Natafuta kanisa la kiroho

Chokochoko

JF-Expert Member
Oct 15, 2011
438
183
Ndugu zangu wana MMU mie ni mgeni kidogo hapa dar natafuta kanisa la kiroho la kwenda kuabudu, kutokana na tuhuma zinazoendelea ambazo sio nzuri kiukweli kuhusu haya makanisa nimekuwa nikijiuliza kila siku kanisa lipi niwe naenda . naombeni kwa wote wanaoyaelewa haya makanisa anijuze
 
Unaishi maeneo gani?
Na staus yako kifedha ikoje?

Maarufu hapa dar
kakobe - walofulia(sinza, karibu na mlimani city)
mwingira - middle klasi(Mwenge???)

kuna fernandes- civilised, sijui location

mzee wa upako - mixer(Ubungo kibangu)

Mch, Mh, Dk rwakatare - matawi ya juu(mikocheni)
 
kuna wale wa ubungo kuelekea kimara, wamejikita kwenye kuumbua wachawi, ukivuka Tanesco ubungo kama unaenda kimara.
 
njoo kanisani kwetu jumapili mchungaji alituombea wote tutakuwa na magari mapya yeye tayari keshanunua range-rover,,,au unataka kanisa la aina gani mkuu???
 
la pdidy-liko mbweni ntakupa mwekahazna kama huna degree ya mahesabu
 
Je wewe umeokoka?...kwanini unahangaika na tuhuma za wamataifa badala ya kumwuliza Roho?...hujui roho ya mpinga Kristo iikazini...hao watunga tuhuma unamjua Mungu wao?...soma Yoh.mt 4.
 
Je ulikuwa unasal wapi kabla?? Makanisa sio ishu ,swala ni kuwa na knowledge of word of God. Stay where u are uzma wa milele umo ndani yako.
 
SLOAM - MBEZI MAKONDE kwa NABII ELIYA ila ujiandae kuacha yote yanayokuponza kufanya dhambi. Mungu akutatangulie

Misa ni kila siku saa 11am - 12am ya pili saa 12am - 1am asubuhi zaidi ya hapo kuna maombezi na cancelling siku nzima mpaka saa kumi jioni tena kuna misa mpaka saa mbili usiku. Kauli mbiu yao ni soma neno tenda neno.

Mimi nategemea kuanza kesho 25/1/2012 karibu utafunguliwa
 
sloam - mbezi makonde kwa nabii eliya ila ujiandae kuacha yote yanayokuponza kufanya dhambi. Mungu akutatangulie

misa ni kila siku saa 11am - 12am ya pili saa 12am - 1am asubuhi zaidi ya hapo kuna maombezi na cancelling siku nzima mpaka saa kumi jioni tena kuna misa mpaka saa mbili usiku. Kauli mbiu yao ni soma neno tenda neno.

Mimi nategemea kuanza kesho 25/1/2012 karibu utafunguliwa

umesahau shika neno
unaweza tenda neno ukalisahau bana lazima ulishike nalipenda lile church sana ana msimamo wa kweli
ingawa wadhambi wanakaaga wanakimbia wakichomwa na mafundisho kisa wanadai jamaa anawasema wao wakati ni moja ya maombezi
 
umesahau shika neno
unaweza tenda neno ukalisahau bana lazima ulishike nalipenda lile church sana ana msimamo wa kweli
ingawa wadhambi wanakaaga wanakimbia wakichomwa na mafundisho kisa wanadai jamaa anawasema wao wakati ni moja ya maombezi

Kumb; ukienda sloam uwe tayari kubadili jina lako ndo ufunuo wa mchungaji wao
 
mmenichekesha sana jaman loh!ilikuwa nimechoka najisikia ovyo ovyo but nimecheka saaana na kwasasa niko poaaaaaaaaaaaa
JF is never boaring!!
 
Hata usipoenda Kanisani!
We baki na IMANI yako ya ubatizo!
Ila usisahau kutoa sadaka popote pale uwapo!
Kwani IMANI yako itakuponya hakika.

Na ujue ya kwmb hizi majaribu ni mengi sana na ndizo dalili zenyewe hizo ya kuja kwa Mwana wa MUNGU!

Haleluyaaaaaaaa!!!!!!!
Hatuna budi kumtukuza Kirsto Bwana mahala popote tulipo!!
 
Unaishi maeneo gani?
Na staus yako kifedha ikoje?

Maarufu hapa dar
kakobe - walofulia(sinza, karibu na mlimani city)
mwingira - middle klasi(Mwenge???)

kuna fernandes- civilised, sijui location

mzee wa upako - mixer(Ubungo kibangu)

Mch, Mh, Dk rwakatare - matawi ya juu(mikocheni)

....aaaa bana, kweli haya?
 
Back
Top Bottom