Natafuta kiwanja maeneo ya

Livanga

JF-Expert Member
Apr 15, 2010
469
148
Bagamoyo road goba to mbezi ya kimara road kigamboni mbezi to kinyerezi road
 
Unatafuta kiwanja cha ukubwa gani, kiwe na hati au squata tu itakutosha, kiwe umbali gani kutoka barabarani? Unaweza kugusia bajeti yako ni kiasi gani, kuna viwanja vya kutosha Kigamboni, kuanzia 4m mpaka 50m kulingana na uwezo na mahitaji yako!
 
Mkuu unataka kujenga nyumba ya kuishi,kanisa au msikiti?mimi ninacho lakini nitakiuza kutegemeana na matumizi ya mtu?
 
Nauza kiwanja changu.

Wapi?
Kimara Mavurunza. Kilometa mbili kutoka Kimara mwisho.
Ukubwa? mita 28 kwa 26
Bei?
milioni 15
Sifa zingine?
. Umeme upo
. Barabara ipo mpaka kiwanjani
. Ni sehemu ambayo tayari kumeshajengeka
. Usafiri wa daladala upo
. Ni karibu sana sana na barabara kubwa
. Hakuna dalali
Mawasiliano? 0782 230159
 
Nunua kiwanja maeneo ya Mbezi kwa Msuguri (Temboni, Msingwa) na Kinyerezi-Kifuru, Dar es Salaam.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na ndugu Oswald Sh. Richard kwa simu namba :
00255784342632 au +255767342632
E-mail : cosiastore@yahoo.fr

1. Kiwanja cha kwanza kipo Mbezi kwa Msuguri, umbali wa kilomita tatu toka barabara ya Morogoro. Kiwanja hiki kipo kando ya barabara ya Msingwa ambayo ni ya changarawe na inapitika. Kina mita 30x40, pia kina nyumba ya vyumba viwili na baraza mbili. Nyumba hii ina umeme. Pia maji yanapatikana mita mia tatu toka kiwanjani. Bei yake ni Tshs. 55 milioni.

2. Kiwanja cha pili kipo Mbezi kwa Msuguri pia. Kuna umbali wa km 2 kutoka barabara ya Morogoro. Barabara ya kuelekea kiwanjani (maeneo ya mtaa wa Temboni) ni ya changarawe na inapitika. Kina ukubwa wa 1350M[SUP]2 [/SUP]
Kimepimwa na hati miliki yake ipo mbioni kutoka. Pia kina uzio wa waya. Bei yake ni Tshs. 60 milioni. Kuna maji umbali wa mita 200 kutoka kiwanjani. Umeme upo.

3. Viwanja vingine vipo eneo la Kinyerezi-Kifuru, umbali wa kilomita 1 toka barabara ya Kinyerezi-Mbezi. Hivi vipo viwanja 14. Vina ukubwa usio sawa.Vipo vya mita 22x25, 20x23, 27x23 na 20x20. Bei zake ni Tshs. 7 millioni kila kimoja. Eneo hili limefikiwa na mradi wa Serikali wa kuwekewa umeme, na wameshaweka nguzo ila bado kuweka nyaya na hatimaye kukamilisha mradi. Maji ya uhakikika kwa sasa ni kama umbali wa kilomita 2.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom