasahau kuwa mke wa kuoa inabidi kumwandaa mapema.Nasikikitika kuwa nilijisahau katika hilo na sasa nakimbilia miaka 33 na sikuwahi kuwa na angalau girlfriend. Kwa kifupi nilikiwa kishule zaidi.

Bahati mbaya shughuli zangu zinanifanya niwe busy karibu masaa mengi na sipati mda wa kujichanganya na washikaji ili nifahamiane na madada, si mnajua tena umhimu wa exposure.Jamani natafuta msichana mpole, mwenye heshima anayewajali watu na kuthamini utu kuliko vitu maana anaweza kupenda mafanikio yangu na si mimi,awe na elimu nzuri angalau diploma, akiwa mwalimu au mwalimu mtarajali itapendeza zaidi, asiwe mhuni (amuogope na kumchaMungu), mimi namuogopa na Kumheshimu Mungu, natoka Ngara, jamani, chonde chonde tusaidiane katika hilo. Awe tayari kupima afya yake na kujishughulisha katika shughuli za uzalishaji nje ya ajira.Kwa yeyote aliye tayari tuwasiliane katika email ifuatayo (nzomwi11@yahoo.com), email zote zitajibiwa.Awe na umri usiozidi miaka 25. Asanteni saaaana
 
Wasifu wako vipi. . . . ?
Tuwekee picha tutume maombi.

Aunt Lzy vp tena..mwanaume picha ya nini?sura kwa mwanaume haicount cha msingi siyo disabled,try it...jump,jump and jump over the move
 
Aunt Lzy vp tena..mwanaume picha ya nini?sura kwa mwanaume haicount cha msingi siyo disabled,try it...jump,jump and jump over the move
Muhimu aiseee. . .
Nataka tukiwa na watoto wawe mahandsome na mapretty girls.
 
Ina maana miaka 33 ujawahi kuwa na g friend,ulikuwa unajichua?kwanini email yako ni nzowi?maana yake nzowi...ukiongeza erufi kidogo,utaleta maafa <kuua>kwa huyu mke! Kwakuwa wewe ni muangaza,basi mtaendana kwani madada wa ngara kwa bia halewi.email hii badiri kabsa,mke aliyesoma akijua utomuoa
 
sasa siku zote uko buz na shule ona sasa huna hata experience undhani kuna mdada atakae kubali hapa,ka hukuwahi kuwa na girlfriend experience utapata wapy.
 
Mwiliweeee.....,Jaribu kujichanganya na watu maana ndiyo ulishahamua. Tembelea hostel mbalimbali mfano Mabibo Hostel na kujichanganya kwenye matamasha mbalimbali. Kumbuka mtaka cha uvunguni sharti ainame.
 
Ina maana miaka 33 ujawahi kuwa na g friend,ulikuwa unajichua?kwanini email yako ni nzowi?maana yake nzowi...ukiongeza erufi kidogo,utaleta maafa <kuua>kwa huyu mke! Kwakuwa wewe ni muangaza,basi mtaendana kwani madada wa ngara kwa bia halewi.email hii badiri kabsa,mke aliyesoma akijua utomuoa

maswali mengi yanini?we kama umevutiwa apply!
 
sasa mkuu unataka wa kutoka Rulenge au bugufi?
Labda kukusaidia tafuta likizo uende ngara. halafu utembelee soko la Mgoma,mkadunduli na Rusumo. siku za jmos nenda rulenge sokoni ndo utawapata kilahisi.yaani itakuwa live interview.
wapo wahangaza ambao ni asili ya wahindi nenda pale kabanga na muhweza. ukitaka walefu nenda nyamiaga na murgwanza. ukitaka wenye tabia za kizaramo nenda kashalazi K9 na benaco. lakini watoto poa wapo kuanzia buhororo hadi kanazi. chaguo ni lako. mia
 
nilidhani sunshow anataka kukkusaidia maaba alitangaza abataka mchumba pia;; mzee ukagowez, ulidhani maisha ni shule tu; nina dada wengi wa nyumban ntakusaidia
 
Wana JF,
Hakika nimekubali humu ndani ndo kuna mawazo tele yanayojenga.Nawashukuruni kwa wote mliotoa mawazo ya kunijenga,hakika nitayafanyia kazi na inabidi kweli nijichanganye ili nimpate wa kuoa.Lakini zaidi ya yote tuombeane maana mke wa kuoa, si mke tu katika familia, bali ni mlezi na mshauri pia.

Na hii ndo inayojenga familia bora yenye kufurahia maisha milele yote.Mzidi kuniombea na kwa wale wanaoweza kuwasiliana moja kwa moja, tumia email nzomwi@yahoo.com.Email zote zitajibiwa. Ni kweli picha ni mhimu lakini.....mhuuuuu!!acha kabisa.Picha itatolewa kwa yule atakayekuwa interested ili tuweze kulisogeza gurudumu la maisha haya yaliyobaki.
Nawashukuruni sana tena sana
 
Back
Top Bottom